Mjini kuna wenyewe

Mjini kuna wenyewe

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
MOYO WANGU TULIA.

1)Sitaki tena sitaki,moyo wangu usumbuke.
Sitaki nipate hiki,rohoni nihangaike.
Sitaki nipate kiki,wa jamii wanicheke.
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

2)moyo wangu funga macho,vya watu visikuteke.
Penda hiki ulonacho,rohoni uburudike.
Chako pekee kificho,ndo bahati ubahatike.
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

3)so kwamba ninaogopa,ila heshima nachunga.
Leo pale kesho hapa,hilo jambo la kijinga.
Moyo hutotoka kapa,tulia ile mpunga.
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

4)acha niunde vya kwangu,ili vije kupendeza.
Niseme hivi ni vyangu,vile nilotengeneza.
Vilivyo chaguo langu,si hivi vya kunguza.
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

Shairi=MJINI KUNA VYA WATU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 
sisi wenye moyo mashine hatuna haja ya kuutuliza utatulia tu😀😀😀
 
Back
Top Bottom