TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Kwa mtindo huu nzega itakuja kuwa mji mzuri sana badae sababu uwepo wa maji ya uhakika na umeme vitachochea sana maendeleo ukizingatia nzega ipo njia panda ya shinyanga mwanza bukoba kigoma kwaiyo wale wakimbia nyumbani tunaweza kuja jificha Nzega
 
Bwana Joseph sanga umetufanyia kitu kibaya sana wana nzega tulikuamini tulikutegemea katika utendaji wako wa kazi katika kutuletea tarifa mbali mbali hapa JF ajabu napata tarifa kuwa umewaacha wana nzega katika sitofahamu kwani umejitoa katika kundi lenu la whatsapp kimya kimya na wakikuona wakikuhoji uwapi majibu zaidi unasema simu ulibiwa hivi kweli jamii forum hawawezi kukupa simu nyingine


Tunaomba jamii forum mpatieni bwana sanga simu nyingine ili aweze tuwakilisha wana nzega maana miezi miwili sasa hatuoni tarifa yoyote kuhusu nzega yetu

Joseph sanga nimepata sifa zake ana msimamo akubali tumika ovyo ovyo ina maana tarifa anazotupa hapa hazina utata wowote
Mfano sasa tunataka kujua ujenzi wa stedi mpya kwanini umesimama kwanini mkurugenzi wa nzega anabana sana wafanya biashara kuna mambo mengi tunaitaji kujua joseph sanga popote ulipo tunakuitaji hapa tarifa zako za kujitoa katika kundi la whatsapp bila tarifa yoyote imetustuwa wana nzega je umenunuliwa ila inakuwaje ununuliwe sasa maana tumepata sifa zako kuwa una misimamo huogopi mtu joseph sanga njoo bwana utujibu hapa
 
Natumai katibu wa mbunge naye anayaona, kama Sanga anapata changamoto basi katibu wa mbunge awe back up, atujuze maendeleo ya huko. kunamichango ya maana sana humu na ninawasiwasi mtaikosa kama hali hii itadumu. Hatahivyo naamini ni sula la muda tu timu itakuwa vzr.
 
Uongozi wa Jamii forum tuambieni Joseph Sanga yupo wapi mambo mengi jimboni yakimaendeleo jimboni yanaendelea tuliambiwa shule ya Bulunde itanza kazi mwezi wa saba sasa kuna tetesi haianzi kazi mwezi wa saba Je ni kweli kitu kingine stand mpya mpaka leo hatujui kitu kinacho endelea zabuni zipo kimya ,kuna tatizo la wafanya biashara na TRA sanga popote ulipo njoo hapa
 
Uongozi wa Jamii forum tuambieni Joseph Sanga yupo wapi mambo mengi jimboni yakimaendeleo jimboni yanaendelea tuliambiwa shule ya Bulunde itanza kazi mwezi wa saba sasa kuna tetesi haianzi kazi mwezi wa saba Je ni kweli kitu kingine stand mpya mpaka leo hatujui kitu kinacho endelea zabuni zipo kimya ,kuna tatizo la wafanya biashara na TRA sanga popote ulipo njoo hapa
Nipo mdau ni shuguli za kiutendaji tu zilingiliana
 
IMG_20170610_180650.jpg
IMG_20170610_154054.jpg
Mdau uliyeulizia kuhusu kuanza kwa kidato cha tano katika shule ya sekondari Bulunde Mwaka huu

Hizo ni picha za ujenzi wa miundombinu wa mabweni na madarasa unaoendelea hivi sasa ujenzi huo ulianza mwezi wa nne mwaka huu 2017 kwa pesa zilitoka serikalini.

Kabla ya ujenzi huu tayali kulikuwa na madarasa mawili ambayo yanekamilika pamoja na bweni moja ambalo ujenzi wake ujakamilika lilojengwa na mbunge kupitia pesa zake binafsi na za mfuko wa jimbo

mpaka sasa ujenzi unaendelea kwaiyo swali lako je shule itaanza kufanya kazi mwaka huu jibu bado kwani uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano uliotangazwa juzi shule ya Bulunde haijapangiwa wanafunzi

Hivyo tuendelee subilia maana siku bado
 
Tumefurahi umerudi bwana sanga ,miye na swali tena kwako kituo cha mabasi vipi mbona washindi wa zabuni za ujenzi mpaka sasa hawajatangazwa wakati watu waliochukuliwa viwanja vyao tunambiwa tayali washalipwa fidia zao jambo gani linakwamisha kutangazwa washindi wa zabuni tuambieni tujue
 
Ndugu yangu sagara sagara mkurugenzi naye ni tatizo hapo nzega inabidi wana nzega tushikane hakuna sababu mpaka leo stedi isianze kazi sanga umerudi tusaidie tatizo nini
 
. Diwani wa nzega mashariki Mh Ruangisa akiwa na wana kamati wa maendeleo ya kata nzega mashariki akiwaonyesha maendeleo ya mradi wa ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Bulunde yaliyofanyika mwaka wa fedha 2016/2017 katika kata yake ya nzega mashariki.



Mh Diwani Ruangisa akisoma tarifa ya maendeleo ya mwaka 2016/2017 kwa wana kamati wa maendeleo wa kata yake nzega mashariki, na wanainchi wa kata yake



Mh Diwani akiongelea maendeleo ya miundombinu katika kata yake ya nzega mashariki

Mh Diwani akiongelea maendeleo ya miundombinu ya barabara katika kata yake

Mh Diwani akiongelea maendeleo ya elimu katika kata yake
M Diwani akizidi kifafanua maendeleo ya elimu katika kata yake

Mh Diwani Ruangisa akielezea maendeleo ya utatuzi wa migogoro ya aridhi katika kata yake

Mh Diwani akiongelea suala la kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya ufundi , na maendeleo ya afya katika kata yake
 
Sanga tupandishie na tarifa za maendeleo ya kata ya nzega magharibi kwa mwaka 2016/2017 tuone upinzani wamefany nini uko
 
Juzi katika star tv habari nimeona diwani hapo akilalamikia kuhusu uyo mkandarasi aliyopewa hiyo kazi ya mabara Swali mkurugenzi wa nzega haoni hayo madudu pia nimepata habari kuna mvutano kuna pesa zimekuja za ujenzi wa shule ya wasichana mkurugenzi anataka fanya ujenzi usimamiwe na halmashauri, mbunge naye nasikia anataka ujenzi ausimamie yeye mbunge yani halmashauri ina vituko hii
 
IMG-20170730-WA0007.jpg
Meneja wa idara ya Maji Nzega, Wa kwanza kushoto akifuatiwa na katiku wa mbunge Jimbo la Nzega mjini bwana majaliwa, wakitoa ufafanuzi kwa timu ya Jamii Forum jinsi gani wameweza kutekeleza mradi wa Tushirikishane katika jimbo la Nzega katika upande wa maji, timu ya Jamii Forum ilitembelea jimboni Nzega kuangalia utekelezwaji wa ahadi za mradi ikiongozwa na dada Asha.
 
Back
Top Bottom