Dah...Ngoja nikuchanganye kidogo...
Kati ya mkaa na mafuta ya taa/ndege kiasi kikubwa cha nishati kinabebwa ndani ya mafuta ya taa/ndege. Mkaa una mgandamizo msongamano wa kiasi cha 10MJ kwa kila uzito wa kilogram 1 na mafuta ya taa ni 46MJ kwa kila kilogram 1.
Bei ya mafuta huku kwetu ni karibu shilling 1900 kwa kilo 1....... na mkaa ni karibu shilingi 1500 kwa kilo 1...sasa kwa kuzingatia matumizi ya kawaida ya nyumbani...joto linalopotea wakati wa kutumia ni kati ya asilimia 30 hadi 80 kwa jiko la mkaa na kati ya 5 hadi 25 kwa jiko la mafuta.... Muda wa kufikia kwenye mchanganyo mkubwa (kukolea kwa moto) ..mkaa hutumia kati ya dakika 5 hadi 20 wakati mafuta ni kati ya nusu dakika hadi dakika 2.....mkaa hutoa joto kwa mtindo wa kielpsi wakati mafuta mtindo wake ni wa kitrapezia.......
Baada ya maelezo hayo naona kila kitu kiko wazi sasa .... Amua mwenyewe 😀😀😀😀😀😀