KERO Changamoto za Umeme Newala

KERO Changamoto za Umeme Newala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Newala -Mtwara, kila Mara Tumekuwa na changamoto ya kukatika umeme , tunashindwa kufanya kazi zetu zinazotumia umeme; mda mwingine siku mbili mfululizo bila kupewa taarifa yoyote, kwa Leo pia Toka jana usiku Kucha na Leo mchana kutwa hakuna umeme, tunatamani kujua tatizo ni nini?
 
Habari, Ndugu Mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.

Pole sana kwa changamoto uliyoipata, pamoja na kuchelewa kurudia.

Tafadhali fahamu kuwa mara tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au hitilafu za ghafla, huwa tunatoa taarifa mapema pamoja na maelezo ya sababu ya usitishaji wa huduma.

Taarifa hizi hutolewa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ujumbe mfupi wa SMS (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na maeneo.

Iwapo hujapata taarifa hizi, tunaomba radhi. Tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp kupitia inbox pamoja na mkoa unaoishi, na tutahakikisha tunakuunganisha kwenye makundi husika ili upate taarifa zote muhimu kuhusu huduma ya umeme katika eneo lako. ^CM
 
Mimi ni mkazi wa Newala -Mtwara, kila Mara Tumekuwa na changamoto ya kukatika umeme , tunashindwa kufanya kazi zetu zinazotumia umeme; mda mwingine siku mbili mfululizo bila kupewa taarifa yoyote, kwa Leo pia Toka jana usiku Kucha na Leo mchana kutwa hakuna umeme, tunatamani kujua tatizo ni nini?
Watendaji wapo bize kupambana na magaidi (upinzani). Hawajishughulishi na shida zetu
 
sio Newala pekeyake, mikoa ya Lindi na Mtwara umeme unasumbua sana kwa takribani miaka kumi sasa. ni nadra siku ikaisha bila umeme kukatika. Gesi inayozalisha umeme inatoka Lindi na Mtwara lakini umeme wa shida. Viongozi wapo tu na hakuna anayejali. Mwaka 2012 vurugu kubwa ya "gesi ya Mtwara" ilitokea kupinga dhulma kama hizi lakini watu waliishia kuuawa na kufungwa jela tu. Watu wamekata tamaa, wametulia tuu
 
Habari ndugu mteja,

Asante sana kwa mrejesho wako.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Aidha, tunaomba utupatie muda kidogo ili tuweze kufanya ufuatiliaji na ofisi ya mkoa husika kwa ajili ya kupata mwongozo stahiki kuhusu suala hili.

Tunathamini uvumilivu na ushirikiano wako. Asante sana. ^HN
 
Back
Top Bottom