Mjengwa Blog: Zikiwa zimebaki siku 20

Majjid,

Nilikuwa nakuheshimu kama mchambuzi mahiri sana lakini napata walakini kama si njaa imekubadilisha basi kuna kitu ambacho si kizuri kimetawala moyo wako badala ya uzalendo kwa nchi yako! Ni vyema ukatulia kuandika habari zinazohusu uchaguzi huu na utumie muda wako kuandika habari zisizohusu uchaguzi ili reputation yako ibaki lakini vinginevyo utajishushia hadhi yako sana mbele ya jamii!

Nchi hii vitu viwili vinaanza kututafuna; 1. kupenda kuchumia tumbo 2. udini! tukiachana na hivi tutakuwa wazalendo wa kweli na mengine yatafuata!

Hapo mkuu umepiga msumari pale unapostahili.Mchanganyiko wa njaa na udini ni kichocheo kikubwa cha wanaojikomba kwa mafisadi.
 
watanzania wataishi katika mazingira magumu saaana,dhiki kuu itatawala,migomo isiyoisha,vurugu za hapa na pale,ufisadi utapamba moto
 
Nilimshauri huyu Maggid, anavyoandika vina siku chache sana kusomeka, kama haamini asubiri baada ya October 31 aone...ukiamua kuwa mchambuzi chambua kila kitu.....wakati chama kikiahidi viwanja vitatu vipya vya kimataifa vya ndege huko Kigoma, Kagera, Dodoma huku kikiwa hakijaweza kumaliza kimoja tu ilichokianza miaka mitano iliyopita huko mbeya, Maggid hasemi kuhusu hayo..yeye ameng'ang'ana na "niliyoyasikia Mwembetogwa"....thats purely the mental slave
 
Dingswayo,

Huu ni upotoshaji wa jumla. Sijui ni kwa faida ya nani? Kwenye Mjengwablog inasomeka kama ifuatavyo na si vinginevyo. Mwenye macho apitie akaangalie:


1. Dr Wilbrod Slaa ( CHADEMA) anawania Urais ili kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa kuanzia.Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa CHADEMA na Dr Slaa kama Rais?


2. Rais Jakaya Kikwete anamaliza ngwe yake ya miaka mitano ya urais wa Tanzania. Ameongoza kwa miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya uongozi wa CCM na JK kama Rais?

3. Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF ) anawania Urais ili kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa kuanzia.Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa CUF na Prof. Lipumba kama Rais?

( Kuna wagombea wengine wa Urais, lakini kwa sasa hao watatu ndio wanaonekana kuwa vinara)

This is JF! mkuu, kaza buti be free, kuna walevi humu,mbumbumbu humu, wajinga humu, tuna werevu humu, great thinkers (wa ukweli) humu and wenye busara. Kikubwa ni pale asiye na akili anapojiona anazo ndipo hatari inapoanzia. Hatari kubwa ni pale usipotambua kuwa una deal na watu gani, utaumia kichwa bure, relax pata pepsi ya bariidi, angalia uhuru wako wa kufanya kila kitu usiwe abusive, ukiwa huru ukapotoshwa haina shida mkuu, just ignore them!!!!!
cheers
 
Nakuheshimu sana, lakini sikutegemea kuwa utashuka kiasi hiki!! Unajua wazi kuwa haya uliyaandika na kuyaweka mwenyewe kwenye blog yako. Nilichofanya mimi ni ku copy na kupaste hapa JF. Sababu zilizonifanya niweke hapa JF ni wewe kubania hoja nilizoandika na kuona kuwa hoja ulizoziidhinisha zilikuwa zinainamia upande mmoja, nikaona niweke hapa JF ili kila mtu achangie. Leo nimeangalia kwenye blog yako nikakuta ile post yako imefutwa na zile za zamani bado zikiwepo. Kwa bahati mbaya url yako sio specific kwa kila post, na leo nimeclick imenipeleka kwenye posts general. Tafadhali uwe mkweli, muogope Mungu wako.

Dingswayo,

Acha unafiki. Ungekuwa unaniheshimu usingekimbilia ku-copy na ku-paste. Ungeniandikia kupata ufafanuzi. Usichokijua ni kuwa, mjengwablog ya mwaka 2006 si ya 2010. Hata kama si blog kubwa sana, lakini kila siku kuna kazi nyingi zinaingia na maoni pia.

Mimi nina kibarua kingine mbali ya hiyo mjengwablog. Hivyo basi, nimefundisha vijana wawili wanaojitolea kuhakikisha Mjengwablog iko hai. Ni kwa njia hii pia nao wanakuza vipaji vyao. Wanachofanya ni kuingiza picha na maelezo. Wanahariri pia. Huwa pia wanarudia kuhariri walichoweka mtandaoni. Sasa wewe ndugu yangu unaonekana umekimbilia ku-copy na ku-paste kile ulichotaka kusikia, hata mimi sijakiona. Ni tatizo lako. Sijawahi hata mara moja kusoma positive reply kutoka kwako kuhusiana na mada zangu. Kwa nini sasa ukuleta hapa JF habari kama hiyo yenye kuwahusu Dr Slaa na Prof. Lipumba? Au taarifa ya Mjengwablog inayohimiza vyama na wanasiasa wanaogombea nafasi mbali mbali za uwakilishi katika uchaguzi ujao watume picha na taarifa zao kwenye Mjengwablog . Kwamba Mjengwablog itarusha hewani bila malipo na bila upendeleo. Vyote hivyo viko kule Mjengwablog. Hujachelewa, kama una nia njema.

Ufahamu, kuwa wakati mwingine hata mimi napitia Mjengwablog kama wewe. Vision yangu ni kuwa Mjengwablog ibaki kuwa hai hata kama mimi sitakuwapo duniani. Ni dhana ile ile ya " Mti mmoja mrefu, haufanyi msitu!". Dingswayo, nakukaribisha tushirikiane ndugu yangu, naamini wewe ni mtu mwema.
 
Sawa mimi ni mnafiki kwa kutokulalamikia. Huo ni mtazamo wako na sitajaribu kuubadili. Lakini ukweli ni kuwa kitendo chako cha kuweka maoni uliyoyapenda wewe kwenye internet, kilinifanya mimi ni copy na kupaste na kupeleaka JF ambamo humo jambo hilo lingejadiliwa bila idhini ya mwenye blog.

Ni vizuri kuwa sasa uankiri kuwa nili copy na kupaste na vilevile nikaweka pia na source nilipotoa. Kwa hiyo ukweli upo pale pale kwamba uliiandika hiyo mwenyewe na sio mimi niliyotunga tofauti na ulivyosema kuwa wewe hukuandika hayo.
 
Sawa mimi ni mnafiki kwa kutokulalamikia. Huo ni mtazamo wako na sitajaribu kuubadili. Lakini ukweli ni kuwa kitendo chako cha kuweka maoni uliyoyapenda wewe kwenye internet, kilinifanya mimi ni copy na kupaste na kupeleaka JF ambamo humo jambo hilo lingejadiliwa bila idhini ya mwenye blog.

Ni vizuri kuwa sasa uankiri kuwa nili copy na kupaste na vilevile nikaweka pia na source nilipotoa. Kwa hiyo ukweli upo pale pale kwamba uliiandika hiyo mwenyewe na sio mimi niliyotunga tofauti na ulivyosema kuwa wewe hukuandika hayo.

Dingswayo,

Baada ya kutuma nilichoandika nikarudi kusoma tena. Nasikitika nimekuita mnafiki, nilikasirika pale niliposoma kuwa unasema unaniheshimu na wakati huo hukuwasiliana nami kuomba ufafanuzi wa malalamiko yako. Uniwie radhi. Una haki ya kulalamika. Lakini nasisitiza kuwa kitu ulichokiona sikukiona pale Mjengwablog, yawezekana ni kwa sababu nilizozieleza. Naomba uniamini.

Nakukaribisha tena uje na maoni, ushauri na mengineyo kuhusu Mjengwablog. Tushirikiane.
 
..Kwa hiyo Maggid unachosema ni kwamba kila kinachotoka kwenye Blog yako sio lazima kiwe kama unavyotaka kitokee bali kuna vijana wako wawili wa kazi ambao wakati mwingine wanaweza wakakosea kupost kitu ambavyo usingependa kitokee na kwa maana hivyo ili tusiwe wanafiki na kuonekana kuwa hatukuheshimu inatubidi kwanza tukuandikie barua kutaka ufafanuzi wa jambo tunaloona kwenye blog yako kabla ya kuli-copy na kuli-paste huku JF?? Kwamba tusipofanya hivyo inakuwa ni kutokukuheshimu???? well!...... :thinking:
 
Matarajio yangu baada ya kuchaguliwa Kikwete tena ni



  1. [*]utekelezaji wa visasi kwa waliokuwa mstari wa mbele kumpinga ktk kampeni zake,
  2. kuwa familia itashika hatamu baada ya juhudi binafsi za kumpigia kampeni arejee tena,
  3. mvua kutonyesha kwa kipindi kirefu baada ya kujichagulia dhahama jingine la miaka mitano ya kukumbatia ufisadi na wizi wa mali za umma.
  4. Heshima ya serikali kushuka baada ya ikulu kuridhia matumizi ya ramli kwenye uendeshaji wake.
Sina mengi sana ya kutarajia maana ahadi na ilani ya CCM hazina mashiko
Wahanga wa kwanza watakuwa baadhi ya JF Members, na JF huenda ikafungwa!
 
kaka yangu unahangaika bure na hawa mavuvuzela, Maggid ni hopeless case, keshalamba mavi hawezi kuwa kamili mwache samaki mmoja akioza mtupe asijekuchafua wengine maana hakuna wa kuoza humu JF. Muhimu mshauri aende kule kwa michuzi huku sio daraja lake. Hatununuliki huku na vipaja vya kuku vya CCM. mwache akavile yeye na mkewe na watoto wake wanenepe watoto wetu wakonde leo lakini wabaki na heshima yao.
 
Kumbe blog zinalipa sana wakati wa uchaguzi....Kwai kuna wanablog wengi ambao tunawajua siku nyingi kuwa ni wapiga debe na makuadi wa CCM, na kuna wengine kama Mjegwa ambaye nilidhani ni mzalendo wa kweli, kumbe nilikua so wrong. Sasa ndugu yetu hebu tuambie kimetokea nini au ndio yale yale ya CCM ya kudakishana. Mimi sasa naanza kukuona kuwa na wewe ndio wale wale wanaoshibishwa kuugeuka uzalendo wao.
 
Je akiwa DC wakuulinda MAFISADI atapata nini kuona watoto wa masikini wakipatashida wakati wakina Nnauye wakifurahi? Ole wenu mlae na wachawi na wezi wa uchumi na elimu na maendeleo ya wa TZ, mungu atawahukumu mpaka mkijua huku duniani mahesabu kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom