Mjinga na Mwelevu katika usaili.

Aug 4, 2015
28
13
Mwelevu na Mjinga walienda ktk usaili, walipofika
kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Mwerevu
kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote wapate
kazi.
Basi Mwelevu akaingia na maswali yakawa hivi:-
Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?
Mwelevu:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila
ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu
mbalimbali..
Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa
Uhuru huo?
Mwelevu:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl.
J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.
Msaili:- Inasemekana ktk sayari ya Mars
kunaviumbe wanaishi, je ni kweli?
Mwelevu:- Watu wengi wanasema hivyo lakini
haijathibitishwa na wanasayansi.
Baada ya Mwelevu kutoka basi Mjinga akapewa
majibu yote..
Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-
Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwka gani?
Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa
mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu
mbali mbali.
Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?
Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J. K.
Nyerere ndiye alikuja kumalizia .
Msaili:- Hivi wewe ni chizi?
Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini
haijathibitishwa na wanasayansi..😂😂😂😂😝😝😝
 
Back
Top Bottom