Mkaa VS Gesi

Watanzania walio wengi vipato vyao vidogo sana ivyo upelekea kumudu kununua mkaa wa 500 mpaka wa 1000 ambao utumika mpaka jioni, sasa uku kwenye gesi shida pale inapoisha ndio ugumu unapoanzia pesa ndani huna lazima utanunua tu mkaa hili maisha yaendelee. Ila sasa kwenye hizi gesi kuna mitungi midogo na mikubwa shida kwenye hii mikubwa sasa ikitokea gesi imeisha na ndani huna hata mia itabidi uuweke pembeni sijui mpk baada ya mwezi mmoja au miwili hata mitano ushuuda ninao wapo wengi sana mitungi mikubwa imewashinda ushaur kama unaona kipato chako cha shida nunua kamtungi kadogo tu maisha yaendelee
 
Hii maada haijabeba uhalisia wa maeneo tofauti tofauti ya Tanzania.. inawezekana mtoa maada amefikiria miji mikuu pekee.. Mfano: Kwa mji wanakoishi wazazi wangu ambao ni makao makuu ya mkoa fulani, tunapata gunia la mkaa kwa sh 17,000/=. Burnout ya mkaa ni tofauti na gesi, Wakemia wanajua vema.. kupika majimbi, maharage, kande, kuchemsha maji ya kuoga familia etc.. kwa ile location mkaa >>>>>>>>gesi
 
Umesema kweli kabisa
 
Kama rahisi kwann isipike maharage?
Hii dhana ya gesi kutokupika maharage sijui inatokea wapi!!!??? Mi naona ni woga wa watu kuhisi maharage yanachukua muda mrefu kuiva kwahiyo yatamaliza gesi na si kwamba gesi haiivishi maharage.
Mimi natumia jiko la gesi kupikia kila kitu na mambo yanaenda poa tu, hofu yangu kwenye gesi ni usalama maana inahitaji umakini mkubwa sana kuihifadhi ili kuepuka mlipuko.
 
Pole mkuu mkaa wa 2,000 ni debe 1 kwetu
 
Hivi ile gesi ya mtwara tuliyoambiwa tutauziwa bei rahisi bado?
 
Naomba utupie picha ya hilo jiko bunifu na sehemu ambayo mtu anaweza kulipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…