TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

Aug 9, 2016
13
67
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Kigoma ujiji chini ya Uongozi wa Mheshimwa Zitto Zuberi Kabwe Zitto

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Kigoma Ujiji.

Katika Warsha ya Kigoma, Mh. Zitto aliongeza ahadi mbili zaidi alizoahidi nazo zitaenda sambamba na nne zilizokubaliwa na wananchi ndani ya mradi huu.

Tushirikishane Kigoma.jpg

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Ujiji Mh. Zitto Kabwe (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Maxence Melo (Kushoto)wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane yakiwa yameshuhudiwa na Meya wa Manisapaa ya Kigoma mjini(katikati)

TUSHIRIKISHANE – AHADI ZA MBUNGE

KIGOMA UJIJI
1. Kuhakikisha kwamba Manispaa ya Kigoma Ujiji inajenga kilometa 20 za barabara za mawe/pavements na Lami kwa lengo la kusafisha mji na kuzalisha ajira kwa vijana.

2. Kuboresha mazingira ya Biashara, kuondoa kero ya ushuru Kwa wafanyabiashara wadogo Kwa mujibu wa Sheria ndogo za Manispaa na kujenga Bandari(Jetty) mpya eneo la Forodha ya Ujiji ili kurudisha hadhi ya mji wa Ujiji, na Bandari ya Kibirizi.

3. Kuhamasisha na kusaidia urasimishaji wa vikundi vya uzalishaji mali vya Wananchi (wavuvi, kina mama, wakulima wa bustani, waendesha vyombo vya usafiri n.k) na kuviunganisha na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuchangia sehemu ya michango yao ili wapate mafao yao kama mikopo nafuu na Bima ya afya. 50% ya Bajeti ya Mfuko wa Mbunge itachangia Mfumo wa Hifadhi ya Jamii wa Manispaa.

4. Kukamilisha mradi mkubwa wa maji ili kumaliza tatizo la maji na kusimamia kikamilifu uboreshwaji wa elimu katika Manispaa; kuboresha chuo cha VETA, kuanzisha High School 2 na kuboresha shule za msingi

NYONGEZA YA AHADI
1. Kuendelea kuwatetea watu wa Kigoma dhidi ya unyanyasaji kuhusu uraia wao na kupunguza kwa kiwango kikubwa manyanyaso hayo na kuhakikisha kuwa mkoa wa kigoma unakuwa kati ya mikoa ya kipaumbele katika kupata vitambulisho vya uraia.

2. Kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na upatikanaji wa Samani na Wenyeviti wa Baraza la Ardhi la Wilaya na kuweka mazingira mazuri kwa mabaraza ya ardhi ya kata.

Mada hii itatumika zaidi na Wana Kigoma Ujiji kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Zitto Kabwe (Zitto )
2. Katibu wa Mbunge, Deogratius W. Dongwe (@Deomageni2810)
3. Afisa habari Kigoma, Wiston Mogha Wistonmogha
4 Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Kigoma Ujiji.

Karibuni.

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Kigoma[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

Akaunti za mradi wa Tushirikishane katika mitandao ya Kijamii:

Tushirikishane (@tushirikishane) • Instagram photos and videos

Tushirikishane | Facebook

Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter
 
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Kigoma ujiji chini ya Uongozi wa Mheshimwa Zitto Zuberi Kabwe Zitto

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Kigoma Ujiji.

Katika Warsha ya Kigoma, Mh. Zitto aliongeza ahadi mbili zaidi alizoahidi nazo zitaenda sambamba na nne zilizokubaliwa na wananchi ndani ya mradi huu.

View attachment 415881

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Ujiji (Mh. Zitto Kabwe) na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media (Maxence Melo) wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane yakiwa yameshuhudiwa na Meya wa Manisapaa ya Kigoma mjini

TUSHIRIKISHANE – AHADI ZA MBUNGE

KIGOMA UJIJI
1. Kuhakikisha kwamba Manispaa ya Kigoma Ujiji inajenga kilometa 20 za barabara za mawe/pavements na Lami kwa lengo la kusafisha mji na kuzalisha ajira kwa vijana.

2. Kuboresha mazingira ya Biashara, kuondoa kero ya ushuru Kwa wafanyabiashara wadogo Kwa mujibu wa Sheria ndogo za Manispaa na kujenga Bandari(Jetty) mpya eneo la Forodha ya Ujiji ili kurudisha hadhi ya mji wa Ujiji, na Bandari ya Kibirizi.

3. Kuhamasisha na kusaidia urasimishaji wa vikundi vya uzalishaji mali vya Wananchi (wavuvi, kina mama, wakulima wa bustani, waendesha vyombo vya usafiri n.k) na kuviunganisha na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuchangia sehemu ya michango yao ili wapate mafao yao kama mikopo nafuu na Bima ya afya. 50% ya Bajeti ya Mfuko wa Mbunge itachangia Mfumo wa Hifadhi ya Jamii wa Manispaa.

4. Kukamilisha mradi mkubwa wa maji ili kumaliza tatizo la maji na kusimamia kikamilifu uboreshwaji wa elimu katika Manispaa; kuboresha chuo cha VETA, kuanzisha High School 2 na kuboresha shule za msingi

NYONGEZA YA AHADI
1. Kuendelea kuwatetea watu wa Kigoma dhidi ya unyanyasaji kuhusu uraia wao na kupunguza kwa kiwango kikubwa manyanyaso hayo na kuhakikisha kuwa mkoa wa kigoma unakuwa kati ya mikoa ya kipaumbele katika kupata vitambulisho vya uraia.

2. Kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na upatikanaji wa Samani na Wenyeviti wa Baraza la Ardhi la Wilaya na kuweka mazingira mazuri kwa mabaraza ya ardhi ya kata.

Mada hii itatumika zaidi na Wana Kigoma Ujiji kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Zitto Kabwe (Zitto )
2. Katibu wa Mbunge, Deogratius (@Deomageni2810)
3. Afisa habari Kigoma, Wiston Mogha Wistonmogha
4 Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Kigoma Ujiji.

Karibuni.

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Kigoma[/HASHTAG]
Itafanyika wapi/eneo gani
 
Karibuni sana wadau wa maendeleo,Viongozi na wanachi katika kujadili mjadala wa maendeleo katika manispaa yetu. Mchango wako wowote unasomwa na mbunge pamoja na madiwani wote na utasaidia katika kuisogeza manispaa mbele zaidi
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 3
Ndugu Wanakigoma salaam!
Katika utekelezaji wa ahadi namba tatu ya kuhamasisha na kusaidia vikundi vya uzalishaji mali vya wananchi(wavuvi,kina mama,wakulima na waendesha vyombo vya usafiri)na kuviunganisha na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuchangia sehemu ya michango yao ili wapate mafao yao kama mikopo nafuu na bima ya afya. 50% ya bajeti hio itachangiwa na manispaa ya kigoma ujiji na mfuko wa mbunge. Tarehe 20/10/2016 Maafisa wa makao makuu toka PSPF walizungumza na wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wa halmashauri ya kigoma ujiji juu ya faida ya hifadhi ya jamii na kuangalia namna bora ya kushirikiana na wananchi wa manispaa hii lengo kuu ni kujenga uwezo kwa madiwani, watumishi na vikundi vya wajasiriamali juu ya mfumo huu. Manispaa itachangia 50% ya kila mwanachama na Bank ya Dunia pia itachangia mfuko huu. Hii ni hatua nzuri kwa halmashauri hii kuwajengea uwezo wa hifadhi ya jamii wananchi katika upatikanaji wa bima ya afya na mikopo kwa wanavikundi.
1477551107850.jpg
1477551134947.jpg
1477551145647.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA TATU
Ndugu wadau wa maendeleo wa mkoa wetu kigoma habarini za asubuhi. Katika muendelezo wa utekelezaji ahadi namba 3 juu ya kusaidia vikundi vya uzalishaji mali vya wananchi kama wavuvi. Hapa ni eneo la KATONGA Bangwe timu ya uwekezaji imefika kuagalia eneo kwaajili ya uendelazaji wa mazao ya ziwani na namna ambavyo watasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya UVUVI hasa injini kwa kuanzisha teknolojia ya injini za solar(umeme wa jua) pichani ni Mbunge Zitto Kabwe, Diwani wa Bangwe(Meya Ruhava) na wawekezaji.
1477555682164.jpg
1477555718684.jpg
1477555740989.jpg
1477555758104.jpg
1477555771126.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA TATU
Ndugu wadau wa maendeleo wa mkoa wetu kigoma habarini za asubuhi. Katika muendelezo wa utekelezaji ahadi namba 3 juu ya kusaidia vikundi vya uzalishaji mali vya wananchi kama wavuvi. Hapa ni eneo la KATONGA Bangwe timu ya uwekezaji imefika kuagalia eneo kwaajili ya uendelazaji wa mazao ya ziwani na namna ambavyo watasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya UVUVI hasa injini kwa kuanzisha teknolojia ya injini za solar(umeme wa jua) pichani ni Mbunge Zitto Kabwe, Diwani wa Bangwe(Meya Ruhava) na wawekezaji.View attachment 425009View attachment 425010View attachment 425011View attachment 425012View attachment 425013
Hili suala jana nimetembelea Katonga nimeona hamasa namna ya wavuvi walivojiwekea vikundi vyao na kujiunga na hifadhi ya jamii ili wapate sola na kuweza kuvua kisasa, nawapongeza sana mtakuwa mmewapunguzi wavuvi gharama za mafuta yalikuwa yanawaumiza sana
 
Wananchi wa kigoma tunashuhudia ahadi ziketelezwa kwa macho yetu Ni furaha sana kwetu Kuwa na Mbunge Zitto na Meya Ruhavya
 
Hili suala jana nimetembelea Katonga nimeona hamasa namna ya wavuvi walivojiwekea vikundi vyao na kujiunga na hifadhi ya jamii ili wapate sola na kuweza kuvua kisasa, nawapongeza sana mtakuwa mmewapunguzi wavuvi gharama za mafuta yalikuwa yanawaumiza sana
Ni jambo jema sana
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA TATU
Ndugu wadau wa maendeleo wa mkoa wetu kigoma habarini za asubuhi. Katika muendelezo wa utekelezaji ahadi namba 3 juu ya kusaidia vikundi vya uzalishaji mali vya wananchi kama wavuvi. Hapa ni eneo la KATONGA Bangwe timu ya uwekezaji imefika kuagalia eneo kwaajili ya uendelazaji wa mazao ya ziwani na namna ambavyo watasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya UVUVI hasa injini kwa kuanzisha teknolojia ya injini za solar(umeme wa jua) pichani ni Mbunge Zitto Kabwe, Diwani wa Bangwe(Meya Ruhava) na wawekezaji.View attachment 425009View attachment 425010View attachment 425011View attachment 425012View attachment 425013
Utekelezaji wa vitendo ndio unaofanya zaidi tuamini utawala huu wa Ndugu Zitto na Act wazalendo wake, huwezi amini baada ya wavuvi kunijuza suala hili nimerudi nami Kigoma kuwekeza kwenye Uvuvi suala la Solar kiukweli ni mkombozi na hifadhi ya jamii imefanya wavuvi waweze kujitegemea mkija kututembelea awamu ijayo mtakuta tuna coldroom kabisa maana mmewafungua watu wa Kigoma kiukweli Mungu atauzidishia utawala huu wa ACTWazalendo
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 1
Halmshauri ya kigoma ujiji imeanza kutekeleza ahadi yake ya kupendezesha mji kwa kujenga sanamu la mgebuka kama kivutio kwenye kata ya Kigoma. Pichani ni Mhe Diwani Hussein Kalyango wa kata ya kigoma akiambatana na mtaalamu wa ujenzi manispaa Ndugu Jumanne Kamuangile wakikagua mradi wa paving Block, Sanamu la Mgebuka na Jumba la mawasiliano ya Utalii (KIGOMA INFORMATION CENTRE) Barabara ya kakolwa km 0.15 kata ya kigoma manispaa ya kigoma ujiji. Mkandarasi M/s Juve construction & general Trading co.Ltd na gharama za mradi huu ni million 77,335,000/=Tshs pamoja na Vat.
1477571227879.jpg
1477571236110.jpg
1477571245295.jpg
1477571256240.jpg
1477571269338.jpg
1477571281575.jpg
1477571290304.jpg
1477571298212.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 1
Ujenzi wa barabara ya mjimwema ya juu kata ya Kigoma kwa kiwango cha changalawe imekamilika kilichobaki ni mifereji ya maji ilikuifanya barabara kuwa imara kupitika kipindi chote masika na kiangazi, Barabara hii ni muhimu kwa wakazi wa mjimwema ya juu na kata ya kigoma tunaomba. Huu ni mwendelezo wa maboresho wa mabarabara za mitaani. Alisema Hussein Kalyango diwani wa Kigoma
1477572920481.jpg
1477572928755.jpg
1477572940083.jpg
1477572947872.jpg
1477572959372.jpg
1477572973772.jpg
1477572985897.jpg
1477572995262.jpg
1477573008475.jpg
1477573017068.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 1
kipengele cha kusafisha mji na kuzalisha ajira kwa vijana. Tar 19/10/2016 Meya wa manispaa ya kigoma Ujiji amefungua mafunzo elekezi ya udhibiti wa Taka kwa wenyeviti wa mitaa 68 iliyopo manispaa ya kigoma ujiji. Ili tuwe na maji safi lazima tuwe na mpango mkakati wa usafi na wajibu wa kiongozi kutekeleza na kusimamia sera na mipango hasa baada ya majadiliano ya leo yapo ya msingi tutapaswa kwenda kuyasimamia ili kuweka mji wetu katika hali ya usafi."Alisema Meya Ruhava" pia aliongeza kuwa wito wangu kwa wanakigoma mjini kila mmoja awe askari wa mwingine ili kudhibiti uchafuzi wa mji wetu.
Lakini pia nimeshuhudia magari yote yataka yametengeneza ajira mpya kwa vijana wa mkoani kigoma kupata ajira ya udereva kwenye kusafisha mji.
1477573980833.jpg
1477573990232.jpg
1477573997890.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 4
Mradi wa Maji Kigoma Ujiji ulikuwa umesimama toka Mwezi March mwaka 2015 ambapo ulipaswa kumalizika. Mradi unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani ( KFW ) na Jumuiya ya Ulaya na kugharimu tshs 32 bilioni. Sasa mradi huo umeanza kutekelezwa baada ya Mbunge kufuatilia Kwa Karibu na kuuliza maswali mbalimbali Bungeni. Mradi ulikuwa sehemu ya ahadi ya za Mbunge na sasa umefikia 80% na utamalizika Mwezi disemba 2016. Pichani ni Mhe Zitto Kabwe Mbunge akiwa na katibu wa mbunge Ndugu deo na picha ya screenshot toka ukurasa wa instagram wa babalevo ikithibitisha ukamilifu wa mradi katika hatua za mwisho.

1477576324600.jpg
1477576335424.jpg
1477576340225.jpg
1477576349209.jpg
1477576360301.jpg
1477576475337.jpg
1477576502047.jpg
1477576520344.jpg
1477576528982.jpg
1477576541388.jpg
 
UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 1
Kwenye hatua za awali mradi wa barabara kata ya mwanga kaskazini chini ya diwani BabaLevo kutoka mabatini inayoungana na barabara ya bibititi imefikia hatua za mwisho na pichani inaonyesha meya Ruhava akiwa kwenye ukaguzi wa mradi huu
1477577592480.jpg
1477577599209.jpg
1477577604777.jpg
1477577616150.jpg
1477577633442.jpg
1477577645256.jpg
 
Back
Top Bottom