C.T.U
JF-Expert Member
- Jun 1, 2011
- 5,074
- 3,735
Ghost/ Vanishing hitchhiker ni Urban Legend ambayo ni maarufu sana ulaya na marekani ni story ambayo inamhusisha mwanaume mmoja ambaye alikuwa anaendesha gari lake mida ya usiku mrefu
katika safari yake alikutana na mwanamke ambaye alikuwa mwenyewe barabarani usiku
kwa imani yule jamaa alifunga breki na kumuuliza kama anahitaji lift
yule dada akakubali na hapo hapo akaingia kwenye gari...
jamaa akaendesha gari lile kwa muda mrefu lakini cha ajabu ni kuwa punde yule dada alipopanda kwenye gari alihisi kuna ubaridi sana
yule jamaa aliamua kumuuliza anaenda wapi na yule dada akajibu kuwa anataka kwenda kwao kwa maana hajafika kwa muda mrefu sana
jamaa akamuuliza kwao ni wapi na yule dada bila ajizi akamuelekeza nyumbani kwao
mwanaume yule akakanyaga gia mpaka nyumbani akamfikisha salama na kumwambia yule dada kuwa wakutane siku nyingine kwani uchu wa mapenzi ulianza kumshika bwana yule
yule dada akapeana nae ahadi na baada ya hapo akashuka kwa ajili ya kwenda kwao yule jamaa akamsindikiza kwa macho mpaka anaingia ndani kabisa yule dada huku akimthaminisha uzuri wake na mate ya uchu yakimtoka bwana yule
alivyotaka kuondoka kuna kitu cha ghafla kilitokea na kikamfanya ahairishe safari yake "scarf" ya yule dada ilikuwa imebaki ndani ya gari..
akaamua aichukue na kumpelekea hivyo akanyoosha moja kwa moja mpaka kwa kina dada yule akagonga mlango
mlango ulivyofunguliwa kitu kisicho cha kawaida kilimshtua kwa kuwa yule dada alikuwa wa mwisho kuingia na alitegemea alipogonga basi yule dada angekuja kumfungulia ila haikuwa hivyo
mama mmoja wa makamo alikuwa kufungua mlango yule
jamaa akamuuliza mrembo yule lakini yule mama alibaki kumshangaa, kwani nyumbani pale anaishi yeye na mumewe tu hakuna mtu mwingine anayeishi pale na saa zile walikuwepo nyumbani na hakuna mtu yeyeote aliyeingia
Yule jamaa akashtuka
jamaa akajitutumua tena na kusema kuwa kuna mdada alimpa lift na kusema kuwa aliacha scarf na scarf yenyewe ni hii hapa akamuonyesha yule mama
ghafla yule mama alianza kulia tena kwa nguvu, akamuita mumewe mumewe akabaki anashangaa, tena akawa anashangaa kuiona ile scarf
yule bwana akadadisi kuwa kunani?
wakamwambia kuwa ile scarf ni ya binti wao ambaye alifariki miaka mingi iliyopita na wakati anafariki alikuwa amevaa hiyo scarf
jamaa hakuamini masikio yake akauliza tena kama wana picha ya yule binti na familia ile wakampeleka mpaka sehemu ambayo wameweka picha ya yule binti yao aliyefariki miaka mingi iliyopita
TOBAAAA.......
ni yule binti aliyempa lift dakika tano zilizopita hivyo ni kuwa jamaa alibeba jini? au alibeba mzimu? au mzuka?
jamaa alizimia hapo hapo
story hii ikawa maarufu sana na kupewa jina la Ghost Hitchhker
video yake ni hii hapa jionee mwenyewe
ENJOY