Mkapa aenda Uswisi kuongoza kikao

Mkapa aenda Uswisi kuongoza kikao

hakika mkapa ni kichwa,nina wacwac na jk kama atapata fursa kama hii,mpaka sasa afrika tnao marais wastaafu wawili wanaoheshmika na hawa wenzet weupe/un ni BEN MKAPA NA THABO MBEKI,UKIACHILIA MBALI WATANGULIZ WAO MWL NYERERE NA KWAME NKHURUMAH,jk jfunze sasa kwa mzee wetu ben
 
Si Mkapa wala JK anayejiita Dr. Kina wajinga fulani ambao wanafikiri JK atawapa mambo fulani na hiyo wanapenda kumuita Dr na kmfurahisha. Na ukweli ni kwamba anafurahi. Mkapa kwa upande mwoingine anaitwa Dr na anapenda. I la sasa hana fursa ya kuitwa hivyo (Dr. ) sana.

Mkapa keshatunukiwa u Dr. ila alikataza waandishi wa habari kumwita hivyo na toka kawakataza sijaona hata sehem moja akiwa refereed kama Dr. Utakumbuka baada ya hapo walianza kujipendekeza kwa kumwita Mtukufu Raisi, akawakataza na kuwaambia anayestahili kuitwa mtukufu ni Mungu pekee.
 
Hili ni product ya Mwalimu!iko fit, pamoja ma mapungufu - mana hata maiti huzidiana kunuka!

Mwalimu alisafiri trip nyingi duniani baada ya kustaafu Urais kuliko alipokuwa Rais kwa miaka 25! Mkapa naye anafuata nyayo!Kama ukifuatilia bios za hao past chairmens utaona kuwa huko hawauzi sura, inapandisha profile ya nchi yetu!

Je mwinyi? Na itakuwaje kwa JK akistaafu?!Tumwombe Mungu atupe maisha kujionea!

EXcellent. Well done.
 
natamani apewe nchitena,maana alipata kunena kuwa akipewa nafasi nyingine atsahihisha makosa yote
 

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th January 2012 @ 15:00

RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, anatarajiwa kuondoka leo nchini kwenda Geneva, Uswisi ambako ataongoza Mkutano wa 28 wa Bodi ya Kituo cha Kusini ambacho yeye ni Mwenyekiti wake.

Kituo hicho kinachoundwa na nchi 52 zinazoendelea, kilianzishwa mwaka 1980 chini ya uenyekiti wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msaidizi Binafsi wa Rais huyo mstaafu, Malago Malagashimba, Rais mstaafu pamoja na kuongoza mkutano, pia atashiriki katika mkutano wa 13 wa Baraza la Wawakilishi la Wajumbe wa Kituo hicho, sambamba na mkutano wa kituo utakaozungumzia hali ya kiuchumi duniani.

Mara kadhaa, Chifu Emeka Anyaoku ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola amekuwa akimwelezea Mkapa kama Mwenyekiti aliyefufua moyo wa Mwalimu Nyerere katika maendeleo ya kituo hicho.

Mkapa ambaye ni Mwenyekiti wa Tano wa Bodi ya Kituo hicho, baada ya shughuli hiyo nzito, anatarajiwa kurejea nchini usiku wa Februari 4, mwaka huu.

Wengine ambao wamewahi kuwa wenyeviti wa Bodi ya Kituo hicho ni Luis Fernando Jaramilla wa Colombia, Gamani Corea wa Sri Lanka na Boutros Boutros Ghali wa Misri ambaye pia amepata kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

mwacheni mzee ale bata jamani
 
Hivi Mkapa kwa nini yeye hajiiti Dr. Dr. Dr. Dr. Dr.? Kama mkuu wa kaya?

Mwasisi wa ufisadi anapeta tu jamani! Mungu hatendi sawa kwa watu wake , hivi hii ndege inayompeleka haiwezi anguka kama ile ya kina ndadaye?
 
Unajua siku JK alicheka ukumbini ghafla pale Davos hata nikabaki nashangaa na kujiuliza alisema nini hadi acheke mwenyewe ukumbi mzima ? But he wa supported kiasi na wanazi wake alio ongozana nao .Mie naogopa sana ikifikia kimataifa na JK anatakiwa kusimama kusema kitu .
 
Back
Top Bottom