TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

hivi hii project ya Kigamboni City imefikia wapi? mwenye update plse!!
 
Habari wakuu, Mradi wa Tushirikishane Kigamboni katika Kuboresha Huduma za Afya, Umewezesha kujenga Chumba cha maabara katika Kituo cha Afya cha Mji Mwema, Sehemu ya kutupa Kondo la Uzazi, Sehemu ya kuchomea Taka ngumu, Upanuzi wa sehemu ya kupumzikia.
Kiga1.JPG

Semu hii imejengwa kwaajili ya kutupa Kondo la Uzazi katika kituo cha Afya cha Mji Mwema Kigamboni.
kiga3.JPG

Hii ni sehemu ya kuchomea taka ngumu katika Kituo cha Afya cha Mji Mwema.
kiga22.JPG

kiga23.JPG

Jengo la Maabara ambalo limejengwa Kwenye Kituo cha Afya cha Mji mwema.
 
Sisi wapanda bajaji hamtutendei haki hata kidogo mnawatisha wenye bajaji Kila siku, mnataka wasipakie abiria ati Hadi kituoni, kwanza vituo vya bajaji havipo,pili mnahama Kila uchao. Hivi kweli nitembee kwa miguu toka feri kufuata bajaji kilometer nzima? Mnatuboa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi mlioko kigamboni tunaomba mseme na NSSF kuhusu swala la upigaji picha darajani,kuna matatizo ambayo yanaendelea hapo darajani ni uonevu mtupu hakuna kibao kinacho kataza au kuonyesha airuhusiwi kupiga picha ila wanakusubiri upige wakukamate na walinzi wa SUMA JKT ndo wamegeuza mradi wao,mimi nilisha wafata uongozi wa NSSF apo darajani wakasema auruhusiwi kupiga picha seheemu ya kukatia tiketi tu ila darajani kwenyewe ruksa lakini SUMA JKT wamegeuza mtaji tena kuna kijana ambae ndo kiongozi wao hao suma jkt apo darajani ndo kinara tena anakujibu nenda kashitaki kokote jana kamuweka mtu chini ya ulinzi kwa masaa 4 bila sababu kwani pale ni kituo cha polisi au?
Daraja alijaja kuwa raana kwetu wakazi wa kigamboni ni manyanyaso sasa wekeni misingi inayo eleweka kama kunasababu za msingi kuto piga picha wekeni vibao sisi sio malaika tujue tu hapa apa ruhusiwi bila kuona alama
Nawasilisha
 
Katika Kituo cha Afya cha Kigamboni, Mradi kunaendelea Ujenzi wa Maabara na Ukarabati wa Sehemu ya Kusubiria Wagonjwa. Vilevile kuna Uboreshwaji wa Sehemu ya Kupitia(Paving), Uboreshaji wa sehemu ya Kusubiria Wagonjwa.
kiga19.JPG
kiga13.JPG

Mafundi wakiendelea na Ukarabati sehemu ya kusubiria Wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni.
kiga20.JPG
kiga8.JPG
kiga12.JPG
kiga7.JPG

Ujenzi wa Maabara Ukiendelea Katika Kituo cha Afya cha Kigamboni.
koga18.JPG

Sehemu ya Paving iliyotengenezwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni.
 
Haya, vyoo ndani ya vituo vya Pantoni, Mbona hamwezi kuwaza ninyi watu? Pantoni Kupanda sh mia mbili, haja ndogo mia mbili, pantoni inachelewa ninabanwa na mkojo mnajipatia fedha ,acheni hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Sidhani kuama umeiona hii habari. "Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo inasimamia huduma za vivuko imeita kikao cha wadau kujadili mapendekezo ya kupandisha nauli za vivuko.

Kikao kinatarajia kufanyika siku ya Jumanne tarehe 1/8/2017.

Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge wa Kigamboni
26.07.2017"

Naomba Uhudhurie pia Mkuu. Wazo lako zuri sana na liweza leta Mabadiliko chanya. Asante.
 
Katika kuboresha huduma za Afya kwa Kigamboni kwenye huu mradi wa Tushirikishane, Limepatikana gari lingine la Wagonjwa(Ambulance). Kwa sasa Jimbo la Kigamboni lina Magari Manne ya Wagonjwa.
kiga5.JPG
kiga17.JPG
kiga6.JPG

kiga 26.JPG
kiga25.JPG
 
VITUO VYA AFYA KIGAMBONI VYAPATA ALAMA ZA JUU ZA UBORA WA HUDUMA

Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba, leo tarehe 28/7/2017 amepokea taarifa ya utafiti wa ubora wa huduma zinazotolewa na vituo mbalimbali vya afya, Zahanati na hospitali zilizopo Kigamboni uliofanywa chini ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.

Akikabidhi taarifa hiyo, mwakilishi kutoka wizara ya afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto Ndg Ruth Ngoni amesema kuwa halmashauri ya manispaa ya Kigamboni imepiga hatua kubwa ya uboreshaji wa huduma za afya ukilinganisha na mwaka jana.

Amesema kuwa mwaka huu jumla ya vituo 13 kati ya 27 vya kutolea huduma za afya vikiwemo vya serikali na binafsi vimepata alama za kuanzia nyota tatu na kuendelea sawa na asilimia 48% huku mwaka jana kilikuwa ni kituo kimoja tu kilichokuwa na alama za nyota tatu sawa na asilimia 5%. Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya vyenye alama za nyota tatu na kuendelea vinafikia asilimia 80% ifikapo Juni 2018.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba mara baada ya kupokea taarifa hiyo amefafanua kuwa Ofisi yake imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma kadri wawezavyo tangu kuanzishwa kwa manispaa hiyo mwaka jana.

Ameongeza kuwa halmashauri ya manispaa ya Kigamboni ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 27 ambapo 17 ni vya serikali na 10 ni vya binafsi, ".....tukiongelea vituo vya kutolea huduma za afya 17 vya serikali tu ambavyo viko chini ya ofisi yangu ambavyo kati ya hivyo 13 vimepata alama za nyota tatu na kuendelea ni sawa na asilimia 76%,.... bado tu asilimia 4% ili tufikie lengo la serikali .....", alisema Mkurugenzi Katemba

Pia Katemba amesema watashirikiana na vituo vya huduma za afya vya binafsi ili pamoja waboreshe huduma zao maana zina athari kwenye matokeo ya ujumla ya manispaa nzima.

Aidha Katemba ametoa rai kwa watendaji wote wa sekta ya afya waliopo chini ya Ofisi yake kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kusisitiza kuwa halmashauri yake itaendelea kuboresha mazingira na vifaa vya kutolea huduma.

Tukio la kukabidhi ripoti hiyo limefanyika Ofisi ya halmashauri ya manispaa ya Kigamboni iliyopo Mji Mwema na kuhudhuliwa na Waganga wakuu kutoka vituo vya afya, DNO, baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri na wanahabari.
 
Mkuu, Sidhani kuama umeiona hii habari. "Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo inasimamia huduma za vivuko imeita kikao cha wadau kujadili mapendekezo ya kupandisha nauli za vivuko.

Kikao kinatarajia kufanyika siku ya Jumanne tarehe 1/8/2017.

Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge wa Kigamboni
26.07.2017"

Naomba Uhudhurie pia Mkuu. Wazo lako zuri sana na liweza leta Mabadiliko chanya. Asante.
Kikao kitakuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kigamboni ni Halmashauri Mpya. Tunarajia ucheleweshaji na urasimu utoaji wa vibali kutokuwepo.
Kama ulipeleka maombi yako Temeke na haujapata kibali, bado ninaweza kukusaidia. Wasiliana nami.
Tunaomba mawasiliano yako hapa ,e-mail au number ya simu itasaidia sana. Maana hili tatizo la vibari vya ujenzi linakera sana
 
Naomba mrejesho wa suala la usambazajwi wa umeme kwa wakazi wa Mwasonga.
Nimepata habari Mh: Mbunge na mkuu wa wilaya mlifanya mkutano huko wiki iliyopita. Yatokanayo na kikao ni yapi?
Inatia hasira kuona huduma ya UMMA imebinafsishwa na watu binafsi. Haiwezekani umeme ufike kijijini kasha uwekwe kwenye nyumba ya diwani tu na kwenye biashara ya mtu. Wengine tumehangaika Tanesco hadi tumechoka hakuna kinacho eleweka.
 
TAARIFA

Jana tarehe 18 Septemba 2017, Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani (Mb) walifanya ziara ya kukagua miradi ya umeme inayolisha Dar Es Salaam na hususan Kigamboni.

Ziara hii ilijumuisha Kamishna wa Nishati toka Wizara ya Nishati na madini, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, wakurugenzi wa Tanesco, Mameneja wa Tanesco wa Kanda, Mkoa, Wilaya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa.

Dkt Ndugulile akiongozana na Dkt Kalemani walitembelea vituo vya kupoozea umeme vinavyojengwa kwenye maeneo ya Mbagala, Kurasini na Tungi, Kigamboni.

Vile walitembelea eneo linalilokusudiwa kujengwa kituo kikubwa cha umeme eneo la Dege, Somangila.

Dkt Ndugulile alimjulisha naibu Waziri kuhusu changamoto za umeme katika Jimbo la Kigamboni ikiwa ni pamoja na kukatika mara kwa mara kwa umeme, umeme mdogo (low voltage) na kusuasua kwa miradi kwa miradi mipya kutokana na uhaba wa vifaa.

Dkt Kalemani aliahidi kusimamia miradi hii kwa karibu na pia aliwahakikishia wananchi wa Kigamboni kupata umeme wa uhakika ifikapo Disemba, 2017.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza Tanesco kuipatia Tanesco Kigamboni vifaa vinavyohitajika kwa miradi mipya kama vile waya, nguzo na transfoma.

Vile vile, Dkt Kalemani aliwataka Tanesco kuharakakisha mchakato wa ujenzi wa substation utakaogharimu Tsh 5 Bilioni ili ukamilike katika muda uliopangwa ifikapo Machi, 2018.

Aidha, Dkt Kalemani alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya kufunga umeme kwenye vitongoji vilivyorukwa kwenye mradi wa REA II na vile vile maeneo mapya kwenye REA III unatarajia kuanza Januari, 2018.

Dkt Ndugulile alimshukuru Dkt Kalemani kwa kutembelea Kigamboni na kumtaka kusimamia kwa karibu ahadi zake ili wananchi wa Kigamboni waondokane na adha ya umeme inayowakabili kwa sasa.

IMETOLEWA NA OFISI YA MBUNGE WA KIGAMBONI
19.09.2017
 
mimi nina swali moja dr. mkuu wa mkoa wa dar es salaam alitangaza hivi karibuni kuwa mpaka ikifika january mwakani, showroom zote dar es salaam zihamie kigamboni, mbele kidogo ya dar es salaam zoo. sasa hii njia ya ya mwasonga huwa mvua zikinyesha huwa haipitiki, mfano hizi mvua zilizonyesha karibuni tu malori ya cement yalikwama yakashindwa hata kupita na kuzuia njia. sasa showroom zikihamia huko hili swala ya barabara mnalifikiriaje?
 
Hongera sana mheshimiwa mbunge wetu Dr. Ndugulile kwa kuteuliwa kuwa naibu waziri. Naamini hii ni chachu nyingine kwako katika kuharakisha maendeleo ya jimbo letu. Tafadhali naomba kukukumbusha kero zetu wakazi wa mwasonga. Umeme. Upo kijijini ila transformer na usambazaji ndio issue. Wananchi tunautaka lakini tanesco hawaeleweki
 
Dr F. Ndugulile:

1. Mahitaji ya umeme kwa Kigamboni ni makubwa sana

2. Laini ya Kigamboni inalisha pia Mbagala na Mkuranga SULUHU

3. Kigamboni kuungwa na vituo vya Mbagala na Kurasini. Tatizo kupungua ifikapo Feb, 2018

4. Ujenzi wa Substation ya Kigamboni umeanza Dege kukamilika Juni, 2018
 
Back
Top Bottom