Mkapa aenda Uswisi kuongoza kikao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa aenda Uswisi kuongoza kikao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th January 2012 @ 15:00

  RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, anatarajiwa kuondoka leo nchini kwenda Geneva, Uswisi ambako ataongoza Mkutano wa 28 wa Bodi ya Kituo cha Kusini ambacho yeye ni Mwenyekiti wake.

  Kituo hicho kinachoundwa na nchi 52 zinazoendelea, kilianzishwa mwaka 1980 chini ya uenyekiti wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msaidizi Binafsi wa Rais huyo mstaafu, Malago Malagashimba, Rais mstaafu pamoja na kuongoza mkutano, pia atashiriki katika mkutano wa 13 wa Baraza la Wawakilishi la Wajumbe wa Kituo hicho, sambamba na mkutano wa kituo utakaozungumzia hali ya kiuchumi duniani.

  Mara kadhaa, Chifu Emeka Anyaoku ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola amekuwa akimwelezea Mkapa kama Mwenyekiti aliyefufua moyo wa Mwalimu Nyerere katika maendeleo ya kituo hicho.

  Mkapa ambaye ni Mwenyekiti wa Tano wa Bodi ya Kituo hicho, baada ya shughuli hiyo nzito, anatarajiwa kurejea nchini usiku wa Februari 4, mwaka huu.

  Wengine ambao wamewahi kuwa wenyeviti wa Bodi ya Kituo hicho ni Luis Fernando Jaramilla wa Colombia, Gamani Corea wa Sri Lanka na Boutros Boutros Ghali wa Misri ambaye pia amepata kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwanini hakwenda yule wa kuchapia?
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nadhani Kikwete ana Wivu hapo... anajaribu kushinda safari na Mkapa; Mkapa ukisikiliza hotuba zake hakuna the the the the

  Smooth with points, ndio maana UN Organizations wanapenda kumtumia...

  Sasa tusubiri baada ya Miaka 3 kaka yetu Kikwete labda atajenga nyumba Dubai lakini hapapendi sana kama Europe & Amerika ambako ndiko Mkapa anapondundikia sasa hivi
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hivi Mkapa kwa nini yeye hajiiti Dr. Dr. Dr. Dr. Dr.? Kama mkuu wa kaya?
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  yule mzee wa Manufacturing of teachers.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kiingereza chenyewe anajua ???
   
 7. M

  MAMC Senior Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili ni product ya Mwalimu!iko fit, pamoja ma mapungufu - mana hata maiti huzidiana kunuka!

  Mwalimu alisafiri trip nyingi duniani baada ya kustaafu Urais kuliko alipokuwa Rais kwa miaka 25! Mkapa naye anafuata nyayo!Kama ukifuatilia bios za hao past chairmens utaona kuwa huko hawauzi sura, inapandisha profile ya nchi yetu!

  Je mwinyi? Na itakuwaje kwa JK akistaafu?!Tumwombe Mungu atupe maisha kujionea!
   
 8. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwani kiswahili hakiruhusiwi huko?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kikwete atakuwa anatuwakilisha kwenye misiba ya watu mashuhuri duniani.
   
 10. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Bora Mwinyi anaweza alikwa kufundisha kiswahili ughaibuni but Jakaya sanasana anachojua ni Viduku.
   
 11. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  achana na kiwira sijui kafanya biashara akiwa ikulu,lakini huyu mzee mpende mchukie,kwenye international platforms yuko vizuri sana
   
 12. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Jamani JF idumu milele maana inatuongezea uhai kwa jinsi inavyotupa raha.
   
 13. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Si Mkapa wala JK anayejiita Dr. Kina wajinga fulani ambao wanafikiri JK atawapa mambo fulani na hiyo wanapenda kumuita Dr na kmfurahisha. Na ukweli ni kwamba anafurahi. Mkapa kwa upande mwoingine anaitwa Dr na anapenda. I la sasa hana fursa ya kuitwa hivyo (Dr. ) sana.
   
 14. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hongera Ben Mkapa, Mungu akutangulie
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kujiita Dr. Haujuusomea ni kujiongezea title baadaye wakukumbuke hayo maintanational organization

  Lakini haujui wanakuita na kukuuliza Maswali; Marais Wangapi wa Nchi wanapata hizo kazi za UN? Wachache haswa

  Uliona Mwinyi hakupata chochote hata kwa African Union; Walimpendekeza kuwa mjumbe wa kamati za African Union akaenda trip moja ya pili kamati ikavyujwa hakuna pesa; pesa zinatoka China.
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Kha! hapo kwenye red ndio umeniacha hoi!
   
 17. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kiingerza anajua ndio nini acha fikra za kitwana bana jipende mwenyewe kwanza
   
 18. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  kinaruhusiwa ila si unajua na yeye anataka aonekane wamo.
   
 19. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Benjamini MKAPA the best president who ruled URT.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkapa akiwa anatoa speech unajisikia fahari kuwa mtanzania sio hili dubwasha la sasa hivi.
   
Loading...