Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,371
- 14,515
Heshima zenu Wakuu, Karibuni ktk Makala hii fupi Kuhusu huyu Kiumbe.
Mamba ni miongoni Mwa Viumbe hatari Zaidi kwa maisha ya Binadamu, Mamba ameorodheshwa miongoni Mwa Viumbe 10 hatari kwa maisha ya Binadamu. Mamba hufanya mawindo yake kwa kuvizia akiwa ndani ya maji na mara chache Zaidi akiwa nchi kavu.
Kimaumbile, Mamba huwa anakuwa na nguvu Zaidi anapokuwa kwenye maji. Utafiti unaonyesha kuwa kuna aina 23 za Mamba wanaojulikana Kitaalamu na kugawanywa kwenye makundi kutegemeana na kufanana kwao kitabia na mazingira wanayopenda kuishi.
Jamii ya Mamba wanaojulikana kama "SALT WATER CROCODILE " au "Indo -pacific crocodile ",ndio wakubwa Zaidi Kuliko jamii zingine zote. Mamba wa aina hii hupatikana Kaskazini Mwa Australia, Kusini Mwa Bara la Asia na baadhi ya maeneo ya India. Tofauti na Mamba tuliozoea kuwaona kwenye mito na Maziwa, "Salt Crocodile "maisha yao ni kwenye maji ya chumvi.
Mamba mkubwa wa aina hii ya "Salt Water Crocodile " ana uzito wa kati ya kilo 1000-2000 yaani tani 1-2,Uzito ambao ni mkubwa kwa Viumbe wote wanaotambaa.
Kimsingi Mamba huweza kuishi kati y'a miaka 40 hadi 60.Mamba jike hupevuka anapofika miaka kati ya 12-14 ,wakati dume hufikia hatua hiyo anapokuwa na miaka 16.Mamba jike huweza kutaga mayai kati ya 40-90 mara Moja kutegemea na jamii zao, kwa maana ya makundi waliyogawanywa.
Mamba mrefu Zaidi anaweza kufikia futi 20,sawa na Sm 600 au mita sita (6) au Zaidi, wakati Mamba mdogo huwa na Urefu wa futi tano (5).
Kingine kinachofurahisha Zaidi kwa Mamba ni kwamba ana uwezo wa kuota meno katika muda wake wote wa maisha.
Source -Gazeti la Nipashe Jumapili, la tarehe 1-7 April 2012.Karibuni sana.