Mkakati wa maandamano ya kupinga kusomwa kwa mara ya pili kwa mswaada wa kuunda katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati wa maandamano ya kupinga kusomwa kwa mara ya pili kwa mswaada wa kuunda katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mwana_mapinduzi, Nov 17, 2011.

 1. M

  Mwana_mapinduzi Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania Wany'onge,

  Nina masikitiko makubwa kwa hayo ambayo yanatendwa na walioshikilia dola. Kusomwa kwa mara ya pili kwa mswada na kushindwa kuwasikiliza walio wengi (Watanzania) kwa kusingizio cha kuwakilishwa na Wabunge wao, ni usaliti tosha. Kama walivyoongea wadau wengi kuhusu mlolongo wa mamlaka ambayo amepewa Rais na hivyo kushindwa kuwawajibisha rafiki zake aliowateua kufisadi mali zetu ni jambo lisilovumilika.

  Kwa yeyote anayetaka kukukata mkono au kukupofosha ili mradi tu ushindwe kuishi kwa raha na kufurahia siku chache ambazo Mola amekupa, inabidi kumwajibisha. Njia pekee ya kuwawajibisha ni kutumia NGUVU YA UMMA. Tujifunze kutoka Tunisia, Misri, Libya na Sasa Syria. KIFUPI, TUKIAMUA, TUNAWEZA KUJIKOMBOA NA UDHALIMU HUU WOTE UNAOENDELEA TANZANIA KWA SASA. NJIA PEKEE NI KUINGIA MTAANI.

  'NASEMA TUKIAMUA TUNAWEZA'. Kwa mujibu wa Taarifa za Kiintelejinsia ya Mkuu wa Polisi TZ bwana Mwema, alisema Polisi mmoja anahudumia watu zaidi ya 3000. Naamini hawatuwezi. Jambo la msingi ni kuwa na mkakati imara itakapofika siku kuingia barabarani.

  Kwa Taarifa ambazo zimetufikia leo hii, baadhi ya Askari wa Jeshi katika nchi ya Syria wameasi na kushambulia kituo cha Upelelezi cha Jeshi la nchi hiyo. Si muda mwingi, Nguvu ya Umma itakomboa nchi ya Syria.

  Kunyimwa kwa fursa ya kuwa na katiba yetu, ni mwanzo mzuri wa kuanza kazi ngumu ya ukombozi wa nchi yetu. Kila Mtanzania atambua kuwa, jukumu la kuikomboa nchi hii ni la kila mmoja wetu. Usidhani kukaa pembeni kwako huta athirika na lolote litakalo tokea wakati Saa ya Ukombozi itakapofika. Ukikaa pembeni utambue kuwa utakuwa ni mmoja wa Wasaliti ambao tulipigania nchi wote na sasa wanatunyonya. Kujitenga na vuguvugu hizi utambue kuwa wewe ni msaliti. Saa ya kuunda baraza la mpito i-karibu. Hima tushirikiane.

  Polisi ni watu kama sisi na ni ndugu zetu kama ilivyo kwa askari jeshi na JKT. Tukiamua Tunaweza. Raia 15 Askari Mmoja. Tukiamua Tunaweza.

  Mkakati wa Maandamano
  1. Endapo polisi watajaribu kuwatawanya, msigeuke nyuma, au kurudi nyuma. Ukigeuka nyuma, mnawapa fursa ya kuwashambulia na kuwafanya lolote.
  2. Waandamanaji wa Mstari wa Mbele, sharti washikane Mikono ili kudumisha Umoja. Waandamani wa Mstari wa Nyuma Watachukua Jukumu la Kuwalinda Wale walio-mstari wa Mbele. Hata silaha, lakini hata mawe yanaweza kutumika kujihami endapo polisi wataamua kutumia mabomu ya machozi au risasi za moto.
  3. Kila Polisi anayejipendekeza kwa kuwasogelea waandamanaji ni Kumkamata Kama Mateka. Kukamatwa kwa polisi kuendelee hata sehemu nyingine, wakiwemo wale Usalama barabarani. Mwishoni, mkakati uwe wa kuwakamata polisi wote wanaovaa kiraia, na yeyote anayefahamika kuwa ni polisi na kuwadhibiti.
  4. Polisi wote wanapenda kutoa amri nao watakuwa katika mkakati wa kukamatwa na waandamaji kwa sababu ni vibaraka wa Watawala.
  5. Kama mjumbe mmoja avyopendekeza, Maandamano yatafanyika kila mahali na sehemu zote zenye mikusanyiko mikubwa mfano, Ubungo, Mwenge, Manzese, Buguruni, Magomeni, Kinondoni, Sinza, Tandale, Kimara, TAbora, Temeke; yaani kila palipo na watu, mikusanyiko itafanyika.
  6. Waandamanaji watakuwa ni watu wa rika zote, wakubwa na wadogo kwa sababu, kila mmoja anaathirika na unyanyasaji na wizi la raslimali zetu kutokana na katibu mbovu.

  Mwisho, mikakati ni mingi na wenzangu mtaendelea kutueleza mingine.

  Naamini Polisi na Jeshi Wataunga mkono harakati hizi za kuikomboa nchi yetu kutoka kwa Mabwenyenye.

  Mwanamapinduzi wa Kweli.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kama tutakua na ujasiri huo kwakwel tutalikomboa taifa.
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hakuna kisicho wezekana chini ya jua,tushikamane ili tuweze kulikomboa taifa.
   
 4. PROF. ENG

  PROF. ENG Senior Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo mkakati wa kwanza ukiweza kufanikiwa zingine zote rahisi.
   
 5. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Huu mkakati si wa ukombozi bali mkakati wa kuangamiza taifa hili. ukisema askari mmoja anahudumia raia 3000 na wote ni vibaraka wa utawala unamaanisha CHADEMA ndiyo watakua watawala wa haki? Ni mwanasiasa yupi aliyeingia madarakani akakubalika na wananchi wote? msipende kuwalazimisha watu kuamini mnachokiamini nyie/wewe. Waelekeze watanzania kuwa wao ndiyo wanapaswa kuiadhibu ccm kwa njia inayoeleweka sio ooh mkaa pembeni ni msaliti ooh tuige ya syria, libya, misri na kwingineko bila kuwaeleza ukweli kuwa yale ni kwa maslahi ya wachache na hata hivyo nchi hizo hazina hata mwelekeo wa kujikomboa hata kidemocrasia ya kisiasa achilia mbali kiuchumi na kijamii. Ni kweli kuwa wananchi wa Libya walikua katika mateso yaliyokuwa yana tajwa na wazungu na vijana? walijua ni mazuzu hivyo wakisukumwa kwa hisia tu wataenda bila kuuliza critical questions. Ina maana watanzania hawaoni yaliyotokea kenya na zimbabwe jinsi waliokuwa wanawaongoza katika kifo ndiyo sasa wako madarakani na wanalipwa mafao makubwa? hawaoni jinsi jukwaa la katiba walivyowalazimisha washiriki wa kongamano kukubaliana na msimamo wao pekee bila kuacha room ya mabishano ya hoja? hawaoni jinsi wanaojiita mawaharakati na wanasiasa walivyomadikteta wasiyopenda kupingwa na mtu yoyote? Hebu endeleza hilo uone ni nani atakayeshikilia huo uongozi wa mpito kama siyo kurudi kuleee kwa awakoloni wa awali?

  Eti katiba mpya!! Hata ije katiba kutoka juu kwa MUUMBA kama maadili hamna hata hiyo katiba ni bure, kamma hakuna uwajibikaji ni bure kama vijana tutakaa vijiweni kupiga siasa kila mara ni bure.

  Sasa jaribuni kufanya hicho mnachokipanga muone jinsi vijana wasiyopenda taamaa za uongozi watakavyopambana nanyi badala ya vita ya kuwateka polisi itakuwa vita yetu wenyewe kwa wenyewe.

  Kama ni mswada wa katiba ni wale mnotuongoza kutoa mapendekezo yenu maana watu hawawaelewi je ni mamlaka ya raisi makubwa mno au wananchi hwajashirikishwa? na je wananchi ni kundi fulani lenye ushawishi au ni kila mmoja kwa hali na nafsi yake? je mtatuhakikishia vipi kuwa hamtafika mahali kama mwananchi anapingana na mnachokiamini ninyi hamtamuua? hamtamtenga? je itakuwa yue asiyekubaliana na harakati zenu akaamua kukaa pembeni au kukimbia ghasia zenu na kuwa mkimbizi sehemu fulani mtamtafuta na kumuua au kumtenga. Hebu kuweni na mipango inayoeleweka na isiyotia mashaka ya kifikra wala ktia uwalakini ili tuwe pamoja katika mbio za kuikomboa nchi yetu na kuifaidi sote kwa mstakabali unaoeleweka. Si hao Action Aid wanatoa mapesa kutoka kwa balozi fulanifulani waanawapa kundi au chama fulani kwa mustakabali waoujua wao. Nafikiri usalama wa taifa unapaswa kuwa active on this matter maana kama wao wanamipango ya kuwateka wanausalama wetu kwanini tusianze nao?
   
 6. m

  mayoya Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jengeni hoja za uhakika watu wangu.
  Hili jambo si la mchezo. Ni wakati wa mabadiliko hakuna mtu au jeshi la kuzuia mabadiliko. Mabadiliko yanaweza kuwa ya amani kama walio na dola watakuwa na dhamira ya dhati kuyakubali hayo mabadiliko la yatakuja hata kama ni kwa damu kumwagika hata kama hatupendi nature ndiyo inaamua. Wale watu wa ndani (spiritual) tunajua haya mambo tayari yalishapitishwa katika ulimwengu wa juu sasa ni wakati wa utekelezaji tuache ujinga watawala ndio watakao tuumiza kama wanajaribu kuzuia mabadiliko haya. Kila mwenye uwezo wa kuomba aombe Mungu ili dola isituumize na Mungu atupe neema ya kupita hapa salama na kuingia new age. Ahsanteni wadau.
   
 7. Abbasy

  Abbasy Senior Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndio tupo pamoja,mabadiliko lazima na kama wangetambua hilo wangejiuzulu mapema nchi imewashinda au tunawatoa kwa nguvu
   
 8. a

  alpha5 JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  daah sawa mwanamapinduzi hiyo mikakati ni mizuri kwalengo moja la kulikomboa taifa hili lililozama, lakini mkakati wako namba 3 kidogo utanisumbua mimi , napenda sana mageuzi na pia ni mwanachama hai kabisa wa CDM ila mke wangu mimi ni police mke wa ndoa nina watoto nae 3. ebu imagine na tunaishi uraiani unategemea nini hapo???
   
 9. m

  mtolewa Senior Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hapo mkuu inakuwa are you with us or against us? mie mwenyewe maza na dingi wote ni wale wale? nimeshawaapigia simu kuwauliza watakuwa upande gani?
   
 10. a

  alpha5 JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  sawa lakini kumbuka lazima tu atakua against us maana na yeye yuko kazini na anaamrishwa na wakuu wake , na upande wa pili mkakati ni kwamba tuwateke mandata wote kuanzia traffic na wote wanao kaa uraiani swali linakuja je mke wangu akitekwa hauoni tena hilo ni tatizo kwangu??mimi naomba namba3 itafutiwe mmbadala
   
 11. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nachukia, dhuluma, uenevu, unyanyasaji, na kila kitendo kibaya anachofanyiwa mtu mwingine na yeyote ama aliye juu kicheo, kiuwezo na kimamlaka au aliye chini.
   
 12. m

  mtolewa Senior Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu mbona hiyo rahisi sana! siku yenyewe we unamteka wife kiana unamfungia chumbani halafu wewe mapambanoni,ukirudi jioni( kama kutakuwa na kurudi) unakutanmaji ya moto tayari.mimi nimewambia kabisa wasiposikia wenye nchi wanataka nini wakatekeleza ya wapangaji wa kwenye nchi,yatakayowapata shauri yao na hakika wajukuu zao (watoto wangu) hawatanilaumu kamwe.
   
 13. C

  Chungu_tamu Member

  #13
  Nov 18, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acheni Ujinga nyie,Mnaweza Mziki walioanzisha waarabu,Nyie upupu tu mnakimbia hovyo ,ngedere nyie!!!!
   
 14. T

  Tunsume Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Maandamano yawe yasiyo na vurugu ni sawa. Kutumia nguvu kujenga hoja na hoja yako kukubalika haina tija. Tusishambulie polisi na hata traffik. Tulinde waandamanaji wetu ili wasitumie nafasi hii kufanya fujo za kihuni ambazo zitawapa polisi fursa kuvuruga amani. Wale watakaoweza watumie simu kupiga picha vitendo vyote vya uvunjaji amani vitakavyofanywa na polisi na raia. Ushahidi huu ni mzuri sana kwa ajili ya kutumia sheria kupata mustakabali wa taifa letu. Tufuate taratibu zote za kuweza kupata kibali cha kufanya maandamano na tukikataliwa tifanye taratibu za kutumia sheria kupata haki hiyo. Tuwe watulivu kwani vurugu haitajenga tutakaoumia ni sisi wanyonge.
   
Loading...