Mji wa Muheza haulingani na vichwa vyake vilivyopo serikalini, tatizo ni nini?

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,717
Yaani nikiangalia huu mji au hii wilaya ya Muheza kwamba ina watu wengi kidogo walioshika nyadhifa serikalini na kwenye taasisi kubwa za serikali. Ila mimi nimeutembelea huu mji lakini sioni uhalisia kabisa.

Mfano tu huyu mkuu NHC Mchechu nasikia ni wakule, hawa nao wasikia sasa akina Kijazi ni majina ya Muheza halafu hata Mbunge wao wa sasa ni waziri na alishawahi kuwa mpaka Balozi.

Ila sasa pamoja na hayo yote huu mji kila napoutembelea sioni chochote cha maana japo ka mji kamekuwa lakini hakuna swagger za kukuonesha kwamba kuna vigogo wa serikalini wanatoka hapo. Huwezi ona nyumba ya kutisha na mahekalu. Yaani kumekaa ki uswahili uswahili tu. Nyumba za hovyo hovyo. Ukikutana na nzuri basi uzuri wake ni wakawaida kabisa. Mfano tu mimi ni mtu Moshi na juzi nimetoka huko kibosho ila ki ukweli hekalu ambazo zipo kibosho Muheza hata tano hazifiki.

Tatizo haswa ni nini wabondei wa Muheza?? Mmejaliwa vichwa na viongozi wakubwa serikalini na kwenye mashirika na hata wafanyabiashara mnao ila ni kwanini mnakosa akili ya kupendezesha mji wenu???
 
Padeshee Mhita ni wa wapi?? Jana nilimwona akimwagia pesa Mzee Mahita kwenye birthday yake.. Alafu dadake ni mbunge wa huko viti maalum na huyo dogo Muhaji anataka kugombea 2020
 
Mimi ni mmbondei wa Muheza. Wabondei ni moja ya makabila ya mwanzo kupata elimu. Waingereza walianzisha kanisa, shule, hospitali Magila miaka zaidi ya 100 iliyopita. Idadi kubwa ya wabondei ilikuwa kwenye serikali ya awamu ya kwanza na baada ya uhuru wabondei wengi waliishi Oyserbay, Masaki, Upanga, Chang'ombe, Kurasini.

Matatizo vijana wengi walilemaa na ile hali ya wazazi wao na hawakujiendeleza sana ki elimu na hii ilipelekea baada ya wazazi wao kustaafu vijana hao wakawa wabangaizaji tu mjini. (Ninaongelea DSM through experience).

Wazazi wao wengi walisettle DSM na wengi walihamia Sinza, Mbezi, Magomeni ect. Sifa moja ya wabondei ni waaminifu sana na wengi wao walifanya kazi kwa uadilifu mpaka anastaafu anaacha mpaka kalamu aliyokuwa anaitumia kwa mtu anaekuja nyuma yake.
Nitarudi kwani ninaandika essay sasa hivi.
 
Na wewe akili zako zimekaa kiswahili swahili kama ndo unafikiria hivyo
 
Ile shule ya kwanza ipo Kiwanda si Magila
 
Mtoa mada brazameni si mnaona ye ni ma swagger tu.. Ila hoja yako nimeilewa ni kweli kabisa wanaotoka muheza wengi wameshika nafasi. Wamepitwa na wachaga. Nikipata nafasi nitatembelea muheza
 
Ile shule ya kwanza ipo Kiwanda si Magila

Ya Kiwanda ni nyingine, Magila kulikuwa na St Martin's ya wavulana na St Mary's ya wasichana. Ilikuwa mpaka na middle school yaani darasa la nane. Waliofaulu pale walikwenda either Minaki, Tabora Girls and Boys auTanga School kwa elimu ya secondary. Kiwanda ilikuwa middle school nyingine.
 
Yaani nikiangalia huu mji au hii wilaya ya Muheza kwamba ina watu wengi kidogo walioshika nyadhifa serikalini na kwenye taasisi kubwa za serikali. Ila mimi nimeutembelea huu mji lakini sioni uhalisia kabisa.

Mfano tu huyu mkuu NHC Mchechu nasikia ni wakule, hawa nao wasikia sasa akina Kijazi ni majina ya Muheza halafu hata Mbunge wao wa sasa ni waziri na alishawahi kuwa mpaka Balozi.

Ila sasa pamoja na hayo yote huu mji kila napoutembelea sioni chochote cha maana japo ka mji kamekuwa lakini hakuna swagger za kukuonesha kwamba kuna vigogo wa serikalini wanatoka hapo. Huwezi ona nyumba ya kutisha na mahekalu. Yaani kumekaa ki uswahili uswahili tu. Nyumba za hovyo hovyo. Ukikutana na nzuri basi uzuri wake ni wakawaida kabisa. Mfano tu mimi ni mtu Moshi na juzi nimetoka huko kibosho ila ki ukweli hekalu ambazo zipo kibosho Muheza hata tano hazifiki.

Tatizo haswa ni nini wabondei wa Muheza?? Mmejaliwa vichwa na viongozi wakubwa serikalini na kwenye mashirika na hata wafanyabiashara mnao ila ni kwanini mnakosa akili ya kupendezesha mji wenu???

Kibosho ni salute Mkuu unaweza zani Beverly Hill aisee
 
1: mbondei wa sasa hivi ni MTU wa kuridhika sana hata kama Hana
2: mbondei ni MTU mwenye dharau sana kuna jamaa wa chadema alikuw anagombea ubunge asili yake ni usambaani Na wa ccm alikuw mbondei mwenzao baloz adad Rajab nlichokiona mmi mwenye vituo vya kupigia Kura ni kumsifia mbondei mwenzao Na Bora wakwao tu
3: wabondei wamezoea shida hawataki maendeleo ya haraka muheza asilimia kubwa ya wafanyabiashara wenye mafanikio ni wageni hata ukienda mashambani asilimia kubwa ya wazalishaj wa mazao ni wageni...mbondei yuko radhi Kula ugali Na chumvi nimeona hii Na kushuhudia Kwa macho yang.....huko mtindiro Na kwabata maeneo ambayo yanasifika Kwa kilimo cha machungwa wakulima wake wakuu ni wabena,wangoni,
4: shida ya maji imekuwa tatzo muda mrefu tanga mjini wanatumia maji ya mto zigi ambayo chanzo chake ni muheza....ila miundo mbinu ya maji muheza ni midogo ukienda halmashauri unaonyeshwa mpango mpya wa kupitisha mabomba ya kisasa lakini utekelezaji hakuna ni zaid ya miaka kumi ni wilaya ambayo imebahatika kuwa Na vyanzo vingi vya maji lakini juhudi za kusambaza maji Kwa uhakika hakuna
5: tatizo la umeme
 
Miji ya namna hii,ili iweze kukua na kuonekana vizuri ni vyema mji kupimwa na kuwa na mji wenye makazi yenye mpangilio.
Miji ambayo ipo bila mpangilio inasababisha jamii kuwa na tabia za kishirikina,majungu na fitna hata ushirikina.
Vile vile ipo miji katika Tanzania isiyo kua kwa hadhi hata madhari kwa sababu ya kutokuwa na mpango mji ,na hivyo kuwa na makazi holela na hivyo kuongeza jamii zenye majungu,wivu,roho mbaya dhidi ya familia zenye bidii na mafanikio.
Miji isiyokuwa na maendeleo ,jamii badala ya kujifunza kutoka kwa familia zilizopata mafanikio,wako radhi kukufanyia ushirikina,au kukutengenezea fitna na majungu.
Tanzania sehemu kubwa imeadhirika na mambo niliyoyabainisha katika maelezo yangu,yaani jamii inayojengeka inataka wote mkose,siyo kuiga mafanikio na bidii za wenye uwezo kielimu,kiuchumi na kifedha.
 
Padeshee Mhita ni wa wapi?? Jana nilimwona akimwagia pesa Mzee Mahita kwenye birthday yake.. Alafu dadake ni mbunge wa huko viti maalum na huyo dogo Muhaji anataka kugombea 2020
inawezekana ni wa huko naye.. ila sijui tatizo ni nini hawa watu wameshindwa ku upgrade mji wao hata na nyumba za kisasa.
 
Mimi ni mmbondei wa Muheza. Wabondei ni moja ya makabila ya mwanzo kupata elimu. Waingereza walianzisha kanisa, shule, hospitali Magila miaka zaidi ya 100 iliyopita. Idadi kubwa ya wabondei ilikuwa kwenye serikali ya awamu ya kwanza na baada ya uhuru wabondei wengi waliishi Oyserbay, Masaki, Upanga, Chang'ombe, Kurasini.

Matatizo vijana wengi walilemaa na ile hali ya wazazi wao na hawakujiendeleza sana ki elimu na hii ilipelekea baada ya wazazi wao kustaafu vijana hao wakawa wabangaizaji tu mjini. (Ninaongelea DSM through experience).

Wazazi wao wengi walisettle DSM na wengi walihamia Sinza, Mbezi, Magomeni ect. Sifa moja ya wabondei ni waaminifu sana na wengi wao walifanya kazi kwa uadilifu mpaka anastaafu anaacha mpaka kalamu aliyokuwa anaitumia kwa mtu anaekuja nyuma yake.
Nitarudi kwani ninaandika essay sasa hivi.
Ulichosema na kile nilichokiona kule ni sawa. Inawezekana kabisa tatizo la wabondei wakishatoka kimaisha hawakumbuki kuuendeleza mji wao. Maana hata navoendaga kule naambiwa mbunge anaishi DSM na kule anakujaga kwa ku beep. Hii ni serious problem.
 
1: mbondei wa sasa hivi ni MTU wa kuridhika sana hata kama Hana
2: mbondei ni MTU mwenye dharau sana kuna jamaa wa chadema alikuw anagombea ubunge asili yake ni usambaani Na wa ccm alikuw mbondei mwenzao baloz adad Rajab nlichokiona mmi mwenye vituo vya kupigia Kura ni kumsifia mbondei mwenzao Na Bora wakwao tu
3: wabondei wamezoea shida hawataki maendeleo ya haraka muheza asilimia kubwa ya wafanyabiashara wenye mafanikio ni wageni hata ukienda mashambani asilimia kubwa ya wazalishaj wa mazao ni wageni...mbondei yuko radhi Kula ugali Na chumvi nimeona hii Na kushuhudia Kwa macho yang.....huko mtindiro Na kwabata maeneo ambayo yanasifika Kwa kilimo cha machungwa wakulima wake wakuu ni wabena,wangoni,
4: shida ya maji imekuwa tatzo muda mrefu tanga mjini wanatumia maji ya mto zigi ambayo chanzo chake ni muheza....ila miundo mbinu ya maji muheza ni midogo ukienda halmashauri unaonyeshwa mpango mpya wa kupitisha mabomba ya kisasa lakini utekelezaji hakuna ni zaid ya miaka kumi ni wilaya ambayo imebahatika kuwa Na vyanzo vingi vya maji lakini juhudi za kusambaza maji Kwa uhakika hakuna
5: tatizo la umeme
Unawafahamu vizuri hawa watu.. na mimi nimeobserve kwa mamcho yangu unayoyasema
 
Padeshee Mhita ni wa wapi?? Jana nilimwona akimwagia pesa Mzee Mahita kwenye birthday yake.. Alafu dadake ni mbunge wa huko viti maalum na huyo dogo Muhaji anataka kugombea 2020
Muhaji agombee nini ?? Haha ,nlijua walau kaka yake Kim posible na udiwani wake na sembe sijui kaacha kutumia
 
Muhaji anataka Ubunge 2020... Watauana yeye, Dadake na yule mtoto wa Kigoda
Haha kabisa Muhaji akawashawishi wasambaa sijui wadigo wenzake wampe kura ?? Aisee sioni hilo likitimia ,Huyo wa Kigoda anaweza pita maana mzee wake nadhani anaheshimika hapo sana na kwa upeo wa wengi mtu anapewa kura sio kwa uwezo wake bali kwa kutembelea nyota ya mzazi wake
 
Back
Top Bottom