Mkandarasi barabarabya Buza - Kilungule apewa siku 60 kukamilisha mradi

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,569
2,648
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkandarasi Group Six Internation Ltd kuhakisha ifikapo Septemba 30, awe amekamilisha miradi ya ujenzi wa bababara ya Nzasa Kilungule-Buza yenye urefu wa kilomita 7.6 na ujenzi wa kituo cha daladala eneo la ekari tano.

Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Julai 8, 2022 wakati akikagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha miradi hiyo yote inayogharimu shilingi bilioni 21.5

Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 20, ujenzi wa makaravati sita na ujenzi wa kituo cha daladala cha kuhudumia Coaster 100 kwa wakati mmoja, maduka 114, mgahawa, huduma za benki na vyoo.

Pia, mkataba huo umeongezewa kazi za ujenzi wa soko la Zakhem lenye ukubwa wa mita za mraba 4,750 ambalo limesanifiwa kuwa na vizimba 136, maduka 150, vibanda vya kuku 35, vyoo 9 na ujenzi wa maegesho ya magari yasiyozidi 25 kwa wakati mmoja.

Bashungwa amesema, kutokana na changamoto ambazo tayari zote zimetatuliwa, mkataba wa awali ulitakiwa kukamilika Juni 2021, lakini kutoka na changamoto za umiliki wa ardhi, kuchelewa kumlipa mkandalasi kwa kazi alizokamisha na mradi kupita kwenye hifadhi ya bomba la TAZAMA, imesababisha mkandarasi kuongezewa muda.

Pia ametoa siku 14 kwa Mkurungezi wa Halmashauri ya Temeke kulipa fidia ya nyumba tatu kwenye makutano ya barabara ya Mbande ili barabara iwe na upana, waweze kuonana kwenye makutano ya barabara ya Nzasa, Kilungule na Mbande.

Naye Meneja wa TARURA Temeke, Mhandisi Paul Mhere amesema mradi umekamilika kwa asilimia 75, ambayo ni barabara ya Nzasa-Kilungule-Buza yenye urefu wa kilomita 5.4 za lami na kilomita 2.2 za zege zitajumuisha mifereji ya pembeni, njia za wanaoenda kwa miguu na taa za barabarani.

Pia daraja moja lenye urefu wa mita 20 linalounganisha Kata ya Kilungule na Buza ambalo tayari limeshakamilika.
 
Back
Top Bottom