Mjengwa Blog: Zikiwa zimebaki siku 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwa Blog: Zikiwa zimebaki siku 20

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Oct 10, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  .....Rais Kikwete anamaliza ngwe yake ya miaka mitano ya urais wa Tanzania. Ametawala kwa miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).Ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho. Mdau, nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ijayo endapo JK atachaguliwa tena ....?

  mjengwa
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  1. dhiki kuu itakuja nchini endapo akiongoza huyu bwana aka VASCO DA GAMA
  2. Wasomi wengi watakimbia nchi kwenda ughaibuni coz life litakuwa tight sana na kutatokea mfumuko mkubwa wa bei na fedha yetu ya madafu itashuka thamani mno.
  3. Kwakuwa huyu bwana ni mzee wa ''ahadi'' nadhani atafanya safari maradufu za nje ili aghalau a'fulfill' promc zake, so tutegemee absence yake kwa miaka 4 kabla hajaja kuaga.
  4. Umaskini mkubwa kwani atajinyakulia chake mapema na kuwekeza nyumba za kifahari nje ya nchi.( CCM-CHUKUA CHAKO MAPEMA)
  5. Ndio utakuwa mwisho wa CCM, kwani hawana mgombea mwingine after next five yrs ATAKAYEWEZA KUSIMAMA NA DK. SLAA.
  6. Matukio mengi tusioyaona huenda yakawa yanajitokeza kwakuwa VISCO DA GAMA anaongoza asipopendwa.
  7. Ongzea mwenyewe........
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Too bad that all the people who really know how to run the country are busy driving taxi cabs and cutting hair.
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mjengwa hshma yako yashukaaa...
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Dingswayo,

  Huu ni upotoshaji wa jumla. Sijui ni kwa faida ya nani? Kwenye Mjengwablog inasomeka kama ifuatavyo na si vinginevyo. Mwenye macho apitie akaangalie:
  [FONT=&quot]
  [/FONT]

  [FONT=&quot]1. Dr Wilbrod Slaa ( CHADEMA) anawania Urais ili kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa kuanzia.Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa CHADEMA na Dr Slaa kama Rais?[/FONT]


  [FONT=&quot]2. Rais Jakaya Kikwete anamaliza ngwe yake ya miaka mitano ya urais wa Tanzania. Ameongoza kwa miaka mitano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya uongozi wa CCM na JK kama Rais?[/FONT]

  3. Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF ) anawania Urais ili kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa kuanzia.Je, ni nini matarajio yako kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa CUF na Prof. Lipumba kama Rais?

  ( Kuna wagombea wengine wa Urais, lakini kwa sasa hao watatu ndio wanaonekana kuwa vinara)
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  :A S 13: Mjengwa na uandishi wa majiTAKA, anakubali kuwepa kabobo kuwaramba visigino mafisadi
   
 7. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Majjid,

  Nilikuwa nakuheshimu kama mchambuzi mahiri sana lakini napata walakini kama si njaa imekubadilisha basi kuna kitu ambacho si kizuri kimetawala moyo wako badala ya uzalendo kwa nchi yako! Ni vyema ukatulia kuandika habari zinazohusu uchaguzi huu na utumie muda wako kuandika habari zisizohusu uchaguzi ili reputation yako ibaki lakini vinginevyo utajishushia hadhi yako sana mbele ya jamii!

  Nchi hii vitu viwili vinaanza kututafuna; 1. kupenda kuchumia tumbo 2. udini! tukiachana na hivi tutakuwa wazalendo wa kweli na mengine yatafuata!
   
 8. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  JK akishinda Mjengwa utakuwa DC
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Majjid????:A S 112::A S 112::A S 112:
   
 10. m

  maggid Verified User

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hata nikipewa dhamana ya U-RC nitasema; " Mheshimiwa, Asante sana, lakini HAPANA kwa sasa". Ndio, nina mke, na watoto wanaonihitaji zaidi katika makuzi yao. Kibarua ninachokifanya sasa na kipato changu, japo kidogo, kinaniwezesha kujikimu. Mimi ni mjamaa, na kamwe sijawahi kuupenda ubepari. Tatizo letu Watanzania ni hulka yetu ya kuangalia ' vyeo' na vyote vyenye kuambatana na vyeo hivyo, kama vile gari la fahari, safari za ndani na nje na posho. Badala ya kuangalia zaidi dhamana inayoendana na vyeo hivyo.

  Ni ujinga pia, kudhani kila mtu anayefikiri tofauti , basi, ni fisadi au kanunuliwa na mafisadi.
   
 11. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Mkuu nifafanulie pale kwenye glob!!
   
 12. E

  Edu Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee this is the paining truth I have ever read in JF.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  matarajio yangu ni kuwa vurugu nchi nzima.

  Migomo na zomeazomea kumkabili JK kila aendapo kwa sababu watu wataamini ameiba kura na wala siyo vinginevyo

  Atakuwa Raisi wa kwanza katika historia ya nchi yetu kufukuzwa kazi na Bunge kwa kuvunja katiba kwa kutoheshimu maagizo ya bunge serikalini na upinzani utaandaa hoja ya kumfuta kazi na wabunge wa CCM nao wataichangamkia vilivyo.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Turejee historia kidogo.

  Mwinyi alianza vizuri sana 1985 na 1986 tukamkabidhi lile 'fagio la chuma'. Baada ya kupata awamu ya pili akaliweka fagio la chuma uvunguni na akawa anajichumia kwa kujiandaa na kustaafu.

  Mkapa, alianza vizuri sana sana 1995. Baada ya kumchagua tena 2005 ndipo akaanza zile biashara chafu za Kiwira na mkewe kufungua biashara pale Ikulu.

  Sasa huyu Rais wetu JK hakuwa na jipya zaidi ya kauli tu na kujivinjari kwa Semina elekezi na safari za mara kwa mara. Tukimchagua tena itakuwaje? Hali itakuwa mabaya mara duifu.
   
 15. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nakuheshimu sana, lakini sikutegemea kuwa utashuka kiasi hiki!! Unajua wazi kuwa haya uliyaandika na kuyaweka mwenyewe kwenye blog yako. Nilichofanya mimi ni ku copy na kupaste hapa JF.

  Sababu zilizonifanya niweke hapa JF ni wewe kubania hoja nilizoandika na kuona kuwa hoja ulizoziidhinisha zilikuwa zinainamia upande mmoja, nikaona niweke hapa JF ili kila mtu achangie. Leo nimeangalia kwenye blog yako nikakuta ile post yako imefutwa na zile za zamani bado zikiwepo.

  Kwa bahati mbaya url yako sio specific kwa kila post, na leo nimeclick imenipeleka kwenye posts general. Tafadhali uwe mkweli, muogope Mungu wako.
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Matarajio yangu baada ya kuchaguliwa Kikwete tena ni

  1. utekelezaji wa visasi kwa waliokuwa mstari wa mbele kumpinga ktk kampeni zake,
  2. kuwa familia itashika hatamu baada ya juhudi binafsi za kumpigia kampeni arejee tena,
  3. mvua kutonyesha kwa kipindi kirefu baada ya kujichagulia dhahama jingine la miaka mitano ya kukumbatia ufisadi na wizi wa mali za umma.
  4. Heshima ya serikali kushuka baada ya ikulu kuridhia matumizi ya ramli kwenye uendeshaji wake.
  Sina mengi sana ya kutarajia maana ahadi na ilani ya CCM hazina mashiko
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  JK akishinda matarajio yangu ni kama ifuatavyo:
  1)Vitendo vya ufisadi vitaongezeka;
  2)Umaskini wa mwananchi wa kawaida utaongezeka;
  3)Heshima ya serikali mbele ya wananchi na jumuiya za kimataifa itapungua sana;
  4)Ridhiwani Kikwete na Miraji kikwete viburi na dharau zao zitaongezeka;
  5)Lowasa atakuwa waziri mkuu;
  6)Kinana atakuwa spika wa bunge;
  7)Vyombo vya habari vilivyokuwa vinandika vibaya habari zake vitafungiwa;
  8)Dr Benson Bana wa Chuo kikuu cha Dar es salaam atalipwa fadhira kama alivyolipwa Prof Mkandala;
  9)Utajiri wa Rostam Azizi uataongezeka kwa kasi ya ajabu;
  10)Abrahaman Shimbo atapandishwa cheo;
  11)Mfumuko wa bei utaongezeka;
  12)Thamani ya shillingi ya Tanzania itazidi kushuka.
   
 18. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tutakoma. Kama miaka Mitano hii yeye na familia yake walikuwa hivi, Je miaka mitano ya lala salama atakuwaje, hasa ukiangalia mfano aliochangia muungwana mmoja hapo juu kuhusu Mzee Ruxa na Mzee wa Ukweli na Uwa-ziii!
   
 19. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maggid ni kweli kuwa ni ujinga kudhania pia kwamba mtu anayefikiria tofauti ni fisadi. Lakini pia ni ujinga kuelezea ubaya wa mgombea mmoja tu na kusema kuwa unafikiri tofauti. Ungekuwa kwa mfano unawachambua wote halafu unasema kuwa kutokana na mizani ya uchambuzi wako unaona fulani anafaa, hapo tungesema unafikiria tofauti. Wewe hufikirii tofauti, bali unapigia debe mtu tofauti na wengi wanayemtaka kwa ajili ya mabadiliko. Kwa hiyo unashambuliwa kwa sababu wewe unataka kudumisha status quo. Na kwa sababu kwa miaka kadhaa ulijipambanua kama mchambuzi mzuri, watu wanajiuliza kulikoni?

  Nini kimekutokea hadi ukawa mpiga debe wa CCM?
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mzee kwa kuwa-unmask sikuwezi.
  Nashukuru kwamba umemfahamu ndugu yetu huyu kwamba ni mnunuliwaji na waliomtuma kwenye kipindi hiki cha lala salama. Naamini bado anawasiliana na Muhingo mzee wa mipango shantashanta.
   
Loading...