Mjue Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad tunayemlilia leo

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
IJUE HISTORIA FUPI YA MAALIF SEIF AMBAYE TUNAMLILIA LEO.

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Mwinyi ameitangazia dunia kuwa mependwa wetu na mwanasiasa wa muda mrefu ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa Rais Mhe.Seif amefariki dunia. Seif amefariki dunia akiwa anapatiwa matibu katika hospital ya Taifa ya Mhimbili.

Kama ilivyo kawaida kwa binadamu yeyote hususani mtu maarufu kama Mhe. Seif watu watatamani kujua historia yake. Leo nitawapitisha katika historia fupi ya huyu mwamba ambaye ametikisa sana katka uhai wake.

Seif alizaliwa Okotba 22, 1943. Alizaliwa kutokana na familia ya wakulima wa kijiji cha Mtambwe, nje kidogo ya mji wa Wete, Pemba. Maalim Seif alivuka bahari ya mkondo wa Pemba kwenda Zanzibar kuendelea na masomo ya sekondari kutoka 1958 hadi 1963.Alipitia shule za Uondwe na Shule ya Wavulana ya Wete kisiwani Pemba kati ya 1950 – 1957. Sekondari alisomea katika shule ya King George VI Memorial mjini Zanzibar, na aliendelea na masomo ya cheti cha cha sekondari katika shule hiyo. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salamaam kuanzia 1972 -1975 na kuhitimu na shahada ya sayansi ya siasa, utawala wa umma na mahusiano ya kimataifa.

Amekuwa katika siasa za Zanzibar tangu miaka ya 1970, akiwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na waziri wa elimu kati ya 1977 – 1980, na mjumbe mwazilishi wa baraza la wawakilishi visiwani humo. Baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 1992, Hamad pamoja na wanachama wengine wa zamani wa CCM waliunda Chama cha Wananchi CUF, na Mwaka 2020 alijiunga na ACT-Wazalendo.

Seif anatajwa kwenye siasa za Tanzania kwa kuwa alianza kuitikisa nchi hata kabla ya mfumo wa vyama vingi. Harakati zake zilianza mapema sana na kuishia kukutana na misuko suko kadhaa.

Katika medani ya siasa Maalim Seif alichaguliwa mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo aliitumikia kwa miaka 11. Katika mwaka 1984 kufuatia kile kilichojulikana kama kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Visiwani kulikoshuhudia kulazimishwa kustaafu kwa aliyekuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, Maalim Seif alichaguliwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lakini kauli zake za mara kwa mara za kuonyesha hafurahishwi na mwenendo mzima wa Muungano na kueleza Zanzibar haitendewi haki kwa baadhi ya mambo ndani ya Mungano kuliepelea kutimuliwa katika chama na pia kupoteza wadhifa wa Waziri Kiongozi kufuatia hatua hio ya chama.

Tokea wakati huo alipitia Mambo mengi na kuonekana tishio la kisiasa.Mwaka 1989 alifunguliwa mashitaka baada ya kupatikana na nyaraka za siri za serikali. Alikaa miaka miwili gerezani, Mpaka alipoachiwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.

Tanzania ilipofungua milango yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Maalim Seif na baadhi ya wenzake aliofukuzwa nao Halmashauri Kuu ya CCM walikuwa miongoni ma walioanzisha Chama chaWananchi (CUF) na kuwa Makamo Mwenyekiti wake wa kwanza na sasa Katibu Mkuu.

Aligombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, mwaka 2000 na 2005. Alishindwa kwa kura chache, lakini mwenyewe amekuwa akiamini alishinda chaguzi zote hizo na aliporwa ushindi kwa sababu Tanzania na hasa Zanzibar haijakuwa tayari kupokea mfumo wa demokrasia kwa moyo safi(Seif aliamini hivyo).

Kwa nini aliamua kujiunga na ACT-Wazalendo? Kwenye siasa za UKAWA alishiriki vipi hadi kukosana na pacha wake Prof Lipumba?

Itaendelea...
 
... wakati Maalim yuko mahututi hospitalini akipigania uhai wake, ninyi mko bize kuandaa taazia yake!
 
Back
Top Bottom