Lucky Dube: Dunia Iliyochanganyikiwa na Uongozi

Lucky Dube: Dunia Iliyochanganyikiwa na Uongozi

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,116
Reaction score
2,732
WIMBO: Dunia Iliyochanganyikiwa
(yaani: Crazy World)
MTUNZI: Lucky dube

1. Hadi sasa, mambo yapo vizuri,
Kwa kuwa bado tunaishi,
Lakini hatujui kesho italeta nini,
Katika dunia hii iliyochanganyikiwa.
Watu wanakufa kama nzi kila siku,
Unaisoma habari kwenye magazeti,
Lakini huamini,
Utajua ukweli wake tu,
Pindi Yule mtu wa koti jeusi refu (muuaji)
Atakapobisha hodi mlangoni mwako —
Kwa kuwa wewe ndiye unayefuatia katika orodha yake.

CHORUS:
Kwa maana tunaishi ndani ya (tunaishi ndani ya)
Tunaishi ndani ya (tunaishi ndani ya)
Hii dunia ya ajabu.

2. Viongozi wanachochea vita
Wakati wowote wapendavyo —
Wengine kwa kudai haki zao,
Wengine kwa mzaha na kwa utukufu wao wenyewe.
Wakiwaacha watu wafe
Kwa makosa yao wenyewe —
Ah! Inauma kweli!

3. Haya sasa, kijana mdogo,
Omba sala zako kabla hujalala.
Kijana akapiga magoti na kusema:
Ee Bwana,
Sasa nalala usingizini,
Naomba Bwana aweke roho yangu salama,
Na kama nitakufa kabla ya kuamka,
Naomba Bwana achukue roho yangu.

Wimbo huu unatafakarisha sana. Hapa ni sehemu ya ubeti:

" Leaders starting wars any time they want"
👉Viongozi wanachochea vita wakati wowote wanavyotaka.

Some for their rights, some for fun and their own glory
👉Wengine kwa kudai haki zao, wengine kwa furaha yao na utukufu wao wenyewe

Letting people die for the wrong that they do
👉Wakiwaacha watu wafe kwa makosa yao wenyewe.

Hii ni sehemu nyingine yenye nguvu katika wimbo huu wa Crazy World. Ubeti huu unaangazia moja kwa moja ukandamizaji na uongozi mbaya, ambapo viongozi wanatumia nguvu zao kuanzisha vita, si kwa manufaa ya watu, bali kwa ajili ya haki zao binafsi, utukufu na urithi wa kibinafsi, hata kama vita hizo zinaua watu wasio na hatia.

Hiki ndicho tunachokishuhudia Congo, Tunachoshuhudia Sudan, Palestina, Ukraine na Sehemu nyingine.
Lucky Dube anatoa wito kwa viongozi kuwa na huruma na kutambua kuwa maamuzi yao yana madhara kwa watu wa kawaida. Viongozi wanapaswa kutumia nguvu zao kutatua migogoro kwa amani na kwa maslahi ya umma, si kwa manufaa yao binafsi.

Kwa kifupi, wimbo huu ni wito wa kimataifa dhidi ya uongozi wa kiubinafsi, na kuhusu mahitaji ya mabadiliko ya kweli ambayo yataleta amani na ustawi kwa wote, badala ya vita na maumivu yasiyo na mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom