Nimeupenda sana mjadala wa leo lakini nadhani ningeupenda zaidi kama kanuni ya audi alteram partem"hear the other side" ingefuata. Kwangu mimi naona mjadala huu umekuwa ni wa upande mmoja sana na hivyo unatufanya tushindwe ku-balance hoja mbili zinazovutana. Hii inaonesha wazi inawezekana mjadala huu umeandaliwa na watu fulani kwa ajili ya kuwakandamiza watu fulani. Kiutaalamu, katika mada kama hizi ni vema sauti za pande mbili zingesikika.
Tujadili uhalali wa mjadala wa upande mmoja

mmh, hivi kwani mkuu ukiambiwa 1+1=2, ni lazima upate na hoja ya upande wa pili ili kujua kama hesabu ni sahihi?
NIngependa kama ungechangia kwenye mjadala wenyewe sio kujaza upupu na kujaza server
Miss Judith!! katika sheria haki ya asili"natural justice" ni kitu muhimu sana na ukitoa hukumu bila kuzingatia haki ya asili ya kusikiliza pande zote basi uamuzi wako utakuwa batili na utatupwa tu. Na ndio maana hata mtu akikamatwa ndani ya nyumba ya mtu akiiba, mahakama haiwezi kumfunga mpaka isikilize utetezi wake.
Kilichotokea leo ITV swali la kipima joto lilikuwa JE SABABU ZA KUILIPA DOWANS NI ZA MSINGI?? Binafsi nimeshindwa kutoa jibu japo kimoyo moyo kwa kuwa sijausikia utetezi wa upande wa pili
mjadala wa television si mahakama, ila kla kitu kwenye mjadala is judged on its own merit. nijuavyo mimi pamoja na haki ya kusikilizwa, kuna wakati mahakama huwa inasikiliza upande mmoja na katika hali kama hiyo nakuna guarantee kuwa anayesikilizwa atashinda.mfano licha ya kusikilizwa peke yake akisema kwa mfano 1+1=3 mbele ya jaji wa hakihawezi kushinda na kama ni jela atenda!
unadhani RA au EL au NK wangeitwa aje hapo wangeweza kuja?
Kaumza, kwa upandee wangu ule haukuwaa mjadala ingawa uliitwa mjadala, kilichokuwa kinajadiliwa ni nini? Ni kuwa Dowans ilipwe au isilipwe? sasa wale wote waliokaa pale wanasema isilipwe, kuna mjadaala hapo? In my view, sio mjadala.
Swali la kipima joto lilitutaka sisi watazamaji tuamue kama sababu za kuilipa Dowans ni za msingi au la! Niambie Miss Judith, ungeweza vipi kutoa uamuzi bila kuusikiliza upande wa pili? Kma wewe ni mwanasheria nadhani unafahamu kuwa katk kutoa uamuzi huwa tunapima hoja zinazowasilishwa na wahusika wa pande zinazovutana na wala huwa hatuangalii tukio. Ndo maana mtu anaweza kubaka kabisa na umati wa watu ukashuhudia lakini mbele ya hakimu akatoka kidedea kwa kuwa tu ametoa hoja nzito kuliko upande wa mashtaka.
Labda unielekeze maana hakuna ajuae kila kitu. Ni mazingira gani natural justice haipewi uzito? Naomba unipe na authorities
Nimeupenda sana mjadala wa leo lakini nadhani ningeupenda zaidi kama kanuni ya audi alteram partem"hear the other side" ingefuata. Kwangu mimi naona mjadala huu umekuwa ni wa upande mmoja sana na hivyo unatufanya tushindwe ku-balance hoja mbili zinazovutana
Ulijaa ushabiki. Hata hivyo Rugemereza alikuwa mwangalifu sana katika ku draw conclusions. Tunataka hao ambao 'hawakutendewa haki wajibu mapigo" nao.
upande wa pili unaotaka ni upi?matamko ya serikali yako wazi na hukumu ya icc walikuwanayo,wamejadili hayo matamko kama yako right or not.usilete porojo na spin za ajabu ajabu,wasaliti kama nyinyi na wamiliki wa dowans mnastahili adhabu ya kunyongwa mpaka mfe.
Kaumza, kwa upandee wangu ule haukuwaa mjadala ingawa uliitwa mjadala, kilichokuwa kinajadiliwa ni nini? Ni kuwa Dowans ilipwe au isilipwe? sasa wale wote waliokaa pale wanasema isilipwe, kuna mjadaala hapo? In my view, sio mjadala.
mmh, hivi kwani mkuu ukiambiwa 1+1=2, ni lazima upate na hoja ya upande wa pili ili kujua kama hesabu ni sahihi?
Nddo maana nikasema tujadili facts in issue na si facts tu. Kamati ya Bunge liliilazimisha serikali ivunje mkataba na pia isinunue mitambo ya Dowans. Wanaoona mbali pamoja na Zitto Kabwe wakasisitiza ni bora serikali iinunue mitambo hiyo. Na kwa kuwa serikali ilikuwa imeingia uaoga hasa kutokana na minyukano ndani ya Bunge na Mwakyembe ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati kuitisha serikali kuwa "tutakutana bungeni", ikaamua kutoinunua mitambo hiyo. Leo tunailazimisha serikali isilipe hizo sh 94bl, na tukuchelewa kulipa ndani ya siku chache zijazo tutalipa sh 94bl+7.5%. Tulishafanya kosa kwa kukubali vipengele vigumu na vinavyotubana ktk mkataba. Ushauri wangu ni kuwa tulipe baada ya hapo tuwe makini ktk kuingia mikataba hasa inayohusu biashara za kimataifa. Kwa sasa hata tukimjua mchawi ni nani haitasaidia. Tuweke siasa pembeni, tudili na sheria