kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 274
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imemhukumu kwenda jela mwaka mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Morogoro Mjini , Charles Matambo (32), mkazi wa Misufini Manispaa ya Morogoro baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia sh milioni 2.6 kwa udanganyifu kutoka kwa askari polisi.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Evodia Kyaruzi, alisema ametoa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo ya kutaka kupata fedha bila kufanya kazi wakati wana nguvu.
Alisema kuwa hukumu hiyo imetolewa baada ya kuridhirika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa polisi, Salehe Kalulu, alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 26 mwaka 2009 majira ya asubuhi huko Kihonda manispaa ya Morogoro kwa kumuuzia kiwanja hewa askari polisi mwenye namba F 3265DC Paulo.
Alidai Matambo alifanya hivyo huku akijua kuwa ni kosa kisheria na kwamba alipofikishwa mahakamani hapo alikiri kosa.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo mbali na kutumikia kifungo hicho pia aliamriwa kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo.
Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea aliomba mahakama kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa yeye ni yatima na kwamba ana familia inayomtegemea.