Tetesi: Mkanganyiko NACTE, TCU, HESLB

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,517
2,000
Mnamo mwezi wa tano NACTE walifungua dirisha la Udahili ambapo wanafunzi kadhaa walilipia fedha ya usajili 50000/=. Guidebook waliyoitoa NACTE iliweka GPA 2.7 kama kiwango cha mwisho cha ufaulu kwa wadahiliwa.

Mwezi wa Sita mwishoni HESLB nao wakafungua fursa ya kuomba mkopo, ambapo wanafunzi wamelipia 30000 kama ada ya kuombea mkopo.

Sasa TCU nao inasemekana wametoa Tamko lao 11 July 2016 kuelezea viwango vipya vya ufaulu kwa wadahiliwa.

Ili upate mkopo lazima upate Chuo. Je hela za wadahiliwa wengi wa Diploma wenye GPA less than 3.5 zitarudishwa? Maana probability ya kupata chuo ni 0.

Wenye kujua watujuze.
 
sime

Senior Member
Jul 14, 2016
146
225

Subiri Nacte nao wazungumze maana site yao ipo offline na kwa Tcu subiri guide book , hilo tamko kama halijaeleweka bado japokuwa linaonekana kwenye site ya Tcu, subira inahitajika brother.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,042
2,000
Tatizo ni kubadilisha gia angani-yaani watu wameshajipanga na ndege imeondoka ndio wewe unatoa tamko. Lakini upepo huu unaendana na filosofia ya awamu ya tano ya kuchuja v.....a. Issue ya timing kwa kweli sio nzuri isipokuwa zile 30, 000 ni za huduma upate mkopo usipate. Swali ni nani alipe kwani kama yangejulikana mapema wengine wasingeomba. Kwa wale wenye vigezo baada ya tamko la TCU ufanyike mpango maombi yao yapelekwe TCU au waruhusiwe kuomba upya kwa gharama zile zile. Ingawa kuomba upya kutakuwa na gharama mpya. Serikali iwafikirie.
 
Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,517
2,000
Subiri Nacte nao wazungumze maana site yao ipo offline na kwa Tcu subiri guide book , hilo tamko kama halijaeleweka bado japokuwa linaonekana kwenye site ya Tcu, subira inahitajika brother.
Mkuu TCU wameshaweka Tamko jipya la kufafanua DD na 4 points. Na lile lingine la GPA 3.5.
Kwa hiyo GPA Lower Second ndo hawataweza kupata Degree au wasubiri uongozi ubadilike. Na vipi Hela Zao?
 
Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,517
2,000
Mbona hawaji wafafanuzi au Invizibo peleka jukwaa la Sheria Uzi huu ili nisaidiwe kurudishiwa 30000 yangu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom