Mkapa amkaanga Kikwete

- Karibu sana mkuu, nimekwambia anytime unapohitaji taarabu karibu sana, ninazo kibao on you! ha! ah! ha! ha! ha! vipi kwenye ule mkutano utakuja tena kwa mgongo wa Professor? ha! ha! ha! ha!

Es!

We kweli sasa umechizika na unataka kuweka antention ili watu wasijadili hapa
 
Mbopo:

1: - Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela!

Hii inajulikana kama PREJUDICE. Nani kakwambia wewe una uwezo wa ku-judge? Washitakiwa hata hwajaanza kujitetea wewe tayari unapitisha hukumu? Au kama walivyosema Wakwere wenzako, lazima profesa aende na maji?

2: - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu

Sheria ya kutumia video conference kwenye uendeshwaji wa kesi, na yatokanayo ndio kwanza imepita. Wakati ule ilikuwa bado! kilichojiri pale ni kituko ukiacha ukiukwaji wa taratibu na haki .

Unathubutu kukiri kwamba ulikuwapo pale! Kama umesomea sheria na ukafuzu(?) basi wewe ni walewale wa za chupi. Shame on you

3 (darkred): - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu Wewe mzushi.

Muuzaji wa jengo lile hajawahi kutoa ushahidi wowote. Upande wa mashitaka ulipaswa kuwasilisha ushahidi wa muuza jengo. Hawakufanya hivyo. Badala yake wakatumia mihela kibao kumleta yule Notary Public na kuhakikisha anasema waliyotaka kusikia. Ilipofika zamu ya Utetezi kumhoji, HAKIMU MWANGESI akachomoa.

Ati mda umekwenda sana, ipangiwe siku ingine. Siku hiyo ni ile ya video kwani Papi alikataa kata kata kurudi Bongo. Shahidi wa piili toka Italia, Avvocato Georgio alifariki siku moja kabla ya kujitokeza kwenye video conference hiyo hiyo. Wewe Mbopo, URONGO ni URONGO tu hata upindishe vipi
!

... By the way kwani Mwandosya angeadabishwa kwa kitu gani vile? Anahusika vipi?

.... By the way, DPP alipoenda kwa Mzee Mkapa akimsihi ajiengue kwenye ushahidi alitolewa nje, sawasawa na Mzee Warioba na wengine wote. kwa taarifa yako na wenzako, Mzee wa watu yuko tayari kwenda pale Kisutu hata kuwa in-person badala ya Kamera. Siku hiyo wewe na wazushi wenzako mchimbe.
 
Huhitaji akili nyingi kujua nani ni mkurupukaji kati yetu. Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu. Yule muuzaji wa jengo lile alionyesha kushangazwa na Tanzania kuwa na maofisa ambao wanalazimisha kutengeneza mikataba miwili tean mmoja ambao una-inflate bei ya mauzo na huku Mahalu akikiri wazi kwamba alitaka kujipatia kitu. Na kwa nini ilielekezwa fedha hizo za malipo ziingie kwenye akaunti binafsi ya Mahalu. Fungua macho! Usiingie kwenye mkumbo wa watu ambao wana chuki binafsi na rais na kubeza hata yale ambayo yanafanyika kuwasaidia watanzania. Kwa mwenendo huu hakika kuna haja ya kutangaza wazi kwamba kila aliye na dhamana ya mali au rasilimali za umma sasa ajichukulie tu! Hivi mnadhani Mahalu ni malaika? Ulizeni mtaambiwa. Jiulize kwa nini imechukua miaka hataki kujitetea kama hana hatia na ana utetezi wa nguvu? Hivi tutabadilika lini na kuweka maslahi ya taifa mbele? Kama Kikwete ni mtu wa bifu basi angemwadhibu Prof. Mwandosya. Mbona wanapiga kazi pamoja tena bila matatizo? Acheni kulishwa sumu na huku mnachekelea!

sasa unapoongelea mahalu sio malaika.. wewe unadhani mahalu alikua na mamlaka gani ya peke yake ya kufanya mambo hayo?

balozi anaweza kufanya maamuzi makubwa kama hayo bila baraka za waziri wa mambo ya nje, katibu mkuu mambo ya nje na pengine hata Rais? kama tunataka kumwajibisha mtu tuwajibishe system yote na sio kumtoa mahalu kafara

halafu umeongelea suala la marando kumtetea mahalu ukaingiza na habari za Chadema ndani yake.. hapo unapotosha maana halisi ya kazi ya marando akiwa mahakamani kama advocate na kama mwanasiasa
 
Mbopo:
1(red): - Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Hii inajulikana kama PREJUDICE. Nani kakwambia wewe una uwezo wa ku-judge? Washitakiwa hata hwajaanza kujitetea wewe tayari unapitisha hukumu? Au kama walivyosema Wakwere wenzako, lazima profesa aende na maji?

2 (blue): - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu
Sheria ya kutumia video conference kwenye uendeshwaji wa kesi, na yatokanayo ndio kwanza imepita. Wakati ule ilikuwa bado! kilichojiri pale ni kituko ukiacha ukiukwaji wa taratibu na haki . Unathubutu kukiri kwamba ulikuwapo pale! Kama umesomea sheria na ukafuzu(?) basi wewe ni walewale wa za chupi. Shame on you

3 (darkred): - Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo) wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu Wewe mzushi. Muuzaji wa jengo lile hajawahi kutoa ushahidi wowote. Upande wa mashitaka ulipaswa kuwasilisha ushahidi wa muuza jengo. Hawakufanya hivyo. Badala yake wakatumia mihela kibao kumleta yule Notary Public na kuhakikisha anasema waliyotaka kusikia. Ilipofika zamu ya Utetezi kumhoji, HAKIMU MWANGESI akachomoa. Ati mda umekwenda sana, ipangiwe siku ingine. Siku hiyo ni ile ya video kwani Papi alikataa kata kata kurudi Bongo. Shahidi wa piili toka Italia, Avvocato Georgio alifariki siku moja kabla ya kujitokeza kwenye video conference hiyo hiyo. Wewe Mbopo, URONGO ni URONGO tu hata upindishe vipi!

... By the way kwani Mwandosya angeadabishwa kwa kitu gani vile? Anahusika vipi?

.... By the way, DPP alipoenda kwa Mzee Mkapa akimsihi ajiengue kwenye ushahidi alitolewa nje, sawasawa na Mzee Warioba na wengine wote. kwa taarifa yako na wenzako, Mzee wa watu yuko tayari kwenda pale Kisutu hata kuwa in-person badala ya Kamera. Siku hiyo wewe na wazushi wenzako mchimbe.

ndo maana mwanzo nikasema huyu jamaa anakurupuka na hajui anasema nini.....
 
- Mahalu hawezi kushinda hii kesi, na akishinda ni uoga wa wasimamizi wa sheria na sio CCM wala Rais, maana ukweli upo wazi kwamba hapa kuna wizi umefanyika, ndio haya tunasema kila wakati kwamba waoga ni sisi wenyewe watendaji wa level za chini, halafu baadaye tunalilia Rais na CCM!

- Sasa Marando naye si tulisema kwamba alikuwa kila siku kushinda kwenye ndege ya Rais Mkapa sasa ndio wakati wa kulipia zile fadhila, huku alikilia mafisadi kwenye Chadema! ha! ha! hili taifa bwana!

Es!

tofautisha marando akiwa anafanya kazi za chadema na akiwa wakili mahakamani.....hivi ni vitu viwili tofauti........labda nikuulize ni kwa nini walienda kwa mzee mkapa kumuomba asitoe ushahidi wake mahakamani......dpp na wengine walienda lakini mkapa akaota nje...
 
Ninasubiri ukweli kamili kwa vile sina imani kabisa na maelezo ya Mkapa nasa pale panapohusisha wizi wa mali ya umma
 
Naweza kusema kuwa siasa za ujanjanja na hovyohovyo zimefanikiwa kuifikisha nchi kwenye state of paralysis, from state capacity to political thinking even among the self anointed critical citizens....

Nimejaribu kuisoma hii sijui ni ripoti ama makala kuona ni wapi ama ni vipi Mkapa amemkaanga Kikwete zaidi ya kujikaanga mwenyewe sioni.

Nikiangalaia kwa karibu nakubaliana na Mbopo kuwa huu ni muendelezo wa siasa za ujanjaujanja ambazo sasa zinaelekea kujikita katika mahakama zetu na kugeuza kuwa kama yale majukwaa rasmi na yasiyo rasmi kisiasa ambayo inaelekea kwa baadhi ya wanasiasa kama Mabere Marando, hayajatosheleza kufisadisha siasa za nchi yetu kwa manufaa ya muda mfupi na yale binafsi.

Watanzania wote tumegeuzwa kuwa mashabiki wa ama upande wa Kikwete ama upande wa "Wengine" bila ya kujali jukumu letu la kuweka mbele umakini zaidi ya ushabiki katika kufuatilia, kuchambua na kuzungumzia maswala muhimu ya kuikomboa nchi yetu kama ambavyo tunapenda kujinadi.

Siamini kama ushahidi huu wa kuwa serikali ilikuwa na taarifa na kwamba eti taratibu zote zilifuatwa zingeliweza kuwa ushahidi wa maonevu dhidi ya mshitakiwa katika macho ya washabiki wa upande mwengine ambao unadai kuwa huu ni uonevu na ulipaji kisasi.

Wote hapa tunajua kuwa utawala wa Mheshimiwa Mkapa ulikuwaje, inashangaza kuona kuwa kuna watu wanadhani kuwa Waziri wa wakati ule alikuwa na uwezo wa kukataa kile ambacho bosi wake Rais anataka ama amekubali kifanyike.

Lakini pia inashangaza kuona kuwa usemi wa kuwa ununuzi huo ulifuata taratibu na ulikuwa na baraka zote za serikali unaweza kusafisha uwezekano wa wizi ama rushwa wakati wote tunajua kuwa hata EPA ilikuwa na baraka na utaratibu uliofuatwa.

Halafu huu mchezo wa kukimbilia kuwa kesi kama hizi ni uthibitisho dhana, madai ama shutuma kuwa Rais ana hulka ya kisasi ni ujinga na upumbavu. Haiwezekani watu tupige kelele Rais achukuwe hatua dhidi ya ufisadi na mafisadi halafu anapochukuwa hatua dhidi ya wale ambao hawamo katika listi zetu za kuwachukia ama kuwahukumu kuwa ndio mafisadi basi Rais ndio ageuzwe mkosaji.

Kwa mtazamo wangu, fikira kama hizi ndio zinazowavunja nguvu na kuwafanya baadhi ya viongozi wetu kuamua ama kujiunga na ufisadi ama kuunyamazia huku wakilinda na kuboresha maslahi yao kwani wanakuja amini kuwa hao wanaopaswa kuwapigania ni mabingwa wa kutoa shukurani za punda kwa kuwapiga mateke pale wanapojitahidi kuwatetea na kuwalinda.
Zaidi naamini umefika wakati na ni muhimu kwa Uongozi wa Mahakama zetu kuchukua hatua kuzuia madhubutu kuhakikisha kuwa mahakama zake hazirasimishwi kuwa majukwaa ya siasa za ujanjaujanja na hovyohovyo kama ambavyo imekuwa ikijionyesha katika miaka ya hivi karibuni. Kama kweli hii habari imetolewa na upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Marando ambaye hivi karibuni amekuwa wazi akitumia habari ama sehemu yake katika shughuli za mahakama kufanyia siasa, ni lazima hatua kali zichukuliwe kabla hali hii haijaota mizizi. Inatosha kuona jinsi mahakama zetu zimegeuzwa kuwa kisima cha rushwa na uonevu mwengine, kuruhusu siasa za majukwaani kuota mizizi katika mahakama zetu ni kucheza na hatima ya nchi yetu.
 
Please tupe source za hii information.....napita!!! nikirudi nitachangia kama utakuwa umetekeleza ombi langu.
 
Hii kesi imeisha siku nyingi...Sirikali inatafuta pa kutokea tu!!

Nakubalina na wewe Mwl, hafungwi mtu hapo-tunachoshuhudia ni mchezo wa kuigiza tu! Kesi ya boss wa IMF, Strauss Kahn imechukuwa muda mfupi sana mtu kauipwa lupango kwa tanganyika jeck, bongo tamthilia bado inaendelea leo mwaka wa tano!
 
Please tupe source za hii information.....napita!!! nikirudi nitachangia kama utakuwa umetekeleza ombi langu.

Changia mada wewe, siyo source source weka na wewe akili yako hapa, plz Red one usiseme chanzo ambaye hataki mpaka chanzo akae pembeni sisi tupige mzigo,
 
Naweza kusema kuwa siasa za ujanjanja na hovyohovyo zimefanikiwa kuifikisha nchi kwenye state of paralysis, from state capacity to political thinking even among the self anointed critical citizens....

Nimejaribu kuisoma hii sijui ni ripoti ama makala kuona ni wapi ama ni vipi Mkapa amemkaanga Kikwete zaidi ya kujikaanga mwenyewe sioni.

Nikiangalaia kwa karibu nakubaliana na Mbopo kuwa huu ni muendelezo wa siasa za ujanjaujanja ambazo sasa zinaelekea kujikita katika mahakama zetu na kugeuza kuwa kama yale majukwaa rasmi na yasiyo rasmi kisiasa ambayo inaelekea kwa baadhi ya wanasiasa kama Mabere Marando, hayajatosheleza kufisadisha siasa za nchi yetu kwa manufaa ya muda mfupi na yale binafsi.

Watanzania wote tumegeuzwa kuwa mashabiki wa ama upande wa Kikwete ama upande wa "Wengine" bila ya kujali jukumu letu la kuweka mbele umakini zaidi ya ushabiki katika kufuatilia, kuchambua na kuzungumzia maswala muhimu ya kuikomboa nchi yetu kama ambavyo tunapenda kujinadi.

Siamini kama ushahidi huu wa kuwa serikali ilikuwa na taarifa na kwamba eti taratibu zote zilifuatwa zingeliweza kuwa ushahidi wa maonevu dhidi ya mshitakiwa katika macho ya washabiki wa upande mwengine ambao unadai kuwa huu ni uonevu na ulipaji kisasi.

Wote hapa tunajua kuwa utawala wa Mheshimiwa Mkapa ulikuwaje, inashangaza kuona kuwa kuna watu wanadhani kuwa Waziri wa wakati ule alikuwa na uwezo wa kukataa kile ambacho bosi wake Rais anataka ama amekubali kifanyike.

Lakini pia inashangaza kuona kuwa usemi wa kuwa ununuzi huo ulifuata taratibu na ulikuwa na baraka zote za serikali unaweza kusafisha uwezekano wa wizi ama rushwa wakati wote tunajua kuwa hata EPA ilikuwa na baraka na utaratibu uliofuatwa.

Halafu huu mchezo wa kukimbilia kuwa kesi kama hizi ni uthibitisho dhana, madai ama shutuma kuwa Rais ana hulka ya kisasi ni ujinga na upumbavu. Haiwezekani watu tupige kelele Rais achukuwe hatua dhidi ya ufisadi na mafisadi halafu anapochukuwa hatua dhidi ya wale ambao hawamo katika listi zetu za kuwachukia ama kuwahukumu kuwa ndio mafisadi basi Rais ndio ageuzwe mkosaji.

Kwa mtazamo wangu, fikira kama hizi ndio zinazowavunja nguvu na kuwafanya baadhi ya viongozi wetu kuamua ama kujiunga na ufisadi ama kuunyamazia huku wakilinda na kuboresha maslahi yao kwani wanakuja amini kuwa hao wanaopaswa kuwapigania ni mabingwa wa kutoa shukurani za punda kwa kuwapiga mateke pale wanapojitahidi kuwatetea na kuwalinda.
Zaidi naamini umefika wakati na ni muhimu kwa Uongozi wa Mahakama zetu kuchukua hatua kuzuia madhubutu kuhakikisha kuwa mahakama zake hazirasimishwi kuwa majukwaa ya siasa za ujanjaujanja na hovyohovyo kama ambavyo imekuwa ikijionyesha katika miaka ya hivi karibuni. Kama kweli hii habari imetolewa na upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Marando ambaye hivi karibuni amekuwa wazi akitumia habari ama sehemu yake katika shughuli za mahakama kufanyia siasa, ni lazima hatua kali zichukuliwe kabla hali hii haijaota mizizi. Inatosha kuona jinsi mahakama zetu zimegeuzwa kuwa kisima cha rushwa na uonevu mwengine, kuruhusu siasa za majukwaani kuota mizizi katika mahakama zetu ni kucheza na hatima ya nchi yetu.

Nakushauri utofautishe siasa za maji taka na rule of law and order. Cha msingi hapa kwamba one is presumed innocent until proven otherwise. Furthermore, kale ka-concept, viz: natural justice... right to be heard na zaidi ya hapo kujitetea.

Kama utapenda, soma contents za Power of Attorney which was appended to my fiirst thread. Sasa Mkuu, kwani huko Sirikalini kazi inafanyikaje? Na hapo add the following, where did the money trail end in the whole transaction?? I am giving you a clue, ipso facto, in two names. Fiorela Pagliuca and Ceres SRL of Monaco. One and the same!

By the way, nimemsikia mjomba wenu mmoja msema chochote (siyo MC) alivyokuwa anabwatuka pale Movenpick siku ileee .... huyu Profesa alituharibia sana mipango yetu ya kampeni.. bla bla bla. Ndiyo nakwambia, Profesa kaonewa! Tafuteni Bangusilo wa hilo.
COMING SOON: ANOTHER REPORT
 
Je kama walipika mambo kwa manufaa ya taifa Accounts books zinasemaje?.

Nawashauri wahasibu na wachunguzi watazame financila report za wizara maana wanaweza kusawazisha maneno but ukienda kwenye Cash book za wizara bado zitapingana nao.

Vyovyote vile kwenye hili jengo kuna usanii Awe Mahalu, Awe Mkapa awe JK.
The only problem watu tunaweka ushabiki badala ya kutazama big picture
 
ndio.....uko sawa kabisa...alichukizwa sana na lile neno alilosema mahalu kipindi kile jk ni waziri wa mambo ya nje....akasubiri alipoingia ikulu ndo akaanza kumkaanga pasipo kujua madhara yake sasa mzee mkapa kamwaga yote

Hapo kwenye bold unaweza kupaelezea zaidi mkuu ili na siye wengine tuielewe hii movie kama ni visasi au ni mambo ya kuheshimu utawala wa sheria tu
 
You are better than this! Yaani badala ya nyie kushangazwa na kitendo cha Mkapa kujishushia hadhi yake kwa sababu tu ya urafiki, sasa mnamshutumu Kikwete kwa kufanya kitu ambacho asingefanya mngemlaumu. Sisi wengine tunajua kabisa juhudi ambazo Mkapa alizifanya kuhakikisha kwamba Mahalu hashitakiwi kwa sababu tu ya urafiki wao. Lakini ukweli ni kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani umemuumbua Mahalu na ndiyo Maana Marando na wenzake walihaha sana kukimbia kila mahakama ili Mahalu asijitetee wakati tayayri kuna uamuzi wa kwamba ana kesi ya kujibu.Hii affidavit ya Mkapa ilikuwa itumike kuombe Nolle Prosequi lakini Mkurugenzi wa Mashitaka alipokataa ndo sasa wakaamua kuitoa hadharani ili kutafuta public sympathy, na huyu Marando akawa anatamba kwamba sasa wanaandika barua ya kuomba Kikwete akatoe ushahidi halafu wai-leak kwenye press na kweli wakafanya hivyo. Hivi mpaka hapo hamuoni kwamba kuna tatizo hapa. Tena wanaofanya hivyo ndiyo wale wanaojifanya kupambana na ufisadi (Marando akiwa Chadema) na huku akifanya mambo ambayo mengine ni kinyume na maadili ya taaluma yake. Nchi hii ni ya ajabu sana. Mtu akiwa mwizi wa mali ya umma watu wanamuona kama shujaa na kumpongeza. Hivi kuna nini cha kupongeza hapa wakati profesa mzima wa sheria anafanya forgery ya wazi na ya kitoto ili kukomba hazina ya nchi? Halafu nyie hao hao mnapigia kelele ufisadi mwingine wakati huu wa Mahalu mnauchekea!

Kiongozi, unachozungumza ni kitu ambacho kweli kabisa na ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa.
Binafsi hili la kesi ya Mahalu naona kama maluweluwe tu.
Kuna ukakasi katika hili suala, nipingane na wewe kitu kimoja sio sahihi kwamba tunaweza kumuita Jk shujaa kwa hili, vile vile Mkapa!
Kama akweli Jk ni shujaa, kuna masuala mengi sana yanayofilisi nchi pamoja na ufisadi uliokubuu pia utendaji wa "kishkaji" wa utawala ameenda nayo mbali kiasi gani?
Jk kufikia ushujaa katika suala hili, angelifanya kama muendelezo wa kupigania hayo niliyoyasema.
Sasa Prof Mahalu anabeba ujiko wa "kuonewa huruma" sababu inaleta picha ya "Dr Msabaha na kisa cha bangusiro".... kondoo wa kafara.
Haiwezekani katika dimbwi la mfumo ulijivuruga katika ufisadi wa kupindukia mbele ya serikali iliyokoma kusimamia masuala muhimu na matatizo ya msingi ya WATU na ubunifu leo hii tumuone Rais wake ni shujaa kwa kukapeleka mahakamani kaprofessa kamoja kalikokuwa balozi huko nje, Mkuu Mbopo hii ni sawa???
Je mifumo ya balozi zetu ipoje? Tunauhakika hayajatokea kama haya ya Mahalu huko kwingine? Nini kinafanyika? Kuna maslahi ya nani?
Hata Mahalu akifungwa na hata kunyongwa na kupigwa risasi, katika namna yetu ya usimamizi wa mambo kwa ilivyosasa ni kazi bure na bado itaonekana ni uonevu tu.
Kwa ninavyowafahamu JK ( kama Rais wangu wa miaka 6) na Mkapa (kama rais wangu mstaafu) katika utendaji wao, kwa hili kila mtu kati ya hao mabwana wawili anamaslahi yake wala hamna maslahi ya taifa hapo, tusidanganyane.
 
Back
Top Bottom