Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Msimamizi wa uchaguzi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Kheri Mkamba, leo ameongoza zoezi la kuanza kwa uchaguzi wa kura za maoni katika Kata ya Mjimpya, Manispaa ya Morogoro.
Pichani Mkamba akionyesha sanduku la kura pamoja na kura ambazo bado hazijapigwa, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uwazi na uaminifu kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.
Uchaguzi huo unalenga kumpata mgombea wa nafasi ya Diwani wa Kata ya Mjimpya na Mbunge watakaokiwasilisha Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.