Sawa mkuu, ngoja na wengine waje tuone michango yao, lakini labda nikuulize ni kwa nini iwe mafuta na isiwe mbegu au unga wake?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu ni hesabu rahisi sana kuijua kwa mtazamo wangu,!
Kilicho na nguvu ya kutibu(dawa) ni mafuta yaliyo ndani ya mbegu ambayo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi yana kemikali asili nyingi sana,
Ili uweze kupata unga ni lazima ama huwa ni vema utoe mafuta kwanza kisha utabaki na makapi ambayo bila shaka waweza kuyasaga kutoa unga. Mfano ni mashudu/mabaki ya mbegu za alizeti na mbegu za pamba.
Si kwamba unga unakuwa hauna yale mafuta la hasha yanakuwepo ila kwa kiasi kidogo sana.
Ukitumia mbegu ni sahihi ambapo utapata mafuta na gamba lake(unga).
Changamoto itakuwa je unahitaji kipimo gani..?
Mfano kwa mujibu wa recomendation (ushauri wa kitabibu wa kisayansi) mwanadamu anatakiwa kutumia kiasi cha mils tano ya mafuta hayo kila siku kwa wastani ambayo twaifananisha ujazo huo sawa na kijiko kidogo cha chai..
Kwa matokeo bora.!
Sasa swali langu ili upate kiwango hiki unachoshauriwa kitaalam kwa siku je unawezaje kupima kiwango hicho kwenye unga? Unahitaji unga kiasi gani ili kupata 5mils.?
Au je utahitaji mbegu ngapi kwa siku ili upate kiwango hicho cha kipimo kwa siku..?
kwa uelewa wangu kushindwa kupata kipimo halisi kwa mahitaji ya mwili wako unaweza kuwa na matokeo ya aina mbili
Kuzidisha kiwango cha dawa au kupunguza kiwango..
Hivyo sabbu ni rahisi zaidi kupata kipimo cha mafuta huenda matumizi ya mafuta ikawa uamuzi bora zaidi kuliko hizo njia nyingine..
Sent using
Jamii Forums mobile app