Mjue Steve Ndaula, mmiliki wa kampuni ya BMC iliyowatapeli watu zaidi ya Sh. Bilioni 16 kisha kukimbilia Dubai

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Bwana Steve Ndaula ni kijana mdogo ambae alianzisha kampuni ya upatu/pyramid scheme ya Bestways Capital Management ambayo imewatapeli watu zaidi ya Sh. Bilioni 16 na kisha akakimbilia Dubai.

Steve alisoma chuo cha IMTU fani ya Udaktari kuanzia mwaka 2012 hadi 2017.

Mwaka 2016, mwaka mmoja kabla hajamaliza masomo yake ya udaktari chuo cha IMTU akajiunga na kampuni ya upatu ya OneCoin ambayo ilitapeli watu mamilioni ya shilingi kisha kutoweka kimiujiza na wamiliki wake kutojulikana walipokimbilia.

Baada ya kampuni ya OneCoin kufunga biashara zake Tanzania, waliokua wamiliki ama wajumbe na viongozi wengine akiwemo Bw. Steve Ndaula wakaamua kuanzisha kampuni nyingine yenye madhumuni yale yale ya upatu na kuiita BMC Ltd.

Mwaka 2020, BMC kaanza kupokea michango kutoka kwa wawekezaji wapya kwa kianzio cha Shilingi milioni 23 na kuendelea.

Kuanzia mwaka 2021 na 2022, kama ilivyo kampuni yoyote ya upatu kwamba lazima itashindwa kutoa gawio ama riba kwa wawekezaji wengine kutokana na kukosekana kwa wawekezaji wapya, kampuni ikaanza kusuasua kulipa wawekezaji. Hapo ndio baadhi ya wawekezaji wakakimbilia Polisi na kumshitaki Bw. Ndaula na kukamata baadhi ya mali zake na kuziuza na hivyo kurejesha pesa zao huku idadi kubwa ya wawekezaji ikibakia haina namna, isijue cha kufanya.

Bwana Steve alifanikiwa kuwarubuni watu wengi wanaopenda faida kubwa ama utajiri wa haraka ndani ya muda mfupi kwa kuwaahidi riba ya 6% ya uwekezaji wao kwa mwezi sawa na 72% ya riba kwa mwaka.

Baada ya mambo kuanzia kuharibika, Bwana Ndaula akaamua kukimbia nchi na sasa yuko Dubai akila maisha.

Na kwa taarifa za ndani ni kwamba wamiliki wa Kalynda walikuwemo pia watu kutoka BMC LTD.

Kwa Tanzania ilivyo, kufa maskini ni kwa ujinga wako, watanzania walivyo rahisi kuwaibia unakufaje masikini?

Soma pia:

1) Zijue platform za kimtandao zilizowahi kuwaibia watanzania

2) Watanzania wapigwa tena na Kampuni ya Upatu ya "Best Capital Management" zaidi ya Bilioni 15
 
Screenshot_20230401_183948_Chrome.jpg
 
Lakini watanzania tuna shida huwa hatuelewi hadi tutapeliwe....kila siku watu wanalizwa lakini hatukommi
Shida ndg yangu shida. Yaani tunaamini tukicheza kweli hiyo michezo tutatusua kumbe ni utapeli mwanzo mwisho.

Na wanaocheza wengi ni wa kipato cha chini, tatizo njaa.
Na wameshajua ni kichwa cha mwendawazimu kila wakati wanatutumia ujumbe wa kutuhamasisha tucheze zaidi
 
Back
Top Bottom