TANZIA Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Renatus Mkinga afariki Dunia

Huyu dingi ilikuwa akipewa nafasi ya kuongea kwenye chombo cha habari au mdahalo, ni lazima ataropoka kuhusu issue ya Deep green, Meremeta au Richmond. Hata kama mada itakuwa ni mechi ya Simba na Yanga, mzee mkinga ataropoka hizo issue.
🤣🤣
 
Wandugu tujitahidi kuzizuia jazba zetu......kukosana au kutokuelewana na mtu ni sehemu ya maumbile ya wanadamu.......tujitahidi kuzishika nafsi zetu.....pamoja na madhaifu na mapungufu lakini marehemu anabakia kuwa binadamu tu na mwanadamu mapungufu ni sehemu ya maumbile yake.....kumsengenya, kumtukana au kumdhihaki mtu aliyekufa inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wafupi wa fikra na kusahau kuwa kifo ni njia ya kila mmoja wetu na kila mmoja ataondoka kwa wakati wake.......tuombeaneni mwisho mwema.....na mengine tumuachie Mungu maana yeye ndiye anamjua kiumbe wake....
👍👍
 
Kuna siku kwenye kipima joto aliongea huku akituhumu watu left right and center, wakaenda break fupi walivyorudi alikuwa ameondolewa kwenye panel 😁 😁 😁 😁
Hahahahahahaa...mm toka jana nakumbuka matukio yake nacheka balaa yaan huyu sijui alisomaje chuo kikuu..yaan ni kivuruge na ukichek age unabisha
 
Huyu dingi ilikuwa akipewa nafasi ya kuongea kwenye chombo cha habari au mdahalo, ni lazima ataropoka kuhusu issue ya Deep green, Meremeta au Richmond. Hata kama mada itakuwa ni mechi ya Simba na Yanga, mzee mkinga ataropoka hizo issue.
Hahahahahaahaha alikua ana uchungu ..siku moja alisema ningekuwa hata mkuu wa kituo kidogo cha Polis muda huu Mkapa angekua mahabusu zile za maskin sio za watu high class hahahahaa wakaitikisa picha..ila alishasikika🤣🤣
 
Wandugu tujitahidi kuzizuia jazba zetu......kukosana au kutokuelewana na mtu ni sehemu ya maumbile ya wanadamu.......tujitahidi kuzishika nafsi zetu.....pamoja na madhaifu na mapungufu lakini marehemu anabakia kuwa binadamu tu na mwanadamu mapungufu ni sehemu ya maumbile yake.....kumsengenya, kumtukana au kumdhihaki mtu aliyekufa inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wafupi wa fikra na kusahau kuwa kifo ni njia ya kila mmoja wetu na kila mmoja ataondoka kwa wakati wake.......tuombeaneni mwisho mwema.....na mengine tumuachie Mungu maana yeye ndiye anamjua kiumbe wake....

Mkuu hapa amedhihakiwa wapi? Huon watu wanamuelezea vituko vyake? Watu tumemkumbuka kwa mbwembwe zake nuthn else! Hebu tuwe saa zingine postive jamani! Hata kidg! Kha
 
Alimkashfu sana aliyekua mgombea urais wa chama fulani cha siasa mwaka 2015.
Kejeli afya za watu sana. Maisha ni fumbo zito sana.
Daktari mhudumu anaondoka na kumwacha mgonjwa mahututi
 
Enzi hizo mdahalo akikosekana mzee mkinga nazima tv naenda zangu kunywa mbege
Alikuwa akialikwa Kipima joto au Malumbano ya hoja utapenda. Mzee anaongea kwa uchungu sana halafu anatamani amalize yote ya kifuani.

Baadae alilalamika kuwa ITV walimpiga marufuku kushiriki vipindi vyao.
 
Huyu dingi alikuwa na chuki binafsi dhidi ya Lowassa. Hakuwahi kumsema Lowassa kwa jema lolote.
 
Mwanaharakati Renatus Mkinga afariki, alikuwa mjumbe wa bodi ya Tasac iliyovunjwa na mama Samia mwezi uliopita.
Source: TPA

=========

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA Bw Renatus Mkinga amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili usiku wa kuamkia tarehe 25 Mei, 2021. Atakumbukwa kwa Mchango wake katika maendeleo ya Sekta ya Bandari. Apumzike kwa Amani.

Kifo kisikieni tu, mkewe hapo Mungu amtie nguvu, wale wanadokolea mali za marehemu na haki za mjane washindwe kwa jina la Mungu.
 
Njaa kitu kibaya sana!!huyu jamaa enzi za jk alikuwa mwanaharakati kweli kweli, kama kina LISU, hususani kwenye mambo ya bandari, ila baada ya jpm kuingia madarakani akawa muimbaji mzuri sana wa tenzi za kusifu na kuabudu, serikali ya awamu ya tano, akalambishwa shavu!!akaanza kujiita mzalendo namba 2, badala ya jpm!!hiyo ripoti ya CAG, ya juzi ikaja kuibua madudu ya kutisha hadi akaivunja bodi ya TASAC!!na yeye akiwa kama mjumbe!!na ulikuwa ukiongea naye lazima ujikinge na mwanvuli kwani sio kwa mvua ile ya mate!
Hivi mnafaidika nini kusema msiyoyajua vizuri na hasa kwa mtu asiyeweza kujitetea? Siasa tu?
 
Back
Top Bottom