Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,582
Jambo la kwanza kumbuka kwamba hakuna mtu anayejali mambo / maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe! Na kila mtu ana muda sawa na mwingine, kwa siku kila mtu amepewa masaa 24 tu. Anza kwa kuzingatia mda, ugawe muda wako katika makundi kwa utashi wako ukizingatia kuwa kila utakachojipangia unakifanya ndani ya muda ulioupanga.
MUDA NI MALI, JALI MUDA WAKATI NA MAHALI
Kwa lolote unalotaka kulifanya lipangie unalifanya lini, mda gani na sehemu ipi.
Mfano!
Siku inaanza saa sita za usiku
– Anza kwa maombi! Haya inabidi yawe maombi ya mda mrefu; maombi unayopaswa kuomba hapa ni kuziweka haja zako mbele ya Bwana.
Alfajiri – Kagua makazi yako ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya mwili
Asubuhi – Tafakari mambo unayopaswa kuyafanya kwa siku hiyo na tanguliza maombi kabla ya kuyafanya.
Mchana – Maombi mafupi (Kumbuka huu ni muda wa chakula cha mchana)
Alasiri – Tafakari kazi ulizozifanya kwa siku hiyo
Jioni – Ongea na marafiki / familia n.k
Usiku – Sala fupi na kupumzika.
TUENDELEE KUSHAULIANA MEMA ZAIDI ILI TUFIKE SALAMA KULE TUNAKOELEKEA.