TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Aug 9, 2016
13
67
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Nzega mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Hussein Bashe

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Nzega mjini.

Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Nzega mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE ni:

a. Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

b. Ujenzi wa Nyumba ya Daktari-Kituo cha Afya Nhobora

c. Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

d. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde​

Tushirikishane Nzega.jpg

Picha ya pamoja na washiriki toka Nzega. Waliokuwa wamekaa ni madiwani
Mada hii itatumika zaidi na Wana Nzega kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:

1. Mh. Mbunge Hussein Bashe
2. Majaliwa Bilali (Katibu wa Mbunge)
3. Josephat Sanga (Afisa habari Nzega)
4. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Nzega mjini.​

Karibuni...

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Nzega[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

=======
Akaunti za mradi wa Tushirikishane katika mitandao ya Kijamii:

Tushirikishane (@tushirikishane) • Instagram photos and videos

Tushirikishane | Facebook

Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter
 
kiongozi mji wa nzega mwaka Jana uligawanywa kutoka halmashauri ya wilaya na kuwa halmashauri ya wilaya ya nzega na kuwepo na halmashauri ya mji nzega

kwaiyo halmashauri ya wilaya ya nzega ilikuwa na high school mbili moja ni shule binafsi ipo chini ya kanisa la roma katoriki ambayo ni shule ya UCHAMA

nyingine ni KILI SEKONDARI ambayo ipo Bukene hii KILI SEKONDARI ni Mali ya serikali hivyo basi kutokana na mgawanyo wa hizi halmashauri shule ya high school ya KILI ikajikuta ipo katika halmashauri ya wilaya ya nzega siyo halmashauri ya mji nzega

hivyo basi halmashauri ya mji nzega ikajikuta haina shule ya high school ambayo si ya serikali ikabaki shule ya high school ya binafsi ambayo ni shule ya UCHAMA

Kwaiyo huu mradi wa TUSHIRIKIANE upo katika jimbo la nzega mjini ambapo Mbunge wake ni Husen Bashe hii ni halmashauri mpya kabisa tangu ianze kazi hivyo hiyo mipango kazi minne hapo juu ipo katika jimbo la nzega mjini.


Bado tatizo la kutokuwepo high school ni kuubwa sana
iwepo moja au mbili bado haitoshi
 
IMG-20160825-WA0009.jpg
IMG-20160825-WA0007.jpg
IMG-20160825-WA0012.jpg
IMG-20160825-WA0011.jpg
IMG-20160825-WA0011.jpg
IMG-20160825-WA0004.jpg
Mu
IMG-20160825-WA0004.jpg
IMG_20160814_080537.jpg


Muonekano tofauti tofauti wa kituo kipya cha mabasi Nzega kinachoendelea na ujenzi, jengo la kituo cha polisi na vyoo tayari vimekamilika, banda la kupumzikia wageni wakiwa wanasubiria magari linaendelea na ujenzi kama tunavyoona katika picha, ikiwa ni mwezi wa kwanza kuanza kwa mradi wa TUSHIRIKIANE NZEGA.
 
Huu ni mwanzo Mzuri tuwapongeze JamiiForums na Wananzega. Mpango wa elimu ya secondari ni Mzuri na waanze kufikiria kujenga Public library (maktaba) kwani itasaidia kuinua kiwango cha ufaulu
 
Kutangulia siyo kufika ndugu yangu Malafyale huu ni mwanzo Mzuri tuwapongeze. Pia pamoja na suala la elimu juhudi zifanyike kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja kwa kwanzisha programmu za fursa ili wananchi wawe na uwezo wa kuwasomesha hao watoto kwa mahitaji mbalimbali. Fursa km vile ufugaji bora wa kuku.nyuki vikundi vya ujasiliamali etc
 
Waongeze bidii kwa kweli
Why wana Nzega wenye mahela yao hapa Dar wasikutane kujenga yao?
Kyela sisi tulikuwa tunakutana kufuatia kata mnazo toka
Sasa tunazo high school 10
Bado hazitoshi na tunaendelea kujenga

Watu wanasubiri serikali Kwa kila kitu.Tunabadilika kidogo Lakini.
Hongereni sanaaaa tu wana Kyela. maana Watu wengi tukisikia wengi tutafata mkumbo Kwa mazuri
 
IMG_20160901_120307.jpg
IMG_20160901_120307.jpg
(2).jpg
(1).jpg
(3).jpg
picha ni madarasa mawili ya kidato cha tano na cha sita ambayo yamekamilika, pia jengo ambalo ni bweni la wanafunzi ambalo lipo katika ujenzi unaoendelea katika shule ya sekondari
Bulunde

Kitu kingine wadau tukumbushane mradi huu upo katika halmashauri ya mji nzega halmashauri ambayo ni mpya kwaiyo ndio inaanza jiimalisha

Kipindi nzega haijagawanywa ni halmashauri moja ya wilaya zilikuwepo shule za kidato cha tano na cha sita shule mbili

Shule ya sekondari UCHAMA ambayo si ya serikali na shule ya sekondari KILI iliyopo Bukene hii ni shule ya serikali

Hivyo basi baada ya wilaya ya nzega kugawanywa kuwa na halmashauri mbili ambayo ni halmashauri ya mji nzega ambayo ndio jimbo la nzega mjini Mbunge wake Husen bashe na kuwepo kwa halmashauri ya wilaya ya nzega ambayo ni jimbo la nzega vijijini Mbunge wake Mh Dr Kigwangala

Basi jimbo la nzega mjini likajikuta halina shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma kwani KILI SEKONDARI ilibakia katika jimbo la nzega vijijini ambayo ni halmashauri ya wilaya ya nzega

Shule iliyopo ya kidato cha tano na sita kwa sasa katika halmashauri ya mji nzega ni ya UCHAMA ambayo si Mali ya umma (serikali)

Hivyo basi huu ujenzi wa sasa nihatua ya kuhakikisha mji wa nzega unakuwa na shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma (serikali)
 
Watu wanasubiri serikali Kwa kila kitu.Tunabadilika kidogo Lakini.
Hongereni sanaaaa tu wana Kyela. maana Watu wengi tukisikia wengi tutafata mkumbo Kwa mazuri
Kwa kujijengea shule,mkisubiri serikali mtakuwa wa mwisho
Huko Kaskazini hasa Knjaro wanajichangisha sana
Then akina Mbowe wakija kwenu wanakuambia msichangie
Lissu kaisha ingia ktk trap hii ya akina Mbowe
Tuchangie elimu jamani
 
Tabora si ndo maana CCM wanashinda asilimia 100 kila uchaguzi
tukipata hizo high school 10 na ccm inakufa
CCM inashinda sana sehemu zenye elimu duni
Luckly,Watu wa mwambao wa Pwani nowdays wanaikataa CCM
CCM inasumbuka sana mwambao wote wa Pwnai Toka Zanzibar,Tanga,Dar,Lindi na Mtwara
Lkn huku Bara wakikunyima elimu halafu Mnyamwezi akimuoa mnyamwezi mwenzake basi hao ni CCM
 
Back
Top Bottom