Mjue Chuma Ulete wa Biashara yako

Mjue Chuma Ulete wa Biashara yako

Chuma ulete ipo tena sana tu, na kuendesha biashara bila kuweka kumbukumbu pia kupo. Chuma ulete ndio kiboko.
 
Moja ya changamoto ambazo zinasumbua biashara ndogo ni imani ambazo wafanyabiashara wanazo. Kuna dhana moja ipo kwenye mitaa yetu kwamba kuna watu ambao ni chuma ulete. Watu hawa wanapokuja kwenye biashara yako na kununua kitu, ukiwarudishia chenchi basi baadaye wanahamisha fedha zote kwenye biashara yako kwa nguvu za kishirikina.

Watu wamekuwa wakihofia sana hili na hivyo kukataa kabisa kuwauzia baadhi ya watu ambao wanajulikana kama chuma ulete au wakiwauzia basi fedha zao wanaziweka pembeni, wanazitenga kabisa na fedha nyingine.

Mwanzoni nilipokuwa nasikia haya kutoka kwa wafanyabiashara nilikuwa nafikiri ni kitu cha utani tu, kwamba wanatania, lakini kila siku ninapokutana na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya ushauri au mafunzo, hili la chuma ulete huwa halikosekani. Kuna wakati mpaka nimesikia likijadiliwa kwenye vipindi vya redio na televisheni, watu wakilalamika kwamba mitaa fulani huwezi kufanya biashara kwa sababu wapo watu hao wanaofahamika kama chuma ulete.

Je chuma ulete wapo?
Swali muhimu la kuanza nalo kwenye makala hii ya leo ni je chuma ulete yupo? Je kuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete?

Mwanzoni nilipokuwa naulizwa swali hili kuhusu chuma ulete nilikuwa nawakatalia watu kabisa ya kwamba hakuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete. Nilikuwa nawaambia watu kwamba ni imani zao tu ndiyo zinawasumbua, hakuna chuma ulete yeyote ambaye anawachukulia fedha zao kwenye biashara.

Lakini baadaye nikaanza kujiuliza kama chuma ulete hakuna, iweje watu wanapata hasara kwenye biashara zao? Iweje mtu mwisho wa siku yake wakati anapiga mahesabu anakuta amepata hasara kubwa? Hapa ndipo niliposhawishika kwamba lazima kutakuwa na chuma ulete.

Je chuma ulete wa biashara yako ni nani?
Baada ya kushawishika kwamba chuma ulete yupo, hatua iliyofuata ilikuwa kumjua chuma ulete kwenye biashara ndogo ni nani. Na hapa nilikuja na jibu ambalo lilinishangaza, kwa sababu lilikuwa na jibu la kweli ambalo likifanyiwa kazi chuma ulete huyo anakimbia kabisa. Jibu nililopata ni kwamba chuma ulete wa biashara zote ndogo ni mfanyabiashara mwenyewe. Ndiyo, yaani kama wewe ulishapatwa na chuma ulete kwenye biashara yako, basi chuma ulete huyo ni wewe mwenyewe.

Hakuna mtu mwingine anayeweza kutoka nje ya biashara yako na kuweza kuchukua fedha kwenye biashara yako kwa njia za kishirikina. Fedha kwenye biashara yako zinaweza kutoka kwa njia mbili pekee, njia ya kwanza ni wewe uzitoe mwenyewe, na njia ya pili ni uzipoteze kizembe. Chuma ulete ni pale ambapo unapoteza fedha kizembe kwenye biashara yako.

Kabla hujakataa kwamba wewe siyo chuma ulete wa biashara yako, na kuendelea kusisitiza kwamba kuna watu wanakuja kwenye biashara yako na kuchukua fedha kwa njia za ajabu, naomba ujiulize swali hili; ulishawahi kusikia benki inalalamika kwamba wameibiwa fedha kwa chuma ulete?

Umeshawahi kusikia biashara kubwa, kama makampuni wakilalamika kwamba kuna chuma ulete wanawaibia fedha? Kwa nini unafikiri ni biashara ndogo pekee zinazoandamwa na chuma ulete? Kama chuma ulete wangekuwa na nguvu hiyo ya kuchukua fedha kwa nguvu za ajabu, je unafikiri wangechukua fedha wapi, kwenye biashara yako ndogo au kwenye mabenki ambayo yana fedha nyingi?

Chuma ulete hawapo kwenye mabenki wala biashara kubwa kwa sababu kule kila kitu kinaendeshwa kwa taratibu. Hakuna fedha inayotolewa bila ya maandishi, hivyo mwisho wa siku kila kitu kinaonekana kimekwendaje, na mzunguko wote wa fedha unaonekana.

Lakini wewe kwenye biashara yako fedha inazunguka bila ya mahesabu yoyote, ukitaka kununua kitu unatoa kwenye droo na kununua, nyumbani wakitaka fedha ya matumizi unatoa na kuwapa, akija mtu kukopa unachukua na kumpa. Unakuwa unajiambia baadaye utakumbuka, lakini kwa uchovu wa siku nzima, inapofika jioni huwezi tena kukumbuka kila kitu ulichofanya kwenye biashara yako kwa siku nzima.

unafanya mahesabu na kugundua kuna hasara imejitokeza, na moja kwa moja unafikiria chuma ulete tayari wamekuibia. Nafikiri unaanza kupata picha ni kwa namna gani wewe mwenyewe ni chuma ulete wa biashara yako.

Je unawezaje kuondokana kabisa na chuma ulete kwenye biashara yako?
Wahenga walisema, mali bila ya daftari, hupotea bila ya habari. Hii ndiyo dawa pekee ya chuma ulete kwenye biashara yako. Usikiamini kichwa chako na kufikiri utakumbuka kila kitu kwenye biashara yako, badala yake kuwa na daftari, na kila kitu kinachofanyika kwenye biashara yako kiandikwe. Andika kila fedha inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, andika kila mali inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, na mwisho wa siku fanya mahesabu kuona kama mambo yanakwenda sawa, kwamba kilichotoka na kuingia kimekwenda sawa na mahesabu yaliyopo kwenye biashara.

Kitu kidogo kama daftari kinaweza kuikoa sana biashara yako, kama utakitumia vizuri na kuzingatia, utaweza kuwa na udhibiti mkubwa wa mzunguko wa fedha kwenye biashara yako. kumbuka fedha ndiyo damu ya biashara yako, hivyo ilinde kwa uwezo wako wote ili biashara yako iweze kustawi na kukuletea mafanikio.

Wewe ndiye chuma ulete wa biashara yako kwa kukubali kuendesha biashara yako kizembe bila ya kuwa na kumbukumbu sahihi za kibiashara. Ili kuondoa hali hii ya chuma ulete kwenye biashara, hakikisha unakuwa na kumbukumbu sahihi za biashara yako. usichukulie mambo kirahisi, huko ndiyo kunakuletea hasara kila siku.
Nakushauri Ndugu yangu Badilika.
Kila la kheri.
We jamaa hujui lolote kwenye biashara zaidi ya kuuza maneno tu,unaongelea mabenki sijui makampuni,wakati chuma ulete wanakaba kwenye biashara za mtaani,nenda yombo dovya kafungue duka la rejareja uone mziki wake,usipojipanga utalizwa...binafsi njia ya kukabiliana na hawa watu ni kuweka bible kwenye droo la hela za mauzo hapo unapeta tu hata waje chuma ulete 100 hawafui dafu
 
Ulivotoa mfano wa mabenki tuu nmekuouuza. Yaan hauna ujifunzalo. Ukitaka kuhakikisha kafanye biashara. Utagundua.

Ndugu yangu lisemwalo lipo watu hawawezi kujitungia tuu uwongo kwa maslah ya naani kwanza??
 
Mimi nimetoa mtazamo na kile nnachokijua kuhusu biashara. kama na ww wajua zaidi ya hapo nipe elimu hasa kuhusu huyo mzee Sadick.
Chuma ulete ipo na yupo karudie huo utafiti wako Mkuu!
 
Moja ya changamoto ambazo zinasumbua biashara ndogo ni imani ambazo wafanyabiashara wanazo. Kuna dhana moja ipo kwenye mitaa yetu kwamba kuna watu ambao ni chuma ulete. Watu hawa wanapokuja kwenye biashara yako na kununua kitu, ukiwarudishia chenchi basi baadaye wanahamisha fedha zote kwenye biashara yako kwa nguvu za kishirikina.

Watu wamekuwa wakihofia sana hili na hivyo kukataa kabisa kuwauzia baadhi ya watu ambao wanajulikana kama chuma ulete au wakiwauzia basi fedha zao wanaziweka pembeni, wanazitenga kabisa na fedha nyingine.

Mwanzoni nilipokuwa nasikia haya kutoka kwa wafanyabiashara nilikuwa nafikiri ni kitu cha utani tu, kwamba wanatania, lakini kila siku ninapokutana na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya ushauri au mafunzo, hili la chuma ulete huwa halikosekani. Kuna wakati mpaka nimesikia likijadiliwa kwenye vipindi vya redio na televisheni, watu wakilalamika kwamba mitaa fulani huwezi kufanya biashara kwa sababu wapo watu hao wanaofahamika kama chuma ulete.

Je chuma ulete wapo?
Swali muhimu la kuanza nalo kwenye makala hii ya leo ni je chuma ulete yupo? Je kuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete?

Mwanzoni nilipokuwa naulizwa swali hili kuhusu chuma ulete nilikuwa nawakatalia watu kabisa ya kwamba hakuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete. Nilikuwa nawaambia watu kwamba ni imani zao tu ndiyo zinawasumbua, hakuna chuma ulete yeyote ambaye anawachukulia fedha zao kwenye biashara.

Lakini baadaye nikaanza kujiuliza kama chuma ulete hakuna, iweje watu wanapata hasara kwenye biashara zao? Iweje mtu mwisho wa siku yake wakati anapiga mahesabu anakuta amepata hasara kubwa? Hapa ndipo niliposhawishika kwamba lazima kutakuwa na chuma ulete.

Je chuma ulete wa biashara yako ni nani?
Baada ya kushawishika kwamba chuma ulete yupo, hatua iliyofuata ilikuwa kumjua chuma ulete kwenye biashara ndogo ni nani. Na hapa nilikuja na jibu ambalo lilinishangaza, kwa sababu lilikuwa na jibu la kweli ambalo likifanyiwa kazi chuma ulete huyo anakimbia kabisa. Jibu nililopata ni kwamba chuma ulete wa biashara zote ndogo ni mfanyabiashara mwenyewe. Ndiyo, yaani kama wewe ulishapatwa na chuma ulete kwenye biashara yako, basi chuma ulete huyo ni wewe mwenyewe.

Hakuna mtu mwingine anayeweza kutoka nje ya biashara yako na kuweza kuchukua fedha kwenye biashara yako kwa njia za kishirikina. Fedha kwenye biashara yako zinaweza kutoka kwa njia mbili pekee, njia ya kwanza ni wewe uzitoe mwenyewe, na njia ya pili ni uzipoteze kizembe. Chuma ulete ni pale ambapo unapoteza fedha kizembe kwenye biashara yako.

Kabla hujakataa kwamba wewe siyo chuma ulete wa biashara yako, na kuendelea kusisitiza kwamba kuna watu wanakuja kwenye biashara yako na kuchukua fedha kwa njia za ajabu, naomba ujiulize swali hili; ulishawahi kusikia benki inalalamika kwamba wameibiwa fedha kwa chuma ulete?

Umeshawahi kusikia biashara kubwa, kama makampuni wakilalamika kwamba kuna chuma ulete wanawaibia fedha? Kwa nini unafikiri ni biashara ndogo pekee zinazoandamwa na chuma ulete? Kama chuma ulete wangekuwa na nguvu hiyo ya kuchukua fedha kwa nguvu za ajabu, je unafikiri wangechukua fedha wapi, kwenye biashara yako ndogo au kwenye mabenki ambayo yana fedha nyingi?

Chuma ulete hawapo kwenye mabenki wala biashara kubwa kwa sababu kule kila kitu kinaendeshwa kwa taratibu. Hakuna fedha inayotolewa bila ya maandishi, hivyo mwisho wa siku kila kitu kinaonekana kimekwendaje, na mzunguko wote wa fedha unaonekana.

Lakini wewe kwenye biashara yako fedha inazunguka bila ya mahesabu yoyote, ukitaka kununua kitu unatoa kwenye droo na kununua, nyumbani wakitaka fedha ya matumizi unatoa na kuwapa, akija mtu kukopa unachukua na kumpa. Unakuwa unajiambia baadaye utakumbuka, lakini kwa uchovu wa siku nzima, inapofika jioni huwezi tena kukumbuka kila kitu ulichofanya kwenye biashara yako kwa siku nzima.

unafanya mahesabu na kugundua kuna hasara imejitokeza, na moja kwa moja unafikiria chuma ulete tayari wamekuibia. Nafikiri unaanza kupata picha ni kwa namna gani wewe mwenyewe ni chuma ulete wa biashara yako.

Je unawezaje kuondokana kabisa na chuma ulete kwenye biashara yako?
Wahenga walisema, mali bila ya daftari, hupotea bila ya habari. Hii ndiyo dawa pekee ya chuma ulete kwenye biashara yako. Usikiamini kichwa chako na kufikiri utakumbuka kila kitu kwenye biashara yako, badala yake kuwa na daftari, na kila kitu kinachofanyika kwenye biashara yako kiandikwe. Andika kila fedha inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, andika kila mali inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, na mwisho wa siku fanya mahesabu kuona kama mambo yanakwenda sawa, kwamba kilichotoka na kuingia kimekwenda sawa na mahesabu yaliyopo kwenye biashara.

Kitu kidogo kama daftari kinaweza kuikoa sana biashara yako, kama utakitumia vizuri na kuzingatia, utaweza kuwa na udhibiti mkubwa wa mzunguko wa fedha kwenye biashara yako. kumbuka fedha ndiyo damu ya biashara yako, hivyo ilinde kwa uwezo wako wote ili biashara yako iweze kustawi na kukuletea mafanikio.

Wewe ndiye chuma ulete wa biashara yako kwa kukubali kuendesha biashara yako kizembe bila ya kuwa na kumbukumbu sahihi za kibiashara. Ili kuondoa hali hii ya chuma ulete kwenye biashara, hakikisha unakuwa na kumbukumbu sahihi za biashara yako. usichukulie mambo kirahisi, huko ndiyo kunakuletea hasara kila siku.
Nakushauri Ndugu yangu Badilika.
Kila la kheri.
Utakua wewe ndie Mkuu wa Chuma ulete so unatetea... Bank ndipo kuna chuma ulete za kufa mtu kawaulize wale maTeller huwa wanalia kila siku na wengi walishindwa kulipa majazio ya hasabu za siku wamefukuzwa makazini bila kujilinda kazi ya u Teller ni hatari mno... Nenda Bank yeyete kawaulize Mateller kuhusu Chuma ulete and then lete thread nyingine humu JF.

Kuna chuma ulete wa mitaani wao huomba coin za mia mia ogopa sana hao
 
Aisee kumbe mateller wanaisoma
 
Usaiache hela kwenye draw/kibox zaidi ya chenji ndogo ndogo
 
Una point nzuri sana ila kuna ukweli ulio wa kina sana unapaswa kuujua nikipata nafasi nitaeleza
 
Leo nakili kabisa chuma ulete ipo tena ipo nimetoka kupigwa pesa zangu sasa hv yaani sikuwa nikiamini aya mambo kabsa lakini Leo kilicho nitokea nakubali chuma ulete noma...
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza, hiyo mada ni mtazamo wako wa kishule shule ila kiuhalisia umepotoka.sumaku za kijadi zipo yaani hii sayansi ni ya kipekee.
Usiongee kama haujawahi kukutana nayo.
Mtaani wapo kibao haswa wale wa elfu kumi kwa kitu cha mia tatu au kuomba chenji
 
Leo nakili kabisa chuma ulete ipo tena ipo nimetoka kupigwa pesa zangu sasa hv yaani sikuwa nikiamini aya mambo kabsa lakini Leo kilicho nitokea nakubali chuma ulete noma...
Peleleza vzuri, kuna mtu ana access na unapotunzia pesa amejichukulia
 
kijitu kimeajiriwa uko,kimezoea kujadili madaraja na nyongeza afu leo kinafundsha wafanyabiashara eti hakuna chuma ulete,pumbaaavu(in ray kigosi voice),,ingia mtaani uanZishe biashara uone,,hafu siku hizi hadi bodaboda wana chuma ulete,,akikupa chenchi ujue inarudi kwake,,huku kuna watu wana madude ya naijeria wanaingiza hadi millioni kwa siku,,,wew rizika na tgts zako,kuchomekea na kuwahi asubuhi kazini,,lakini sio kujifanya kuzungumzia chuma ulete kua haipo wakati ata biashara hufanyi... N:B..mimi kama mimi nshabutuliwa M3..nlishtuka kumekucha...hapo nikakubali kujifunza madarasa ya mtaani...wachaa kabisa nakwambia usiombe yakukute
 
Acha kuongopa mkuu Yani chuma ulete wakakupiga m3 hivihivi lete ufafanuzi....???
 
Back
Top Bottom