Mkapa amkaanga Kikwete

Red one

Member
Apr 22, 2011
99
26
UTETEZI uliotolewa mahakamani kwa njia ya maandishi na Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, imemuweka njia panda Rais Jakaya Kikwete,

Mkapa ambaye ni shahidi wa pili wa kesi hiyo alitoa utetezi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambao unaweza kuandika historia mpya katika mwenendo wa kesi nchini, kupitia kiapo chake ambacho kiliwasilishwa mahakamani na wakili wa mshtakiwa huyo, Mabere Marando.

Duru za kisheria zinasema kuwa utetezi wa Mkapa kwa Profesa Mahalu ambao umepingana na upande wa serikali, utamuweka njia panda Rais Kikwete kwani hawezi kuipinga serikali yake inayoendesha kesi hiyo.
vyanzo vya kuaminika vinaeleza kwamba kabla ya Mkapa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi, zilifanyika juhudi kubwa za makusudi kujaribu kumzuia kiongozi huyo mstaafu kuchukua uamuzi huo.

Chanzo kimoja cha habari kinaeleza kuwa mmoja wa watu ambao walikuwa wakitarajiwa kumfikia Mkapa na kujaribu kumshawishi kuutafakari upya uamuzi wake huo ni Waziri Mkuu mstaafu.

Katika moja ya vipengele 13 vya kiapo hicho, pasipo kutaja jina, maelezo ya Mkapa, yanamgusa moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mmoja wa wanasheria maarufu nchini ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ushahidi wa Mkapa unaonyesha kuwa kila kilichofanywa na serikali yake wakati Kikwete akiwa Mambo ya Nje, kilikuwa sahihi na kilipata baraka za serikali.

“Kama Mkapa anasema kila kitu kilikuwa sahihi, Kikwete ambaye serikali yake ndiyo iliyofungua na kuendesha kesi hiyo, atakapotoa ushahidi wake, atawezaje kumpinga Mkapa, lakini pia atawezaje kuipinga serikali yake mwenyewe?” alisema.

Wakili huyo ambaye alisema anasubiri kwa hamu kuona mwisho wa kesi hiyo aliyoiita ya kihistoria, alisema kama Rais Kikwete akiamua kutoa ushahidi kuitetea serikali yake wakati Mkapa amekwishaiumbua kuna hatari ya kesi hiyo kuibua mgongano kati ya serikali ya Mkapa na ya Kikwete.

Alisisitiza kuwa Kikwete yuko njia panda kwani kama ataamua kuitetea serikali yake, maelezo aliyoyatoa bungeni kuhusiana na ununuzi wa jengo la balozi linalolalamikiwa, yatamweka katika wakati mgumu kisiasa na kisheria.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Agosti 3, 2004, Kikwete alitoa maelezo bungeni kuhusu utata uliokuwapo awali kuhusu ununuzi wa jengo hilo la ubalozi.

Kikwete katika maelezo yake hayo ambayo yako pia katika kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) anaeleza, “Mheshimiwa Naibu Spika mwaka 2001/02 wizara ilinunua jengo la ubalozi counsel katika ubalozi wa Rome katika jitihada za kuondokana na tatizo la kupanga majumba ya watu huko nje na pia kupunguza gharama za kuendelea kulipa pango la nyumba kila mwaka.

“Ununuzi wa jengo hili ulifuata taratibu zote za manunuzi ya majengo ya serikali kwa kuzishirikisha wizara za ujenzi, ardhi na maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Fedha.

“...Jengo lilifanyiwa tathmini na wataalamu wetu na kukubaliana na ununuzi wa Euro 3,098,781.40 Machi 6, 2002 fedha za awamu ya kwanza katika ubalozi wa Rome zilipelekwa nazo zilikuwa shilingi 700,000,000 Juni 28, 2002 zilipelekwa shilingi 120, 000,000.

“Mwishoni mwa Agosti 26, 2002 zilipelekwa shilingi 1,000,000,000 jumla ya fedha zilizokuwa zimepelekwa zikafikia shilingi 2,900,000,000 na baada ya hapo ubalozi wetu ulitekeleza taratibu zote za ununuzi wa jengo na kumlipa mwenye nyuma kiasi hicho cha fedha,” alieleza Kikwete.

Hadi jana, Ikulu ilikuwa haijajibu ombi la wakili wa Mahalu, Mabere Marando, la kutaka afike mahakamani kutoa ushahidi wake juu ya kesi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Marando alisema hawajapata majibu ya Ikulu, lakini pia hawana haraka sana kwani hata mshitakiwa mwenyewe (Mahalu), hajaanza kujitetea.

Marando alisema Katiba haimzuii Rais kuja kutoa ushahidi mahakamani, lakini kama atashindwa anaweza kutoa kwa maandishi kama alivyofanya Mkapa.

“Akishindwa kabisa kuja, basi tutaomba kesi iahirishwe hadi atakapomaliza muda wake wa urais 2015,” alisema Marando.

Gazeti hili lilipowasiliana na Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu, kwa njia ya simu kujua endapo Rais amekubali kutoa ushahidi katika kesi hiyo, hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Kama ilivyokuwa kwa Salva simu ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, ilikuwa ikiita muda mrefu bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, pia hakuweza kujibu swali hilo.

Katika hati ya kiapo chake cha Machi 31 mwaka huu, ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (The Registration of Documents Act, Cap. 117 of 2002), Mkapa anaeleza kuwa kila kilichofanywa na Mahalu kilikuwa sahihi na kilikuwa na baraka ya serikali aliyokuwa akiingoza toka mwaka 1995-2005.

Ushahidi huo wa rais Mkapa umeorodhesha maelezo yake yaliyoainishwa katika vipengele 13.

Mkapa katika utetezi wake huo anadai kuwa mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo la ubalozi lililoko katika mtaa wa Vialle Cortina d’Ampezzo 185 mjini Rome ulizingatia sera ya serikali ya upatikanaji au ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi na makazi na kwamba ulizingatia maslahi ya taifa.

Hati hiyo ya kiapo ambayo tayari wakili Marando amesema ameishaiwasilisha pia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, inaanza kwa kusema, “Mimi Benjamin Mkapa, mtu mzima, Mkristo, mkazi wa Dar es Salaam, ninaapa kama ifuatavyo, ’nilikuwa Rais mtendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viliwili mwaka 1995-2005 na nina uhakika wa yote haya nitakayosema ndani ya kiapo hiki.’”

Katika kiapo hicho Mkapa anadai pia kuwa alifahamishwa na watendaji wa serikali aliyokuwa akiiongoza jinsi mchakato uliofanyika na ripoti za uthamini wa serikali zilizotumika katika kufikia hatua ya kununua jengo hilo la ubalozi.

Anadai kuwa tathmini ya jengo hilo ambalo Mahalu anadaiwa kufanya udanganyifu na wizi kwa kulipa fedha kinyume na ilivyotajwa katika mkataba ambayo ilifanywa na serikali ya awamu ya tatu kupitia wizara mbili tofauti, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi na Maendeleo Mijini.

Anaendelea kudai kuwa anatambua kuwa ripoti ya serikali ya uthamini wa jengo hilo iliandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa kiwango cha dola za Marekani milioni tatu na Wizara ya Ardhi kwa thamani ya euro milioni 5.5.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa wa aina mbili, mmoja ni rasmi na mwingine wa kibiashara na kuongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu ya serikali ya Italia na kuwa hilo lilifanyika kwa baraka za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shahidi huyo wa Mahalu anadai pia kuwa kwa mujibu wa kiapo chake anakumbuka vyema taarifa ya serikali iliyotolewa bungeni Agosti 3 mwaka 2004 iliyosema na kuthibitisha kuwa taratibu zote zinazohusiana na manunuzi ya jengo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali, zilifuatwa na kwamba muuzaji wa jengo hiilo alilipwa fedha zote.

Akimwelezea Mahalu katika utetezi wake, Mkapa alidai katika kipindi chote alichokuwa Rais wa nchi alifanya kazi na mshtakiwa huyo katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma na kwamba mshtakiwa huyo ni mtu wa tabia njema, mkweli, mwaminifu na mchapaji kazi.

Mkapa anahitimisha utetezi wake kwa kueleza kuwa kutokana na mwenendo huo wa kutukuka, Rais wa Italia alimpatia moja ya tuzo za heshima yenye hadhi ya juu kabisa ya taifa hilo Profesa Mahalu, muda mrefu baada ya balozi huyo kuwa ameshaondoka nchini humo.

Katika kesi hiyo namba 1/2007, inayosikilizwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Ilivin Mugeta, Mahalu anashtakiwa pamoja na Grace Martin.

Mahalu na Martin wanatuhumiwa kwa wizi wa sh bilioni tatu katika ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome.

Mapema mwaka 2007, Jamhuri kupitia mawakili wake toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln na Ponsian Lukosi, iliwafikisha mahakamani hapo kwa mara ya kwanza washtakiwa hao kwa makosa ya uhujumu uchumi. Mahalu anakusudia kupeleka jumla ya mashahidi 10.

Mashahidi hao ni mteja wake (Mahalu), Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, kwani wakati akinunua jengo hilo ndiye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ndiye aliyempa nguvu ya kisheria ya kuendelea na ununuzi wa jengo hilo, aliyekuwa waziri wa Ujenzi wa John Magufuli.

Mashahidi wengine ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba ambaye pia anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bil. 11.7.
 
Nyenzo zote wanazo hivyo siyo issue kwa kikwete watachakachua kisheria!!Hapa kwa mtu wakawaida anawezakuona kama ni issue jiulize EPA ikowapi??Kagoda,Meremeta??Je Mchuchuma ilikuwaje je unakumbuka??Tanzania inawezekana kupindisha sheria!!
 
Hii kesi imeisha siku nyingi...Sirikali inatafuta pa kutokea tu!!
 
siku zote ukweli hucheleweshwa ila huja kuumbua aliyekuwa amekumbatia huwo uozo
 
JK mtu wa visasi saaana, sasa yatamgeukia

You are better than this! Yaani badala ya nyie kushangazwa na kitendo cha Mkapa kujishushia hadhi yake kwa sababu tu ya urafiki, sasa mnamshutumu Kikwete kwa kufanya kitu ambacho asingefanya mngemlaumu. Sisi wengine tunajua kabisa juhudi ambazo Mkapa alizifanya kuhakikisha kwamba Mahalu hashitakiwi kwa sababu tu ya urafiki wao. Lakini ukweli ni kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani umemuumbua Mahalu na ndiyo Maana Marando na wenzake walihaha sana kukimbia kila mahakama ili Mahalu asijitetee wakati tayayri kuna uamuzi wa kwamba ana kesi ya kujibu.

Hii affidavit ya Mkapa ilikuwa itumike kuombe Nolle Prosequi lakini Mkurugenzi wa Mashitaka alipokataa ndo sasa wakaamua kuitoa hadharani ili kutafuta public sympathy, na huyu Marando akawa anatamba kwamba sasa wanaandika barua ya kuomba Kikwete akatoe ushahidi halafu wai-leak kwenye press na kweli wakafanya hivyo. Hivi mpaka hapo hamuoni kwamba kuna tatizo hapa. Tena wanaofanya hivyo ndiyo wale wanaojifanya kupambana na ufisadi (Marando akiwa Chadema) na huku akifanya mambo ambayo mengine ni kinyume na maadili ya taaluma yake. Nchi hii ni ya ajabu sana. Mtu akiwa mwizi wa mali ya umma watu wanamuona kama shujaa na kumpongeza. Hivi kuna nini cha kupongeza hapa wakati profesa mzima wa sheria anafanya forgery ya wazi na ya kitoto ili kukomba hazina ya nchi? Halafu nyie hao hao mnapigia kelele ufisadi mwingine wakati huu wa Mahalu mnauchekea!
 
You mean like HASSY KITINE?
 
Je ulishasoma kitabu cha mfalme juha? Tungoje tuone mpambano wa wasanii nani zaidi, afu wanajuana hawa wala wasituchanganyie habari.
 
Kikwete anataka kulipa kisasi kwa mahalu kufuatia kuzinguana wakati JK akiwa waziri na Mahalu akiwa balozi ndo maana alitengeneza hyo kesi,lakini Mungu si John sasa atahaibika mwenyewe na mahalu atapeta,JK ana laana ya visasi
 
Mawakala wa ufisadi utawajua tu! Hata kwa Liyumba na Babu Seya mlisema hivyo hivyo. Nadhani nchi hii imelaaniwa!
 
Kikwete anataka kulipa kisasi kwa mahalu kufuatia kuzinguana wakati JK akiwa waziri na Mahalu akiwa balozi ndo maana alitengeneza hyo kesi,lakini Mungu si John sasa atahaibika mwenyewe na mahalu atapeta,JK ana laana ya visasi

ndio.....uko sawa kabisa...alichukizwa sana na lile neno alilosema mahalu kipindi kile jk ni waziri wa mambo ya nje....akasubiri alipoingia ikulu ndo akaanza kumkaanga pasipo kujua madhara yake sasa mzee mkapa kamwaga yote
 
You are better than this! Yaani badala ya nyie kushangazwa na kitendo cha Mkapa kujishushia hadhi yake kwa sababu tu ya urafiki, sasa mnamshutumu Kikwete kwa kufanya kitu ambacho asingefanya mngemlaumu. Sisi wengine tunajua kabisa juhudi ambazo Mkapa alizifanya kuhakikisha kwamba Mahalu hashitakiwi kwa sababu tu ya urafiki wao. Lakini ukweli ni kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani umemuumbua Mahalu na ndiyo Maana Marando na wenzake walihaha sana kukimbia kila mahakama ili Mahalu asijitetee wakati tayayri kuna uamuzi wa kwamba ana kesi ya kujibu.

Hii affidavit ya Mkapa ilikuwa itumike kuombe Nolle Prosequi lakini Mkurugenzi wa Mashitaka alipokataa ndo sasa wakaamua kuitoa hadharani ili kutafuta public sympathy, na huyu Marando akawa anatamba kwamba sasa wanaandika barua ya kuomba Kikwete akatoe ushahidi halafu wai-leak kwenye press na kweli wakafanya hivyo. Hivi mpaka hapo hamuoni kwamba kuna tatizo hapa. Tena wanaofanya hivyo ndiyo wale wanaojifanya kupambana na ufisadi (Marando akiwa Chadema) na huku akifanya mambo ambayo mengine ni kinyume na maadili ya taaluma yake. Nchi hii ni ya ajabu sana. Mtu akiwa mwizi wa mali ya umma watu wanamuona kama shujaa na kumpongeza. Hivi kuna nini cha kupongeza hapa wakati profesa mzima wa sheria anafanya forgery ya wazi na ya kitoto ili kukomba hazina ya nchi? Halafu nyie hao hao mnapigia kelele ufisadi mwingine wakati huu wa Mahalu mnauchekea!

kijana hujui unalosema unakurupuka tu........
 
- Maneno mazito sana haya mkuu, yanahitaji kuyatafakari sana!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom