Mjue Lucky Dube

Rlechas_3a60

Member
Oct 4, 2018
12
27
Msanii, mwanamapinduzi, mpinga ubaguzi na mtetezi wa haki za watu ambao daima wamekuwa wakionekana wanyonge Lucky Philip Dube, ambaye alifariki dunia Alhamisi ya Oktoba 18, mwaka 2007, baada ya kupigwa risasi, akiwa na wanae wawili ndani ya gari lake.

Alikuwa mmoja kati ya watu ambao huwa waliaminika kwa wateule walioletwa duniani kwa ajili ya kuifanya dunia kuwa sehemu inayofaa kuishi na hata kupewa hadhi ya dunia,

Kifo chake kilikuwa ni pigo kubwa sana kwa wanamapinduzi, kwani naamini kuwa hili ni zaidi ya ambavyo neno pigo kubwa linaweza kumaanisha si tu kwa wapenzi wa muziki wa rege, na wafuasi wa imani za kirasta, bali kwa wale wote ambao wamekuwa wakiamini katika usawa wa mwanadamu.

Wengi wanamkumbuka kwa nyimbo zake ambazo kama ilivyo ada ya nyimbo nyingi za rege zenye kuimbwa na wafuasi wa imani za kirasta, zilikuwa ni zenye kubeba ujumbe ambao ni lazima ungeweza kumgusa mtu kwa namna moja ama nyingine.

Nyimbo zake kama Think about the children (1985), Slave (1987), Together as one (1988), Prisoner (1989), Captured Live (1990), House of exile (1991), na nyingine nyingi ambazo zilikuwa zimebeba ujumbe ambao uliweza kuwatoa machozi baadhi ya watu waliokuwa wakizikiliza kwa umakini

Lucky Dube, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 43, huku albamu yake ya mwisho kuitoa ikiwa na jina la Respect ambayo ilitoka mwaka 2006, albamu hiyo ilikuwa ya 21 zikiwemo albamu 6 alizozitoa katika lugha ya Mbaqanga, na moja aliyoiimba katika lugha ya kiafrikana.

Dube, kama walivyo watu wengine wengi mashuhuri duniani, alizaliwa katika mazingira magumu baada ya baba na mama yake kutengana kabla hajazaliwa. Alikulia kwa mama yake ambaye alikuwa akiishi na nyanya wa Dube, katika kitongoji cha Ermelo mashariki mwa Transvaal, eneo ambalo kama ilivyo sehemu kubwa ya Afrika Kusini, lilikuwa limetawaliwa na ubaguzi wa hali ya juu wa rangi.

Aliwahi kufanya kazi za kutunza bustani enzi za udogo wake na katika umri huo huo wakati akiwa shuleni, yeye na marafiki zake kadhaa walijiunga na kikundi cha kwaya na kuunda bendi iliyojulikana kwa jina la Skyway band.

Katika umri wa miaka 18, Dube alijiunga na bendi ya binamu yake iliyokuwa ikijulikana kwa jina la The love Brothers, alikokuwa akipenda kupiga muziki wa kitamaduni wa kizulu uliokuwa ukijulikana zaidi kwa jina la Mbaqanga. Katika bendi hii alikuwa akifanya kazi zaidi wakati wa likizo kwani wakati huo Dube bado alikuwa ni mwanafunzi.

Albamu zake za awali mbili alizitoa katika kipindi ambapo lugha ya kiingereza bado ilikuwa ikimpa shida kidogo na baada ya albamu hizo (Lucky Dube & Super soul), Dube aliamua kwenda kujifunza zaidi lugha ya kiingereza, bila shaka baada ya kuona kuwa mafanikio yake yako katika muziki na hivyo inabidi awe msanii wa kimataifa, na hilo linamlazimu kujua lugha za kimataifa.
Ingawa albamu yake ya mwaka 1984 aliyoipa jina la Rasta never die, ilielezwa kuwa haikuwa na ubora wa kutosha katika kuirekodi, alifanikiwa kuwakamata mashabiki wa kutosha kutokana na ujumbe uliokuwa unapatikana ndani ya nyimbo zilizokuwa katika albam hiyo.
Alifanikiwa kutwaa tuzo zaidi ya 20, ikiwa ni pamoja na ile ya World Music Awards, aliyoipaya mwaka 1996 kupitia albamu yake ya Serious reggae Business, albamu ambayo pia ilimfanya atajwe na watathmini wa mauzo ya muziki huo wa rege kama msanii muuzaji bora wa muziki wa rege barani Afrika.

Wengi wetu pia tutamkumbuka Dube kama mmoja kati ya wafuasi wachache sana humu duniani wa madhehebu ya kirastafarian ambao walikuwa hawavuti sigara, hawavuti bangi na hawanywi pombe. Mbali ya muziki, Dube pia aliwahi kucheza filamu ya Getting Lucky na pia kushirikishwa na msanii wa filamu John Savage, katika filamu ya Voice in the Dark.

Aidha, Dube pia alikuwa ni mshabiki mkubwa sana wa michezo ya farasi ambapo alikuwa akimiliki shamba la wanyama na mchezo huo, katika eneo la Kwazulu Natal. Yote haya hivi sasa yamekuwa historia,

Mahakama kuu huko Johannesburg iliwahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kwa miaka 15 kila mmoja kwa kujaribu kwao wizi wa gari la Dube na hatimaye kuuwa,

Watu hao watatu waliokuwa katika gari aina ya VW Polo, huku yeye mwenyewe Dube akiwa ndani ya gari lake aina ya Chrysler, akiwa na wanae wawili ambao walisalimika katika tukio hilo.
FB_IMG_1568992776299.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom