fungi6
JF-Expert Member
- Nov 24, 2017
- 292
- 261
Mtu alie kua mpweke mno. Hakua na mke wala mchumba wala maisha yakuchangamana na mtu yoyote yule duniani.
Huyu jamaa aliwai kua na rafiki mmoja maishani.
Alivyokua chuoni isaack newton alipata kua na rafiki mmoja tu kwa jina akifaamika kama JOHN WICKINS
urafiki wao umetokana na kua wamekua wakikutana sana njiani mda wakiwa wanatoka vipindi na kua karibu (majirani) kwenye vyumba vyao vya kuishi chuoni.kutokana na sababu hii apa ikawafanya wawe marafiki maana waliweza kuongea kwa kusalimiana mara kwa mara pale wanapo kutana.
Kwa kipindi cha miaka kazaa awa jamaa wakawa marafiki wakubwa bila kujali utata alio nao newton kwenye maisha yake. John wickin akujali ayo yote bali aliishi nae vyema kwa kua muangalizi mkuu wa newton akiwa anamuakikishia kua anakula na kupata muda wakupumzika.
Walikua wakisoma mambo ya shule kila wakati jambo ambalo walikua wanalipenda wote pamoja na pia john wickins amekua msaada mkubwa kwa crazy experiment tofauti tofauti ndani ya maabara akimsaidi newton kama assistance wake.
Ajabu nikua hawaku kaa kwa muda mrefu pamoja!!!!
hii ilitokea kwa sababu Newton hakua mtu wakujali watu hata kidogo nakuwa haoni umuhimu wao mpaka pale atakapo muhitaji mtu, kwa lugha nyepesi tunaweza sema huyu jamaa hakua akijali mtu kabisa
Baada ya John Wickins kuachana na Newton, Wickins ajawai kumuongelea kokote pale newton katika maisha yake!!!, japo watu wengi walitumai ukaribu wao na vitu baadhi walivyo fanya vitawapa majina na heshima kubwa kubwa duniani ila zote zikabaki wa newton pekee.
Inapo shangaza zaidi nikua huyu jamaa hata kwa watoto wake (John wickins) hakuwai kuwaambia kua anamfahamu newton!!!!!!!
Ila baada tu ya John wickins kuondoka Newton aliuona umuhimu wake sasa kwa maana uyu jamaa alikua anajitolea vyema kwenye maabara ya newton bila hiyana yoyote. Basi newton akaona umuhimu wa watu na kuanza kutafuta msaidizi wake kwenye maabara yake
Na uo ndo ulikua mwisho wa urafiki wao ambao hajawai tena pata rafiki wa namna hiyo
Newton hakuwai kua na maisha ya fun wala maraisi bali amekua mtu wakuhangaika tu akikosea vingi na kuoata furaha ndogo maishani ila akaishia kua mtu mashuhuri duniani.
Maisha yake yanaleta mjadala mkubwa sana duniani ukiongelea je ni vyema kuishi maisha ya anasa mbeleni au kuishi maisha magumu yakutafuta suluhisho zuri mbeleni ili kusaidia dunia na maisha yajayo?
(Hapa tunatakiwa tuwaze wenyewe)
Unadhani kuna umuhimu wakua na marafiki??
Marafiki ambao sio wa msingi sana kama maji na hewa vilivyo vya msingi katika maisha.. Ambao wachache ni wamanufaa ila wengi ni wakukukwamisha.
Basi ni vyema mtu kuchagua namna nzuri yakuishi bila kutegemeana sana kila kitu..