Mjue vizuri bi.kidude | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjue vizuri bi.kidude

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Somji Juma, Sep 2, 2012.

 1. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Bi.Kidude ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika. Jina lake halisi ni Fatuma binti Baraka. Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrikaumekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko. Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar. Bi Kidude anasema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90. Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji. Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji. Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya 'wanja' na 'hina' ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa 'Unyago' na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe. Watu wanasema 'Utu uzima dawa' Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar. Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza. Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake. Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa Jang'ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani. Bi Kidude pia amekuwa akishirikishwa na wasanii wengi wakongwe na chipukizi katika nyimbo zao. Miongoni mwa nyimbo zinazotamba sana siku hizi ambazo Bi Kifude ameimba na vijana wa kisasa ni za Msanii Ali Toll maarufu AT. Mbali na AT lakini pia Bi Kidude amewika na kung'ara zaidi katika wimbo mwingine wa vijana wa Ahmada Umelewa wa Msanii Offside Trick ambao umepigwa marufuku kupigwa kwa sasa visiwani Zanzibar.
   

  Attached Files:

 2. Baraka F.K

  Baraka F.K Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hajui tarehe yake ya kuzaliwa na mwaka,
  Sasa alijitambua vipi kwamba amefikisha miaka 10 na 13??
   
 3. c

  christmas JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,608
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  nampenda sana huyu bibi Mungu aendelee kumuweka
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ahmada umelewa kwanini umepigwa marufuku?
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,215
  Likes Received: 10,569
  Trophy Points: 280
  Weka paragraph wewe inachosha kusoma.
   
 6. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Anakumbuka alianza mzk akiwa na miaka hyo ila hajui ilikua mwaka gan,umeelewa.?
   
 7. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Eti umekosa maadil,ila inasemekana AT anawahonga wakubwa kwenye baraza la sanaa zanzibar ili kuwabania offside trick..
   
 8. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Lakin c umeisoma.?
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
 10. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  huwezi amini huyu bibi anajulikana hasa nchi za kiarabu dubai, abudhabi na oman tena na vijana ila hawajawahi hata kumuona walikuwa wanashangaa kumuona bibi kizee anaimba nyimbo taratibu kama zile za kwao, hii nilishuhudia mwenyewe tulitoka sehemu na mwenyeji wangu nikiwa pande za ulaya tukakutana na rafiki zake waarabu kwao ni omani, huyo mwenyeji alinitambulisha nimetokea tanzania kuna mmoja alikuwa hajui akacheki kwenye google map akaiona akasema na hivi visiwa vya zanzibar nikamuambia basi huwezi amini alisikilizisha kuna wimbo flani hivi wa bibi kidude na yeye akawa anaimba hata hajui anamaanisha nini ni ile kuigilizia maneno nilishangaa sana akaniambia kwao huko wanaupenda sana wimbo huo hadi baadhi watu waliigilizia wimbo huo kuimba ila bado hawajampatia hichi kitu kilikuwa ni mshangao mkubwa sana kwangu nikaamini huyu bibi masikini anajulikana sana na anathamani kubwa kwa wenzetu i wish ningekuwa na uwezo wa upromoter lazima ningempeleka pande za huko sema imekuwa too late now na mimi mambo ya promoter yamenipita pembeni
   
 11. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi hakuwahi kupiga picha akiwa kijana tumuone alifananaje.
   
Loading...