Mkanganyiko Wa Siku Ya Pasaka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkanganyiko Wa Siku Ya Pasaka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 24, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Iringa Mjini, saa kumi na mbili na nusu jioni. Ni Jumapili. Ni Sikukuu ya Pasaka. Ona bucha hiyo ya nyama, ' Executive Butcher'. Mwone mama huyo mwenye haraka. Mwingine angedhani, kuwa siku hii ni yenye pilika nyingi.


  Hapana, si kila mahali. Ninapopiga picha hiyo nimesimama kwenye meza ya magazeti, mwuzaji anaitwa Salumu. Hakuna mteja mwingine, ni mimi tu, na mwuzaji. Na mie sijafika mjini tangu asubuhi, nimekuja kuchungulia vichwa vya habari.


  Ndio, mahali hapaniliposimama ni karibu na Soko Kuu, lakini kuna ukimya mkubwa. Wanaotembea mitaani wanahesabika. Ndio, kuna ombwe fulani hivi- vacuum.


  Siku kama ya leo kwa wengine ni yenye mkanganyiko mwingi. Ni mkanganyiko wa kimaisha. Uliye Ughaibuni, au hata uliye Tanzania lakini uko mbali na hali halisi, huenda usielewe ni kwanini bucha hiyo iko wazi mpaka giza linapoingia, tena kwenye Jumapili ya Pasaka.
  Mwenye bucha anaielewa jamii inayomzunguka. Hajakosea. Siku kama ya leo kuna baba au mama aliyewaacha watoto nyumbani wakisubiri aende akahangaikie nyama ya pasaka. Hata kama kila siku familia inakula ugali na maharage au mboga za majani, basi, walau siku kama ya leo nyama iliwe, si Pasaka!


  Lakini kilo ya nyama imefikia elfu nne. Leo si siku ya kurudi nyumbani na nusu kilo ya utumbo. Na mzazi huyu amehangaika wiki nzima kutafuta hela ya Pasaka. Huenda kuna baba au mama aliyeahidiwa elfu hamsini jana jioni. Kaifuata, hakuipata. Kaambiwa arudi leo mchana. Ikafika mchana, kaambiwa arudi saa kumi na moja jioni. Bahati, ameipata, elfu hamsini.


  Huyoo, ataanza mwendo kuitafuta bucha ya nyama. Kama hakuna wenye bucha waelewa kama mwenye ' Executive Butcher', basi, kuna familia nyingi, siku kama ya leo zingeipitisha kwa kula ugali na maharage, kwa vile, bucha zote zimefungwa saa sita mchana!


  Nilipata kuandika, kuwa watu wa Ulaya na Marekani wanajua zaidi namna Waafrika tunavyokufa. Si wanasoma kwenye magazeti na kuona kwenye runinga, lakini hawajui jinsi tunavyoishi. Na watashangaa sana kuona ' Executive Butcher' iko wazi mpaka saa moja usiku, siku ya Pasaka!

  Maggid,
  Iringa.
  Jumapili, Aprili 24, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama monika mbege au fredirik mwakalebele angekuwa mbunge wa iringa-mjini usingeandika upupu huu.

  aluta continua.
   
 3. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mjengwa ametoa simulizi la maisha ya kawaida ya kitanzania bila kujali siasa wala wabunge ambao kwa wingi wao pale mjengoni hawana habari na umaskini wetu utawasikiaa tu wakisema ndiyooooooooooooooooo so kumtukana sioni kama ni busara
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Asante sana Makondo, hata mimi nilishangaa ndugu yangu huyo alipoingiza habari za akina Mama Mbega na Mwakalebela.
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Unajipa big up mwenyewe?
  Crap!
  Nani asiyeijua iringa? Au mkoa mwingine wowote?! Wtf.
   
 6. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wakuu heshima mbele sana tu,
  Mimi nadhani ni muhimu sana kusoma maudhui kwa makini kabla hatujajibu lolote, maelezo ya mleta mada ukiyasoma vizuri utagudua kuwa Iringa ni mfano halisi wa matatizo ya watanzania wengi! Aina hii ya matatizo hata ya kumwambia mama bandika maji ninakuja na kisha mtu anakimbia kwenda kupiga mzinga wa kilo ya unga ndiyo hasa maisha yetu halisi. Isipokuwa wachache sana ambao wakiona watu wanagoma kwa sababu mkate umepanda bei basi wanauliza kwa nini wasinunue donati.!!! Kwa kweli kama usomaji uchangiaji na uandishi wetu mara zoote utajaa bashasha za kisiasa huenda hatutaweza kabisa kukomba taifa hili lilizama katika umaskini wa kupindukia. Ndugu zangu wanachama wa vyama vya siasa kumbukeni kuwa watanzania wengi sana si wanachama wa chama chochote na hivyo kuwashawishi wakuunge mkono katika mageuzi yoyote unahitaji hoja ya haja
   
 7. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli habari ndefu nyingi humÙ huwa hazivutii mtu kusoma hadi mwisho ila hii ni moja ya zile zinazotoa hamu mtu unataka uendelee kusoma

  Yaani umeandika kiasi kwamba nimejawa na fikira nyingi sana sasa za kuhusu maisha ya waTanzania wengine nchini humu ila tukumbuke kwamba kuna wengine duniani boti moja. Imenigusa sana

  Umeandika kama vile hadithi yaani ulivyo yaweka maneno ki aina hiyo hadi raha. Hivi bucha hiyo ilikuwa wazi kweli tarehe 24 April 2011? na hadithi ni true au ya kutunga? Usinishangae naona una ujuzi wa kulezea
   
 8. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Unaposoma habari hii kitu cha kwanza kujiuliza ni kwann hali imekuwa kama ilivyo?na nani ametufikisha hapo!wenye nchi wanalijua na jitihada gani zinafanywa kulikabili?
   
 9. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unadhani.........

  endelea kudhani.

  mtoa mada anajulikana kwa uhodari wa kuandika mafumbo.
   
 10. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maggid namfahamu na post zake nimezisoma,lakini hiki kipande kimevuka mipaka ya itikadi,kinahusika sana kwenye maisha ya kitanzania (ambayo hayana itikadi yeyote zaidi ya kuwa tu ya kimasikini na ya kusikitisha)
  Nimezaliwa Iringa,nimekulia Iringa. Lakini pia nimetembea na kuishi sehemu nyingi sana Tanzaniani mwetu humu. Nipo kwenye nafasi ya kumuelewa mwandishi vyema mnoo!Ndio, machozi yalikaribia kunitoka wakati nikiendelea kusoma. Najua si tu kwa ajili ya mistari hii,bali kumbukumbu ambayo kipande hiki kimeitonesha. Nikakumbuka siku mlezi wangu alipofanikiwa kurudi na firigisi na miguu ya kuku mwendo wa saa 10 jioni. Tukiwa wadogo kabisa,hatukujali kufahamu ameitoa wapi! Au pengine kuhoji,"mama mbona firigisi na miguu,kuku wenyewe wako wapi?"...badala yake,tulijawa na furaha isiyo kifani kwamba hatimaye.....yes hatimaye, subira imevuta heri ya kula "kuku" japo ni saa 11 jioni! Baada ya miaka mingi,ndipo nilikuja kufahamu kuwa firigisi na miguu,ni "mapanki" kwenye mabucha ya kuku. Umenikumbusha mbali Maggid!
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi majuha na wajuaji na wanajidai wanajua kila kitu na kwa bahati mbaya ikatokea walichokisoma au kuelezwa hawajaelewa basi huishia kutukana au kuharibu topic au kuikejeli kama alivyofanya mchangiaji wa kwanza. Bibilia inasema anayejibu bila kuelewa ni MPUMBAVU.
   
 12. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Maggid ulichoeleza hapa kimenikumbusha kona ya Marehemu Kiona Mbali na nepi yake enzi hizo alivyokuwa anachambua maisha ya mtanzania. wakati nikiishi Mwananyamala kwa Kopa kwa ndugu yangu miaka ya 1993-94 nikipita mitaani kuja kutokeza Kinondoni Mosque niliweza kuona maisha halisi ya Mtanzania. Ulichoeleza ni ukweli mtupu. Ni kwamba Pasaka na sikuku nyingine inafana zaidi kwenye vyombo vya habari ila si katika maisha halisi ya mtanzania. Hali ya Watanzania walio wengi haiwaruhusu kusheherekea kitu chochote kwa kubadili mlo bali huingia katika mkumbo kwa sababu tu tarehe ya sikukuu imefika.

  Tutatoka lini huku?
   
 13. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukisoma Post hizi atleast utaelewa JF kuna watu ambao kwao maelezo yoyote ni siasa. Au kuna watu ambao kwao post ikiwekwa na fulani basi anatakiwa atukanwe haraka saana ili akome kupost tena. Kuna tatizo kubwa saana la kiuelewa. Kuna vitu vidogo na vya kawaida kabisa lakini response huwa ni za kushangaza. Kuna kazi kubwa mbele yetu.
  Maggid hayo ndio maisha ya Kitanzania. Kuna matatizo pande zote mbili. Serikali na watu wake. Serikali imejaa takwimu ya mafanikio ya kiuchumi lakini wananchi wanaonekana kutopelea kwenye umasikini wa kutisha. Lakini upande mwingine nikijikumbuka mwenyewe wakati huo tupo kijijini tulilazimika kufuga kuku ili siku ya sikukuu na mahitaji mengine yaweze kupatikana kwa njia hizo. Labda initiative za aina hii zinaweza kuwasaidia wananchi.
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Maggid ameibua swala moja ambalo nafikiri katika uhai wangu ningependa litokee Tanzania. Ile culture ya kuazima fedha au kukopa na kutegemea fulani atakupa pesa, na baadaye kuzungushwa kwa muda mrefu, unaweza kuwa unafuata pesa kwa miezi au hata mwaka kila siku njoo kesho etc. Au njoo kesho muhindi wangu atakuwa amenipa pesa etc.

  Tufike mahali tuseme basi na banks ndio wawe watu wa kuwakopesha Watanzania na sio kaka mjomba shangazi rafiki, muhindi wangu etc.
   
 15. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli wana jf mtu kusoma sio kuelewa na ni vizuri mtu kusoma kitu hata mara mbili kabla ya kukimbilia kujibu as kusoma na fikira zingine kichwani inaponza wengi na hata katika mambo muhimu kama mitihani etc pia katika kujibu maswali ya job interview.

  Wengine huwa wanasoma kwa kuruka mistari na hii inasababisha kutosoma point muhimu.

  Hii yote ni kuelimishana na kujifunza ili kuwa bora kesho na msomaji mzuri na kuelewa kinachoelezezwa sio kufikiria vingine as inapotezea mtu mengi
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe ni miongoni mwa mazezeta humu JF. Toa upupu wako hapa. unataka kila kinachoandikwa kisifu chadema tu. kwani iringa kuwa na mbunge wa chadema ndo imebadilika kutoka TZ yetu?
  Thanks Mjengwa kwa kueleza hali halisi ya maisha yetu. Mimi naenda mbali zaidi kuna wengine siajabu walikuwa wanatafuta angalau milo miwili badala ya mmoja waliozoea siku zingine, halafu jitu kama prophet linakuja na ujinga wake hapa wa chadema.
   
 17. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umeelezea tu maisha kwa Ujumla lakini naona Chadema wameona una mpiga vijembe Mbunge wao! Lakini Ndugu zangu wa Chadema hamtaki hata mtu aongee mambo yanayo endelea Iringa na maeneo mengine! Mbona nyie mnaisema Serikali kila siku,lakini mkiguswa na wakati mwingine mnajihisi tu mmgushwa basi inakuaa balaa mna anza matusi! Hivi mkija shika serikali tutaongea kweli! Nadhani hata JF mtaifunga na wanaharakati wengi watafanyiwa assasination! Maggid haja mlaumu mtu wala Kumtaja huyo Mbunge wa Chadema! Wafuasi wa Chadema acheni upimbi,acheni ushabiki mahaba!
   
 18. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Acha chuki zisizo na msingi wewe.Mjengwa kaandika kitu makini sana.mimi nahisi wewe umeshindwa kuelewa hayo aliyoyaandika ..pole sana.
   
 19. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mjengwa Hongera sana kwa "post" hii,imenikumbusha mbali sana mwaka 1999-2000,baba yetu alitoka Mkoani Singida kuja Dar na ilikuwa ni sikukuu ya Eid.Alinunua kuku wa kienyeji watatu.
  Aliwaweka kwenye "buti" ya basi enzi hizo za basi la Golden Coach...alipofika Dar es salaam bus enzi hizo lina simama mtaa wa Msimbazi kariakoo..kufika pale Kuku wote watatu walikuwa wamekufa..alisikitika sana na aliamua kuwatupa wale kuku ila kabla ya kuwatupa kuna vijana walimuona wakamwambia Mzee "usitupe hao kuku,leo ni sikukuu ya eid na watoto wetu hawajapata pilau wala kipande cha nyama,Mzee tuachie hao kuku tutaenda kula na familia zetu"
  Hayo ndo maisha ya Mtanzania halisi.ebu piga picha enzi hizo ni 2000 maisha yalikuwa hivyo,je leo hii 2011?maisha yamekuwa magumu mara ngapi?
  Hali imekuwa mbaya sana.
   
 20. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maggid Hongera kwa kuonesha picha halisi ya maisha ya Bongo! Wala hujataja Mbunge wa Chadema kwanza haiana uhusiano kabisa! Hivi tukianza kuisifia Chadema pasipo sitahili sifa huo utakua ni ujinga kabisa! Chadema msiishi kwa kusifiwa sifa huja baada ya matokeo!
   
Loading...