Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,267
Kobe ni mnyama jamii ya Reptilia ambaye kwa kumtazama tu lazima ujiulize maswali mengi.Kitendo chake cha kuficha kichwa, mwendo wake na gamba lake gumu!!
moja unayotakiwa kuyajua kuhusiana na kobe!!!
[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] hawezi kuogelea kabisa lakini anaweza kubana pumzi zake kwa muda mrefu sana!! Ukimwondoa Nng’e kobe anafuata kwa uwezo wa kuishi muda mrefu bila kupumua!!!
[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wamekuwa ulimwenguni zaidi ya miaka milioni mia mbili iliyopita!!! Ni zaidi ya mijusi na wanyama wengine!!
[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wa sasa unaowafahamu wanaweza kuishi hadi miaka mia moja!!
[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wameweza kuishi kila bara kasoro bara moja tu Antarctica!!
[HASHTAG]#Gamba[/HASHTAG] la kobe limeundwa na mifupa 60 tofauti tofauti!! Na mifupa hii yote imeungana.
[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] wa kike hutaga kati ya mayai mawili hadi kumi na mawili na huchukua siku 90 hadi 120 kuyaatamia na hatimae kutotoa.
[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] wa kike ana uwezo wa kutaga kila baada ya miaka mitatu baada ya kukutana na kobe dume!!
[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] hana hata jino moja!!
[HASHTAG]#Licha[/HASHTAG] ya kuwa na gamba gumu sana, kobe akiguswa hata na unyoya wa kuku anatambua kuwa ameguswa!! Ana hisia kali sana!!
[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] mkubwa kabisa duniani ana uzito wa kilogram mia saba.. hii inamfanya kuwa reptilia mzito kupita wote!!
[HASHTAG]#Kuna[/HASHTAG] aina 40 ya kobe!!!
Huyu ndiye kobe………