Si mtoto,ni Mamba mkubwa tu.Ujanja wa mamba ni kwenye maji ya kina kifupi,ili mamba akudake vizuri ni lazima asimike miguu na mkia kwenye tope apate "balance" ya kukuvuta na kukujeruhi.
Kwenye kina kirefu,mamba anakuwa hana nguvu,hivyo mnaweza kuzungushana kama tu una pumzi na unaweza kuogelea.Watu wa ziwa Nyasa,maeneo ya Lituhi,Lihuri na Manda Area hadi Mbaba-Bay wanajua sana kucheza na akila za mamba kwenye kina kirefu,ukienda maeneo ya Ukara huko Ziwa Nyanza hiyo michezo ya kuwakwepa mamba wanaijua sana.
Miaka fulani wakati wa Mwalimu Nyerere,tulipelekwa kisiwa cha Ukara,kule walikuwa wanasemwa kama ni "Wachawi" sana,wanatumia mpaka uchawi wa kukutumia mamba kwenye makarai ya chuma tulikuwa tukiogea zamani.Unaweza ukawa unaoga ukaona mamba ameibuka toka kwenye karai.
Watumishi wakawa hawaendi wakifika Ukerewe wakiambiwa wanapangiwa Ukara,wanaacha kazi.Kule tulienda kufanya "tafiti" ya mazingira ya wenyeji na kwanini wengi wanaogopa kwenda.Ukifika kule utajua jinsi watu wanavyomuona mamba kama kenge tu