Mjini raha

Mjini raha

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,161
Mjini raha kweli kweli, kijijini mimi sirudi mwenzenu. Tutabanana hapa hapa. Kwani nani asiyependa kupanda daladala, kutumia maji ya bomba kuogea badala ya kuogea mtoni, kupikia gesi badala ya kupikia mkaa/kuni, kwani nani asiyependa kutembea kwenye barabara ya lami badala ya kutembelea kwenye udongo mwekundu ? kweli kabisa mimi kijijini sirudi.

Tutabanana hapa hapa. Wewe utarudi kweli?
 
naona wa born here here haituhusu.
Ila Mrembo by Nature ujue kijijini raha sana yaani kuku mweupe anachemshwa na chumvi tu ila mtamu balaa
siyo huku makuku yetu ya rangi

Mimi nimetia nanga kijijini sirudi, beach ningeionea wapi kama sio kuwa mjini? ningejuaje facebook kama sio mjini, instagram je?blog ya ma mkubwa je? Mwenzenu killage sirudiiiiiii waache wale kuku wa kienyeji mtamu ila huku raha sana
 
nikiwa zangu mitaa ya banana ma do, wanapita wa kila aina kama wanyama mbugani
 
mjini ndo mpango....mjini shule kijijini tuisheni.
 
Kijijini sembe iwepo?wanaitoa wapi? mijini raha hasa ukimpata bwana muuza sembe anayeweza badilisha status from unknown to known....hehehe msinisute mie.
 
Na sisi tuliozaliwa mjini tusemeje?! Ha! ha! haaaaaaaaa!! napita tu nikipata nauli nitarudi......!!
 
Kijijini sembe iwepo?wanaitoa wapi? mijini raha hasa ukimpata bwana muuza sembe anayeweza badilisha status from unknown to known....hehehe msinisute mie.
eti ulimwibia shogako ule hela za dona 1
 
Mjini raha ila ninachoogopa ukimpata bwana mwenye hela haishi kuwindwa na mashoga zako....hapo tu ndo patanifanya nikimpata wa hivyo nikamfiche kijijini kwanza wasimuibe manake wanaume wameadimika
 
eti ulimwibia shogako ule hela za dona 1

Heeehh aliibwa alichukuliwa mwenyewe na akatembea kwa miguu yake miwili? hapo ni karata zilichezwa vizuri. Ukiona mjinga analia jua kuna mjanja anacheka. Ushoga wa kweli ni kijijini tena ushoga ule wa kusukana nywele chini ya miembe. Mjini tunakutana kimisheni town tu likiwepo dili watu wanageukana fasta, kwani hujui???chezeya mjini wewe, sema ndo tatizo la town bwana lazima umfiche manake wakijua zimo hawaishi kukupindua. Wtamganda weee kama inzi, mara oohhh shemeji naomba mkopo, shemeji mwanangu anaumwa naomba lift ya hospo....akikaa sawa mara kakosea kutuma meseji ya mapenzi imeingia kwa shemeji, mara ndoa, haoooo umeachwa solemba.

Mjini mipango.
 
Back
Top Bottom