Ndugu wanaJF,
Waziri John Magufuli alipokuwa akisoma bajeti ya Wizara yake alisema contractor wa barabara ya kutoka KIA kwenda Mererani amefukuzwa kutokana na utendaji mbovu. Hakuendelea na detail yeyote ile kuhusu huo mradi, huenda hakutaka watu wajue zaidi au yeye mwenyewe hajui kilichotoekea.
Ukweli ni huu:
Kampuni iliyopewa kazi ya kujenga hiyo barabara inaitwa Strada International iliyoonyesha ina Makao Makuu yake UK. Ukubwa wa mradi ulikuwa ni km 26 za kiwango cha lami na gharama za mradi jumla ni 26bn.
Contractor alipewa advance payment ya takribani 3bn (am not sure ila ni kati ya 2.5 mpaka 3.2). Baada ya kupewa hiyo pesa contractor huyu ambae asili yake ni singa singa hakufanya chochote toka mwezi wa 5 mwaka jana mpaka mwezi wa kwanza mwaka huu. Zaidi alisafisha barabara mita 600 tu ambayo ni hatua ya mwanzo kabisa. Hata kujenga camp yake alishindwa, na mbaya zaidi hakuwa na vifaa vya kufanyia kazi. Alinunua grade 2 za kichina na hela hakumalizia kulipa. Mradi ulitakiwa kuwa na zaidi ya tipper 25 lakini alikuwa na tipa 2 za kukodi. Pamoja na kampuni ya usimamizi ya LEA kutoa vielelezo toka mwezi wa 10 kwamba Contractor hana uwezo wa kufanya kazi, aliendelea kulelewa mpaka mwezi January alipokimbia.
UFAKE WA KAMPUNI HII
Inashangaza kuona kampuni ya kigeni ambayo ni ya kisanii imepewa tenda ya kujenga km 26 za rami ambazo ni sh 26bn wakati kampuni hii haijawahi kujenga hata mita 5 za changarawe. Hii kampuni haijawah kufanya mradi wowote wa barabara, lakini walisubmit Company Profile iliyoomyesha wamejenga barabara Sudan, Ghana, Msumbiji, Ethiopia, Qatar, UK na Namibia. Kabla ya kupewa huu mradi kwa kuwa ni kampuni mpya tanroads huwa na utaratibu wa kujiridhisha kwa kupeleka wajumbe baadhi ya nchi kwwnda kuona miradi iliyofanywa na hiyo kampuni. TANROADS ilituma wajumbe ghana na msumbiji, na wajumbu hao walirud na report ya kuonyesha kwamba ni kweli walifanya na mbaya zaidi walirudi mpaka na ripoti za idara na mamlaka za barabara ktk nchi husika kwamba hiyo kampuni ilifanya kazi huko (Kitu ambacho si kweli, wajumbe walihongwa na kuchakachua report zote za Msumbiji na Ghana kwamba kampuni ilifanya kazi huko na kukamilika).
HASARA KWA SERIKALI
Serikali imepata hasara kubwa katika maeneo makuu matatu:
1. Adnvace pyament ya 3bn. Serikali imeambulia grader 2 za kichina zisizo na thamani ya zaid ya milioni 200.
2. Gharama za kumlipa mhandisi msimamizi kwa zaidi ya miezi sita aliyokaa. Ambapo ni zaidi ya million 700.
3. Kuandaa tender upya ambapo gharama za mradi lazima zipande kutokana na kupanda kwa maisha. Maana 26bn ni tender iliyotangazwa mwaka 2012.
NINI KILITOKEA MPAKA STRADA IKAKIMBIA
Katika hali ya kusuasua alikokuonyesha, serikali ilianza kuichunguza hii kampuni kwa undani zaidi maana hata wale waliokuwa wamekula hela kwa kuipa kazi hii kampuni ilionekana wanashindwa kuibeba. Serikali ikagundua kumbe hata bank guarantee iliyowekwa ni feki! Hiyo bank ilikana kuijua hiyo kampuni hii na hapo ndipo serikali ilipochanganyikiwa maana mdhamini aliyewekwa ili kama mambo yakiwa sivyo yeye ndo alipe fidia haijui hiyo kampuni. Watu hao hao wa TANROADS waliokula dili hilo wakamshtua mteja wao kwamba serikali imeshtukia mchezo na jamaa akakimbia mpaka leo.
Kuonyesha kampuni ilikua ni ya kitapeli, ilikopa mpaka furniture za ofisi. Vitendea kazi kama computers na printers walikopa duka la Compcat hapo Arusha. Ana deni kubwa la milion ka 200 hivi kutoka kwa NSK. Wafanyakaz wanadai mishahara ya mwezi wa kumi na mbili ma wa kwanza na hapo ni baada ya kugoma kwa wiki nzima na kumtumia mkuu wa Wilaya na mbunge mh Lema kumpigia simu ndipo alilipa deni la mwezi wa 10 na 11.
EXIM WANUSIRIKA
Bank ya Exim ilibakia kidogo tu nayo itapeliwe baada ya hiyo kampuni ku-process mkopo wa milion 450. Katika hali iliyoonyesha bahati kwa Exim, walichunguza kabla ya kutoa hizo hela maana walikuwa tayari wameshajiridhisha kwa asset zilizowekwa ambazo miongoni mwao ndo zile grader ambazo sasa serikali imezizuia kupitia TANROADS Arusha.
KAULI SAHIHI
Ukweli ni kwamba mkandarasi Strada alikimbia mwenyewe na si serikali kumfukuza. Na amekimbia baada ya kuona ukweli kuhusu kampuni yake kufoji vitu umejulikana. Lakini wameondoka na faida kubwa na kuitia hasara serikali. Maana ktk 3bn, alizotumia Bongo hazifiki hata 1.5bn mpaka anaondoka.
NANI WA KUWAJIBISHWA
Kitengo cha Procurement cha TANROADS lazima kiwajibike kwa hili maana walifanya Investigation kwa hii kampuni na kutoa report za uwongo. Maana huwezi kuniambia walivyoenda Ghana na Msumbiji walidanganywa na hizo mamlaka kuhusu kampuni hii. Na pia bank guarantee walishindwa ku-confirm kabla. Hili swala lilifanyika wakiwa wanajua dhahili ukweli kuhusu kampuni hii.
Na ningependa kuona Magufuli akilitolea ufafanuzi swala hili na hatua zilizochukuliwa kwa watendaji waliosaidia kuidanganya serikali. Na pia mbunge husika, Olesendeka na ningependa ajue kuhusu hili maana barabara ipo jimboni mwake.
Nawakilisha.