Standalone
JF-Expert Member
- Nov 15, 2014
- 676
- 576
Yaan Kila wanachofanya Lumumba tunakipata mapemaa….Angalieni attachment ya Mkakati wa kupitisha kura ya ndio. Fungua kiambatanisho hapa chini.
===========================
===========================
MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA KAMATI ZA KAMPENI YA KURA YA MAONI YA
KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Sheria ya Kura ya Maoni inaanzisha Kamati kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kura ya maoni. Kifungu cha 12 cha sheria hiyo kinaanisha kamati hizo kama ifuatavyo:-
Kamati mbili katika ngazi ya kitaifa; na
Kamati mbili katika ngazi ya Jimbo
Kamati hizi zitaundwa na makundi ya watu, vyama vya siasa na taasisi au asasi zinazokusudia kuunga mkono au kupinga Katiba Inayopendekezwa. Swali litakaloulizwa ni lile lililochapishwa na Tume ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali na. 414A la tarehe 17 Oktoba, 201: "Je unaikubali Katiba Inayopendekezwa?, mpiga kura atatakiwa kutoa jibu la "ndiyo" au "hapana"
Kamati ya kura ya maoni katika ngazi ya taifa au jimbo inapaswa kuomba usajili kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndani ya siku ishirini na moja kabla ya kipindi cha kampeni ya kura ya maoni kuanza. Kwa mantiki hiyo, kwa kuwa kipindi cha kampeni cha kura ya maoni kinaanza tarehe 30 Machi, 2015, Kamati husika zinatakiwa kuomba usajili Tume kabla ya tarehe 9 Machi, 2015.
Kwa kuwa Sheria ya Kura ya Maoni inatoa masharti kwa Kamati zinazokusudia kuomba usajili kuteua kiongozi na kuainisha majina ya wajumbe, ni vema tukaanza maandalizi kuhusu suala hili mapema.
Katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaipigia kura ya NDIYO Katiba Inayopendekezwa, inashauriwa kwamba muundo wa Kamati ya kura ya maoni kwa ajili ya kuunga mkono swali lililochapishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwe kama ifuatavyo:-
Kamati ya kitaifa iwe na jumla ya wajumbe 300.
Katika kamati hii, kila mkoa utapangiwa wajumbe 12 ambao watakuwa na jukumu la jumla la kusimamia Kampeni ya NDIYO katika mkoa husika. Kamati hii itajumuisha wajumbe kutoka:
Makundi ya watu Vyama vya Siasa Asasi zisizo za kiserikali; na Wadau na wakereketwa wa Katiba Inayopendekezwa Namna ya kuwapata wajumbe 12 wa kila mkoa.
Wajumbe watatokana na viongozi wa Chama wa mkoa husika ambao ni:-
- Mwenyekiti wa CCM wa mkoa - Katibu wa CCM wa mkoa
- Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa - Katibu wa Uchumi na Fedha wa mkoa - Mwenyekiti wa UWT wa mkoa
- Mwenyekiti wa Wazazi wa mkoa - Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa
Wajumbe wengine watano (5) watokane na orodha ya wajumbe 125 walioorodheshwa.
Sababu za mapendekezo haya;
(1) Kuwateua viongozi wa mkoa husika kuwa sehemu ya wajumbe wa kitaifa kutajenga ushirikishwaji wa kutosha kutoka katika mkoa huo ambao kimsingi watakuwa wanajua mbinu zaidi zitakaozwezesha kuongeza ufanisi katika zoezi hili.
(2) Wajumbe watano kutoka katika orodha iliyoambatishwa, washirikisha viongozi wa kitaifa na makundi ya watu wengine vikiwemo vyama vya siasa, Asasi zisizo za Serikali na wadau wengine wakereketwa wa Katiba Inayopendekezwa.
Kamati ya Jimbo imependekezwa iwe na wajumbe 50
Inapendekezwa wajumbe hawa wateuliwe chini ya usimamizi wa Kamati ya Siasa ya wilaya na ijumuishe:
- Viongozi wakuu wa chama wa wilaya
Wabunge wa Majimbo yaliyoko kwenye wilaya
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya wenye uwezo wa kuitekeleza kazi hii walioko katika Jimbo husika hususan Madiwani, Wenyeviti wa kata, Makatibu kata, Makatibu wa Siasa na Uenezi, Uchumi na Fedha wa kata na viongozi wa Jumuiya.
Makada wengine wa chama, viongozi wa dini na Asasi nyingine wenye mtazamo wa kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa.
MAPENDEKEZO YA MAJINA YA WAJUMBE WA KAMATI YA KITAIFA WANAOTOKANA NA VYAMA YA SIASA, ASASI ZISIZO ZA SERIKALI NA WADAU WENGINE
Orodha iliyoambatishwa iwe ni pamoja na wajumbe wa kitaifa waliopendekezwa kutoka katika mkoa husika, wajumbe wengine wasiotokana na mikoa ni hawa wafuatao:-
VYAMA VYA SIASA
1. Philip Mangula (Mwenyekiti)
2. Abdulrahman Kinana CCM na Jumuiya zake
Mizengo Pinda
Balozi Seif Iddi
Nape Nnauye
Mohamed Seif Khatib
Zakia Meghji
Mwigulu Nchemba
Abdallah Bulembo 10. Sophia Simba
Jerry Slaa
Adam Kimbisa
Khadija Aboud
Emmanuel Nchimbi
Samia Suluhu Hussein
Makame Mbarawa
Anna Tibaijuka
Shamsi Vuai Nahodha
Pindi Chana
Hussein Mwinyi
William Lukuvi
Maua Daftari
Steven Wasira
Jesta Mhagama
Asha Bakari
Amina Makilagi
Eva Kihwele
Salama Aboud
Sadifa Hamis Juma
Sixtus Mapunda
Anna Abdallah
Shaka Hami Shaka
Mfaume Ali Kizigo
Wilson Mukama
Martine Shigela
Anthony Mavunde
37. Hamad Rashid CUF/ADC
38. Khadija Abdalla Ahmed
39. John Cheyo UDP
40. Juma Khamis Faki
41. Rashid Yusuph Mchenga AFP
42. Mwanamrisho Ahmeed Demokrasia Makini
43. Tatu Mbarouk APPT Maendeleo
44. Peter Kuga Mziray
45. Mwanaid O. Tahir NRA
46. Juma Ali Khatib TADEA
47. Augustino Mrema TLP
Hussein Juma
Fahmi Dovutwa
ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI
50. Magdalena Rwebangira Chama cha Wanasheria Wanawake
(TAWLA)
51. Siti Abbas Ali Chama cha Wanasheria wanawake
52. Salama Aboud Talib Zanzibar (ZAFELA)
53. Amon Mpanju Shirikisho la Vyama vya Watu wenye
54. Frederick Msigala Ulemavu (SHIVYAWATA);
55. Shaban Suleman Muyombo
56. Agatha Harun Senyagwa Shirikisho la Vyama vya Wakulima
57. Suzy Samson Laizer Tanzania (TASO)
58. Dkt. Maselle Z. Maziku
59. Hadija Kondo
60. Reuben Mtango
61. Veronica Sophu (M/Kiti) Mtandao wa Vikundi Vidogo vya
62. Catherine G. Sibuti Wakulima Tanzania (MVIWATA)
63. William Tate Olenasha
64. Makeresia Pawa Pastoralists Indigenous Non-
65. Mashavu Yahya Governmental Organization (PINGOs)
66. Said Abdalla Bakari
67. S.Mwakifwamba Shirikisho la Wasanii nchini
68. Jacob Stephen
69. Nasib Abdoul
70. Ali Kiba
71. Steve Nyerere
72. Mrisho Mpoto
73. Mohamed Lyasi
74. Mariam Hamdan
75. Hamis Mwinjuma (Mwana FA)
76. Mohamed Mavala
77. Valeri Msoka Mtandao wa Jinsia Tanzania
(TGNP)/TAMWA
78. Dkt. Ave-Maria Semakafu ULINGO
79. Idrissa Kitwana Mustapha Asasi za Kiraia za Zanzibar (Youth
80. Fatma Musa Juma (Sukwa) Centre, MYDO
81. Mary Paul Daffa Tanzania NGO's (TANGO)
82. Mzee Kingunge Ngombale Taasisi ya Tiba ya Jadi
Mwiru
83. Elizabeth Minde KIWAKUKI
84. Godfrey Simbeye Private Sector Foundation of
Tanzania
WADAU NA MASHABIKI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Dkt. Francis Michael
Evod Mmanda
Dkt. Benson Bana
Prof. B. Rutinwa
Mohamed Fakihi
Prof. Costa Mahalu
Asha Abdallah Juma
Doroth Malecela
Prof. Remmy J. Assey
Dr. Suzan Kolimba
Prof. Esther Daniel Mwaikambo
Prof. Romuald Haule
Makame Omar Makame
Dkt. Mwinyi Talib Haji
Layila Ali Salum
Hamis Dambaya
Ali Ahmed Uki
Asha Makungu Othman
Hawa Mchafu
Waziri Rajabu
Biubwa Yahya Othman
Fatma Hamid Salim
Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
Mch. Ernest Kadiva
Askofu Amosi Muhagachi
Sheikh Thabit Nouman Jongo
Sheikh Hamid Masoud Jongo
Juma Bakar Alawi
Dkt. Jasmine Tiisekwa
Magdalena Songora
Honorata Chitanda
Teddy Malulu
Shamsa Mwangunga
Asha Mtwangi
Paul Kimiti
Jesca Msambatavangu
Yasmin Aloo
Shamim Khan
Agness Likokola
Margaret Sitta
Felista Bura
B. MAPENDEKEZO YA MAJINA YA WAJUMBE WA KAMATI YA JIMBO
Inapendekezwa kwamba kila Kamati ya jimbo iwe na wajumbe 50. Wajumbe hao wahusishe:-
VYAMA VYA SIASA
1. Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya
2. Mbunge wa Jimbo husika CCM na Jumuiya zake
3. MNEC
4. Wajumbe wengine wote wa Kamati * Inapendekezwa kuwa
ya Siasa ya Wilaya* wajumbe wote wa Kamati ya
5. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siasa ya Wilaya majina yao
Wilaya/Manispaa/Mji/Jiji yaorodheshwa hapa.
anaetokana na CCM
6. Madiwani wote wa CCM katika Na pale ambapo Wilaya ina
jimbo husika** majimbo zaidi ya moja basi
wajumbe wagawanywe katika
kila jimbo.
** majina wa madiwani wote
wanaotokana na CCM katika
jimbo husika majina yao
yaorodheshwe hapa
7.
8. ADC
9. UDP
10. AFP
11. Demokrasia Makini
12. APPT Maendeleo
13. NRA
14. TADEA
15. TLP