Mkapa aitosa CCM, aigomea kwenda Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa aitosa CCM, aigomea kwenda Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Patriote, Mar 9, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  UZINDUZI wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi uliokuwa ufanyike Machi 10 imeingia dosari kubwa kufuatia kukataa kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kufanya kazi hiyo.

  Habariza kuaminika kutoka ndani ya CCM zimedai kuwa Mkapa amegoma kufungua kampeni hizo zilizokuwa zifanyike eneo la Usa River nje kidogo ya jiji la Arusha nakuna habari kuwa uongozi wa juu umelazimika kuahirisha na kusogeza mbele siku ya uzinduzi.

  Ofisa mmoja mwandamizi wa CCM ameliambia Tanzania Daima kuwa Mkapa amechukua uamuzi huo baada ya kubainika kuwa ataaibika kutokana na msuguano mkali wa chini kwa chini baina ya makundi yaliyoibuka tangu wakati wa mchakato wa kura za maoni.

  Mtoa taarifa wetu amesema kuwa Mkapa ametoa sharti zito la kuutaka uongozi wa wilaya, mkoa na taifa kuhakikisha kuwa umeshughulikia kikamilifu msuguano wa makundi hayo, la sivyo hataweza kushiriki uzinduzi wa kampeni hizo. Habari zimedai kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishiria Kaaya, na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa, James Milya, wameitwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili msuguano huo.

  Imedaiwa kuwa wengine walioitwa ni pamoja na wagombea wawili waliokuwa wakichuana kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo, William Sarakikya, na Elirema Kaaya (ambaye aliwahi kushikiliwa na Takukuru akituhumiwa kutoa rushwa kwa wagombea).

  Taarifa zimedai kuwa hali ndani ya chama hicho ngazi ya mkoa ni mbaya pamoja na wagombea walioangushwa na Siyoi Sumari kukubaliana kuwa wataungana pamoja kumpigia kampeni mwezao ili ashinde. Hata hivyo, habari zimethibitisha kuwa uhasama baina ya makundi hayo, lile la James Milya na Mary Chatanda, kwa upande mwingine, yamekuwa katika mvutano wa siku nyingi na kwamba uchaguzi huo mdogo umeibua uhasama huo.

  Alipopigiwa simu kuthibitisha kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa kampeni hizo na ukweli wa kugoma kwa Mkapa, Chatanda alidai kuwa yuko barabarani na akaombwa apigiwe simu kesho (leo). Hata hivyo, alipoambiwa ni jambo la dharura, alikata simu na kuzima.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa, Nape Nnauye, alipoulizwa juu ya kukataa kwa Rais Mstaafu Mkapa, alikana kujua lolote huku akitaka mwandishi amuulize aliyemwambia habari hizi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha, James Millya, hakupatikana na mmoja wa watu wake wa karibu, alilieleza Tanzania Daima kuwa kiongozi huyo machachari wa UVCCM, alikuwa jijini Dar es Salaam kikazi.

  Mkapa aliteuliwa hivi karibuni na makao makuu ya CCM kuzindua rasmi kampeni za ubunge wa jimbo hilo, ikidaiwa kuwa ndiye mmoja wa viongozi wachache wenye uwezo mkubwa wa ushawishi katika masuala ya kampeni. Itakumbukwa kuwa Mkapa ndiye aliyezindua na kisha kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani Tabora, ambako kampeni zake baina ya CCM na CHADEMA zilivunja rekodi kwa mbwembwe, mikikimikiki na tambo za kila aina ikiwa ni pamoja na matumizi makubwa ya fedha.

  Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki unatabiriwa kuwa utakuwa na ushindani mkubwa kati ya wagombea wawili wa vyama vya CCM (ambacho kimemsimamisha mtoto wa marehemu Jeremiah Sumari), Siyoi Sumari, na CHADEMA ambacho kimemteua Joshua Nassari kupeperusha bendera yake.


  Source: Tanzania Daima
   
 2. M

  MR.SILVER JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani ni kutokana na mgogoro ndani ya CCM tu bali pia unaenda kunadi watu wenye tuhuma za rushwa zinazoendelea ni aibu sana
   
 3. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kutakuwa na tatizo zaid mana hawa CCM wana nyuso za mbuzi, hilo kwao sio tatizo mana JK aliwanadi mafisadi bila hata aibu, sioni kwann Mkapa ajifanye ni mgeni na huo utaratibu.
   
 4. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Jamani, jamani, jamani, hii kali...! Mkapa mwenyewe ana zigo la tuhuma, sasa hiyo aibu itoke wapi? Nilidhani ndege wafananao huruka pamoja, yaani hadi nasikia kichefuchefu!
   
 6. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Haya Chadema kazeni buti mwenzenu kiatu kimemvuka
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Sharti ni kuwa kabla hajamnadi Siyoi ni lazma ajibu tuhuma zake kwanza
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wanangu kuweni na hekima. Mkapa hajagoma bali ameogopa aibu. Hivi angeulizwa kuhusu Kiwira, NBC, IPTL na madudu mengi angesema nini? Naona kama CCM imeishiwa watu wenye udhu hadi kumtuma Mkapa mtuhumiwa wa ufisadi hadi wa ufisadi hata wa EPA. Kama AruMashariki wataachana na siasa za kutumiwa, wana wakati na fursa nzuri ya kuipiga teke CCM ili liwe somo kuwa ufisadi haulipi.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Na bado!
   
 10. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Siasa cku zote ni mchezo wa kuotea.a see like chadema wamepata faul ndani ya 18,mkapa hata angekuja huu upepo hawezi kuutuliza.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Mkapa kashajua atazomewa kaona bora ajichimbie tu.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kapa was wise kuchomoa kwanza.... Arusha sio Newala
   
 13. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Mkapa anajua mwenyewe alichosema na kufanya kule Akeri wakati akizindua shule ya sekondari ya Akeri. Hawezi rudi saa hii
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  aende nape nauye kwa niaba ya mkapa
   
 15. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Si walipeke lile zee lao wanalolitumiaga kwenye kukata utepe.
   
 16. aspen

  aspen JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  yani juzi tu wamemtosa nec leo wanamtaka akazindue kampeni .
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Sio kweli, kama Mkapa amekataa kuzindua kampeni, hizo tarehe zitakuwa zimeingiliana tuu na ratiba zake kwa sababu ndani ya CCM rushwa is the order of the day!. CCM sio tuu inanuka rushwa bali ni imeoza kwa rushwa mpaka inatoa uvundo na la kuvunda siku zote halina ubani!. Kama kawaida wanaousikia huo uvundo wa rushwa, ni wale walioko nje ya CCM tuu!, kwa wana CCM wenyewe, pua zao zimeisha zoea hiyo harufu na hawaisikii kama unavyopita maeneo ya Feri, unapokelewa na harufu ila ukikaa kidogo tuu pua zinaizoea na huisikii tena!. Wenyewe wa Feri, hawaisikii kabisa!.

  Ila pamoja na uoza wote huu wa rushwa huko CCM, matokeo ya uchaguzi huo ni mashindano kati ya udhalimu na uadilifu, uchafu wa rushwa vs usafi wa dhamira, ufalme vs ya demokrasia ya kweli, ukoloni wa kutawaliwa kifkra vs ya ukombozi wa kweli!. Nawahakikishia udhalimu, uchafu wa rushwa, ufalme, ukoloni wa kutawaliwa ki fikta ndio utashinda!. Naisubiri April 2 kuwathibitishia hili!.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  utakosa ile kazi bro... shauri yako!!
   
 19. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Pamoja na tuhuma za BWM zinazojulikana na wasomi na wanaopenda kujisomea (kumbuka kwa Tz kundi hili halizidi 3), miongoni mwa Watanzania wengi jamaa anabaki kuwa ni turufu kichwa kwa ccm, Kwa muda sasa hali ya maisha tangu BWM ameondoka imebadilika sana na hasa suala la mfumuko wa bei tofauti na kipindi cha Mkapa ambapo bidhaa hazikuwa zinapanda kiholela.
  Sisi ndo watanzania na tunaishi kitanzania, Mkapa akijitokeza tegemea makubwa.
  Japo sina uthibitisho, (mwanzoni alikataa) kitendo cha BWM kufunga kampeni za JMK pale Jangwani kulikuwa na maana kubwa sana katika kufanikisha ushindi wa mtawala wetu.
   
 20. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Kumbe kuna harufu, nipo maeneo muda huu, na wala sijasikia magogoni wanapuliza uturi kwa kukerwa na harufu ya Feri, ha hahha, 'naelewa mazoea yana taabu..................'
   
Loading...