Mjini raha

Hahahahahahahahahaha na mafuriko yakianza je si mnalala shuleni?hili hata hawalijui ila wanajua mko mjini.
Haahahahahahahaha nani atawaambia mambo ya mafuriko wakati sote twaishi masaki na oysterbay we vipi. Tena ukifika kijijini wanauliza he wamjini wamefika wanakaa jirani na mkuu wa nchi . Skwambii hizo heshima unazopewa kama msaidizi wa mkuu wa nchi vile. Tena ukiwachanganyia kile Kiswahili cha uswazi mamamamamamama uuuuuiiiiiiiiii . Hata ukitaka kuchochea chungu cha ugali wanakuambia acha utaungua wewe wa mujini. Wangejua kwa mfuga mbwa huwa tunapikia mkaa wangeisoma. Kila wakitaka mwaliko unawatolea nje ama kweli siri ya mtungi aijuae kata.
 

Hapa ndo mjini kila mtu mjanja na kila mtu wa masaki........kila mtu ni kubwa kuliko. Haha na waje tuwe wengi si unaona mabasi yanayotoka mkoani kila siku yanakuja yamejaa??
 
nsaidie kumwelewesha dada mkubwa wangu!
we nahisi anaweza akakuelewa!
mimi alishakariri ni toto tundu tu toka enzi!so hata nikiongea cha ukweli
anabaki kusali novena kuniombea kwa mama wa huruma nibadilike!
Mjini kila mtu profesa bwana. Tena nini unachohitaji usikipate mpaka vyeti sijui vya nini nini vinapatikana pesa yako tu. Hata waganga wa kienyeji wanakuja mujini kijijini kwenye uhitaji mkubwa wa kinga ya kuzuia wachawi wasiibe mazao kichawi wanapakimbia. chezea chai wewe . Pacha wangu atazoea taratibu na wa namna hii wakishajua utamu wa mjini bwana itakua tabu kumwabia turudi kijijini.
 
enhe manake hao ndo wanahusika na vizazi na vifo!
watu tukutane kariakoo kwenye english gold af unajifanya unanijua sana!
ahahahahha HEB NIPISHE MIE!

hehehe na baadae mlikutana pia kwenye harusi ya Mama Mushka kule tandale....!! Na dua waliloomba sidhani kama litampata mwewe!! mwewe ashaakwapua kifaranga muda huu anamalizia miguu nyie mmebaki na oohh Mungu atamlipia MTASUBIRI SANA!! WANASEMA UJANJA NI KUPATA SI KUWAHI.
 
ha haa, we mdogo wangu kweli umefika mujini.......
huko ni majanga bana, mi sitaki.
hivi naweza shindana na akina cacico kweli? si ni kujitafutia pressure bure?
 
Last edited by a moderator:
Tena nakumbuka hizo lesswig kijijni kwetu wanaziita nywele za walio R.i.P mweee. Kweli mjini shule jamani shamba kilimo. Yaani mujini unavaa viatu kama nyumba lol kijijini unapekua tu au unavaa viatu vya matairi navyo kama vipi unavivua na kuendelea peku. Mujini mr anakwambia I love you , darling na mengine mengi nani anataka kuambiwa mama maganga nalekotogwa sana ie mama maganga moyo wangu umekudondokea wote. Mjini wanalalia vianda , kijini kwetu thubutu ni vitanda vya kamba kwa kwenda mbele.
 
Hapa ndo mjini kila mtu mjanja na kila mtu wa masaki........kila mtu ni kubwa kuliko. Haha na waje tuwe wengi si unaona mabasi yanayotoka mkoani kila siku yanakuja yamejaa??
Na wakija kututafuta simu haipatikani kwani si unajua hata kula yetu ya tabu kidogo, mpaka tuuze mihogo ya kutafuna na matango. Nani anataka mzigo ooh mamdogo sijui nataka kusoma , utafanywa hg bila malipo chezea mjini wewe. Ukiulizia sana mshahara wako utaambiwa unawekewa bank wewe. Sasa jiulize huko bank wewe huwezi kuweka au siku hizi account inafunguliwa tu bila muhusika kuwepo. Na ukizidisha kiburi utaletewa mpaka kadi ya AtM mwe lkn password hautapewa maana wewe huwezi kutunza pesa kumbe ni changa la macho.
 
Mimi mbona kijijini kwetu nakupenda sana, almost everything i use in town i get there,
mara nyingi nakumis sana village, majukumu tu ndio yanabana siweze kukaa sana.
I love my home village Katangara Rombo.
 
ha haa, we mdogo wangu kweli umefika mujini.......
huko ni majanga bana, mi sitaki.
hivi naweza shindana na akina cacico kweli? si ni kujitafutia pressure bure?
My twin raha ya mujini usiingie kwenye mashindano hakuna wa kukubughudhi ni mpaka utakapotaka kuingia anga za watu
 
Kinachonifurahisha zaidi mjini ni kwamba kila mtu kasoma hakuna aliyeishia la saba jamani. Tena usipende kuuliza kazi za watu utabaki mdomo wazi. Unajiuliza kwanini ikifika jioni pilika pilika zinaongezeka hasa kwa wadada. Asubuhi wanaamka saa saba mchana na kupata kikombe cha chai na andazi moja chakula cha mchana akili mukichwa, nimeamini bongo/dar kuna vyuo vingi jamani
 
Mjini kuna raha zake bandugu, hata omba omba hawashindi njaa, uongo jioni elfu 3 hakosi, kijijini ushaona omba omba barabarani?

Kwa suala la mishemishe mjini kuna faa hiyo inatokana na wingi wa watu na kuwepo na mzunguko wa fedha wa haraka, lakini kwa utulivu kijijini kuna raha yake.
 
Hivi mnajua kwamba mji una masharti? ukikosea masharti utauona mchungu....mnaokuja mjini jipangeni na mtii masharti, ohooooooo
 
Hivi mnajua kwamba mji una masharti? ukikosea masharti utauona mchungu....mnaokuja mjini jipangeni na mtii masharti, ohooooooo
Hivi sharti la kwanza ni lile linalosema eti mjini wanuome wote ni beibi au naona kama sikukariri vizuri wakati bus linaingia mujini nadhani kwa sababu mimi mwanamke.
 
Hivi sharti la kwanza ni lile linalosema eti mjini wanuome wote ni beibi au naona kama sikukariri vizuri wakati bus linaingia mujini nadhani kwa sababu mimi mwanamke.

Kumbe unajua baadhi ya masharti, pili mjini hakuna undugu
 
Pia inategemea na kitaa unachoishi huku ninakoishi kila mara kuna matarumbeta ya msuto lol mpaka tumezoea.
ha haaa hapo sasa
ngoja niangalie uwezekano wa kupata nyumba jirani na Magogoni, lol!
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…