Ama kweli mjini shule!
Binti mmoja alikuwa akitaka kumuingiza mjini bwanake mmoja. Akatuma
meseji hivi: "Baby ninataka kununua jeans moja nzuri lakini tatizo
nimesahau pochi nyumbani." Baada ya dakika kadhaa meseji ikaingia kwenye
simu ya binti: "Umepokea Shilingi 600 kutoka kwa Jofu. Binti akatuma
meseji tena: "Jamani Baby, sasa hii 600 ya nini wakati jeans inauzwa
50,000!" Jamaa akajibu meseji: "Shilingi 300 nauli ya kwenda kufuata
pochi nyumbani na Shilingi 300 nyingine ni nauli ya kurudi kununua
jeans!. Du kasheshe.