Mjadala wa Mikoa Masikini Waligawa Bunge

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
TAKWIMU kuhusu mikoa mitano masikini zaidi nchini, zimezidi kuzua mjadala bungeni huku wabunge wakizitumia kutaka misaada zaidi katika mikoa yao na wengine wakidai zinawafanya wahofu kwamba kuna ajenda ya siri kwani hawaamini usahihi wake.

Katika mjadala wa jana kuhusu bajeti inayopendekezwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, aliyeanza kulalamikia takwimu hizo na kukataa kuunga hoja hiyo ya serikali ni Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengelwa.

Mbunge huyo wa CCM alisema katika utafiti wake, amegundua kwamba waziri alipata takwimu hizo kutoka halmashauri, lakini akasema yeye ametafiti na kugundua kwamba kamwe Pwani haiwezi kuuzidi mkoa wa Mwanza kwa utajiri kama takwimu hizo zinavyoonesha.

Alisema takwimu hizo zinaonesha kana kwamba mkoa wa Pwani, una hali nzuri wakati si kweli, kwani hali ni mbaya, vyama vya msingi takribani vyote vimeanguka na kwamba anapata hisia kuwa takwimu hizo, zimetumiwa kuinyima Pwani mambo mengi katika bajeti inayopendekezwa.

“Rufiji, kwa mfano haijawahi hata kupelekewa trekta… Hali ni mbaya na hata bajeti kwa ajili ya kuinua kilimo Rufiji hakuna. Mimi kama mwanasheria niko tayari kuapa kuonesha kwamba takwimu alizotumia Waziri si sahihi,” aling’aka.

Naye Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM), alisema anadhani mkoa wa Pwani umewekwa kwenye kundi la mikoa tajiri kwa bahati mbaya, kwani akitazama kila kitu hakiendi vizuri.

“Hata korosho ambalo ndilo zao kuu la biashara mkoa wa Pwani tuko chini, hatuwezi kulingana na wenzetu wa Lindi au Mtwara,” alisema na kutaka waziri aeleze vigezo vilivyotumika kuainisha mikoa yenye hali mbaya kiuchumi nchini na yenye hali nzuri.

Lakini Mbunge wa Nyamagana mkoa wa Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuanza kwa kuupa mkoa huo Sh milioni 50 zilizoahidiwa katika kila kijiji ili wananchi wa mkoa huo wapunguze ‘umasikini wao’.

“Ninaomba hizi shilingi milioni 50, zianzie katika mikoa iliyoainishwa kuwa masikini kwa mujibu wa takwimu za waziri ukiwemo mkoa wangu wa Mwanza,” alisema Mabula.

Naye Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jason Rweikiza alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuwaondolea wakulima wa kahawa kodi 26 wanazolazimika kulipa pamoja na kudhibiti ugonjwa wa mnyauko unaoshambulia migomba ili kuwaokoa wananchi wa Kagera na umasikini.

“Kahawa inakatwa kodi 26, kwa nini wananchi wasiwe masikini? Migomba inaelekea kumalizika kabisa kwa sababu ya ugonjwa wa mnyauko, kwa nini wananchi wasiwe masikini,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Maria Kangoye anayewakilisha mkoa wa Mwanza alipinga takwimu zinazoonesha kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini nchini.

Alisema takwimu za Benki Kuu (BoT) zinaonesha kwamba Mwanza ni mkoa wa pili nyuma ya Dar es Salaam katika kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitaja mikoa masikini zaidi kuwa ni Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza; wakati mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umasikini nchini.

Akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa (CCM), alisema utafiti kuhusu kipato cha kaya, umebaini mikoa mitano inayokabiliwa na umasikini uliokithiri na kumtaka Majaliwa kueleza serikali itafanya nini katika mikoa hiyo ili iondokane na aibu wakati ina fursa za kiuchumi ikiwemo kilimo cha pamba, mibuni na michikichi.

Majaliwa alisema serikali haijaacha jambo hilo kama lilivyo, bali imekuwa ikishawishi wananchi kujianzishia miradi na wengine waunde vikundi, ikiwemo vya Vicoba ili kujijengea mtaji wa pamoja ili waanzishe miradi hiyo.

Alisema kwa Tanzania msingi mkubwa wa kuondokana na umasikini ni kilimo na maeneo ya kulima yapo, ndio maana Serikali inasema ‘Hapa Kazi Tu’ ili watu wajikite katika kilimo.
 
bunge-dodoma.jpg

Lakini Mbunge wa Nyamagana mkoa wa Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuanza kwa kuupa mkoa huo Sh milioni 50 zilizoahidiwa katika kila kijiji ili wananchi wa mkoa huo wapunguze ‘umasikini wao’. “Ninaomba hizi shilingi milioni 50, zianzie katika mikoa iliyoainishwa kuwa masikini kwa mujibu wa takwimu za waziri ukiwemo mkoa wangu wa Mwanza,” alisema Mabula.

Naye Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jason Rweikiza alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuwaondolea wakulima wa kahawa kodi 26 wanazolazimika kulipa pamoja na kudhibiti ugonjwa wa mnyauko unaoshambulia migomba ili kuwaokoa wananchi wa Kagera na umasikini.

“Kahawa inakatwa kodi 26, kwa nini wananchi wasiwe masikini? Migomba inaelekea kumalizika kabisa kwa sababu ya ugonjwa wa mnyauko, kwa nini wananchi wasiwe masikini,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Maria Kangoye anayewakilisha mkoa wa Mwanza alipinga takwimu zinazoonesha kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini nchini.

Alisema takwimu za Benki Kuu (BoT) zinaonesha kwamba Mwanza ni mkoa wa pili nyuma ya Dar es Salaam katika kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitaja mikoa masikini zaidi kuwa ni Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza; wakati mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umasikini nchini.

Akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa (CCM), alisema utafiti kuhusu kipato cha kaya, umebaini mikoa mitano inayokabiliwa na umasikini uliokithiri na kumtaka Majaliwa kueleza serikali itafanya nini katika mikoa hiyo ili iondokane na aibu wakati ina fursa za kiuchumi ikiwemo kilimo cha pamba, mibuni na michikichi.

Majaliwa alisema serikali haijaacha jambo hilo kama lilivyo, bali imekuwa ikishawishi wananchi kujianzishia miradi na wengine waunde vikundi, ikiwemo vya Vicoba ili kujijengea mtaji wa pamoja ili waanzishe miradi hiyo.

Alisema kwa Tanzania msingi mkubwa wa kuondokana na umasikini ni kilimo na maeneo ya kulima yapo, ndio maana Serikali inasema ‘Hapa Kazi Tu’ ili watu wajikite katika kilimo.
 
PICHA%2B22.JPG

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa asilimia 48.9, ukifuatwa na Geita (asilimia 43.7), Kagera (asilimia 39.3), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3).
Dk. Mpango aliendelea kueleza kuwa, mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na ahueni ya asilimia 5.2 ya umaskini wa kipato, ukifuatia Kilimanjaro na Pwani (yote asilimia 14.7) na Manyara (asilimia 18.3). Hayo yote aliyasema akiwa anawasilisha bajeti yake.
Katika mjadala wa jana kuhusu bajeti inayopendekezwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, aliyeanza kulalamikia takwimu hizo na kukataa kuunga hoja hiyo ya serikali ni Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengelwa.Alisema takwimu hizo zinaonesha kana kwamba mkoa wa Pwani, una hali nzuri wakati si kweli, kwani hali ni mbaya, vyama vya msingi takribani vyote vimeanguka na kwamba anapata hisia kuwa takwimu hizo, zimetumiwa kuinyima Pwani mambo mengi katika bajeti inayopendekezwa
“Rufiji, kwa mfano haijawahi hata kupelekewa trekta… Hali ni mbaya na hata bajeti kwa ajili ya kuinua kilimo Rufiji hakuna. Mimi kama mwanasheria niko tayari kuapa kuonesha kwamba takwimu alizotumia Waziri si sahihi,”
Lakini Mbunge wa Nyamagana mkoa wa Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuanza kwa kuupa mkoa huo Sh milioni 50 zilizoahidiwa katika kila kijiji ili wananchi wa mkoa huo wapunguze ‘umasikini wao’.

“Ninaomba hizi shilingi milioni 50, zianzie katika mikoa iliyoainishwa kuwa masikini kwa mujibu wa takwimu za waziri ukiwemo mkoa wangu wa Mwanza,” alisema Mabula.

Mbunge wa Viti Maalumu, Maria Kangoye anayewakilisha mkoa wa Mwanza alipinga takwimu zinazoonesha kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini nchini.
Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopita pia serikali ilitoa taarifa za kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato licha ya kuwa makao makuu ya mkoa ni Geita na hakuna uwanja wa maana jambo lililolalamikiwa na wadau kwamba ni dalili za upendeleo.
Nini maoni ya wana JF katika hili katika kuhakikisha kumbukumbu sahihi zinawekwa?
 
TAKWIMU kuhusu mikoa mitano masikini zaidi nchini, zimezidi kuzua mjadala bungeni huku wabunge wakizitumia kutaka misaada zaidi katika mikoa yao na wengine wakidai zinawafanya wahofu kwamba kuna ajenda ya siri kwani hawaamini usahihi wake.

Katika mjadala wa jana kuhusu bajeti inayopendekezwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, aliyeanza kulalamikia takwimu hizo na kukataa kuunga hoja hiyo ya serikali ni Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengelwa.

Mbunge huyo wa CCM alisema katika utafiti wake, amegundua kwamba waziri alipata takwimu hizo kutoka halmashauri, lakini akasema yeye ametafiti na kugundua kwamba kamwe Pwani haiwezi kuuzidi mkoa wa Mwanza kwa utajiri kama takwimu hizo zinavyoonesha.

Alisema takwimu hizo zinaonesha kana kwamba mkoa wa Pwani, una hali nzuri wakati si kweli, kwani hali ni mbaya, vyama vya msingi takribani vyote vimeanguka na kwamba anapata hisia kuwa takwimu hizo, zimetumiwa kuinyima Pwani mambo mengi katika bajeti inayopendekezwa.

“Rufiji, kwa mfano haijawahi hata kupelekewa trekta… Hali ni mbaya na hata bajeti kwa ajili ya kuinua kilimo Rufiji hakuna. Mimi kama mwanasheria niko tayari kuapa kuonesha kwamba takwimu alizotumia Waziri si sahihi,” aling’aka.

Naye Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM), alisema anadhani mkoa wa Pwani umewekwa kwenye kundi la mikoa tajiri kwa bahati mbaya, kwani akitazama kila kitu hakiendi vizuri.

“Hata korosho ambalo ndilo zao kuu la biashara mkoa wa Pwani tuko chini, hatuwezi kulingana na wenzetu wa Lindi au Mtwara,” alisema na kutaka waziri aeleze vigezo vilivyotumika kuainisha mikoa yenye hali mbaya kiuchumi nchini na yenye hali nzuri.

Lakini Mbunge wa Nyamagana mkoa wa Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuanza kwa kuupa mkoa huo Sh milioni 50 zilizoahidiwa katika kila kijiji ili wananchi wa mkoa huo wapunguze ‘umasikini wao’.

“Ninaomba hizi shilingi milioni 50, zianzie katika mikoa iliyoainishwa kuwa masikini kwa mujibu wa takwimu za waziri ukiwemo mkoa wangu wa Mwanza,” alisema Mabula.

Naye Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jason Rweikiza alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuwaondolea wakulima wa kahawa kodi 26 wanazolazimika kulipa pamoja na kudhibiti ugonjwa wa mnyauko unaoshambulia migomba ili kuwaokoa wananchi wa Kagera na umasikini.

“Kahawa inakatwa kodi 26, kwa nini wananchi wasiwe masikini? Migomba inaelekea kumalizika kabisa kwa sababu ya ugonjwa wa mnyauko, kwa nini wananchi wasiwe masikini,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Maria Kangoye anayewakilisha mkoa wa Mwanza alipinga takwimu zinazoonesha kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini nchini.

Alisema takwimu za Benki Kuu (BoT) zinaonesha kwamba Mwanza ni mkoa wa pili nyuma ya Dar es Salaam katika kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitaja mikoa masikini zaidi kuwa ni Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza; wakati mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umasikini nchini.

Akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa (CCM), alisema utafiti kuhusu kipato cha kaya, umebaini mikoa mitano inayokabiliwa na umasikini uliokithiri na kumtaka Majaliwa kueleza serikali itafanya nini katika mikoa hiyo ili iondokane na aibu wakati ina fursa za kiuchumi ikiwemo kilimo cha pamba, mibuni na michikichi.

Majaliwa alisema serikali haijaacha jambo hilo kama lilivyo, bali imekuwa ikishawishi wananchi kujianzishia miradi na wengine waunde vikundi, ikiwemo vya Vicoba ili kujijengea mtaji wa pamoja ili waanzishe miradi hiyo.

Alisema kwa Tanzania msingi mkubwa wa kuondokana na umasikini ni kilimo na maeneo ya kulima yapo, ndio maana Serikali inasema ‘Hapa Kazi Tu’ ili watu wajikite katika kilimo.
Mimi nilishaiona hii kwenye ile thrd yako ya nyuma. Kama wewe ni mbunge basi naomba uamini tuko wengi nje ya Bunge tunaoyaona mambo kama hayo mapema sana. Mukitutumia tutaisaidia nchi. Huwezi ukapanga mikoa maskini kwa takwimu wakati huo kwa uwazi wa macho unaona kabisa kwamba mikoa tajiri inafahamika. Niliwahi kuweka komenti hii:
Kumbe wewe hujui? Tukishaweka takwimu za aina hiyo, sasa tumepata kisingizio cha kuwapa umuhimu wananchi wa mikoa hiyo ktk bajeti ili kupunguza 'umaskini'.

Sasa usiulize kwa nini tunapeleka miradi mingi ktk mikoa hiyo.
 
hahaha! jamaa anataka apeleke kila kitu kwao kwa kisingizio!
Kati ya mikoa 5, ukiondoa pwani mikoa 4 ni kambi za upinzani!
Kwa takwimu za TRA mkoa maskini wa Mwanza ni mkoa wa ,2 kwa kulipa kodi! Hawa maskini wanaolipa kodi kiasi hiki sijui wanauza nini ambacho faida yake yote imehama kuwa kodi!
Jiji kubwa la pili nchini, eti linazidiwa na Manyara, kijiji kilichopewa hadhi ya mkoa?
Eneo lililopewa sifa za umaskini mkubwa pia ndilo lililotoa mawaziri wengi kwa uwiano ktk awamu hii!
Lkn kama Geita maskini kwanini sasa pesa zipelekwe kujenga uwanja wa ndege badala ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi?
Yaani vitu ni mkanganyiko kwa kweli!
Kweli tutaisoma namba....!
 
inabidi tuwe na formula ya wazi ya jinsi ya kugawana pesa za maendeleo.
Nahisi tunaweza kuwa na mgogoro mkubwa sana hapo baadae!
Toka nchi hii iumbwe hatukuwahi kuwa na matabaka ya namna hii, ndio yanaanza sasa!
Ule utawala wa majimbo nadhani ndio unataka kuanza rasmi!
Haiingii akilini, jimbo hili moja la kanda ya ziwa eti ndilo likawa linahitaji kusaidiwa!!!
Nadhani hata mpango wa kuchukua pesa za halmashauri na kuzitawanya nchi nzima kupitia TRA sio mpango mwema!
 
Hili jamaa bana wataalamu wa mipango limewaloga, wanasheria ndio usisema hata hongo!! halafu linapigana na ufisadi et
mimi ni wa wote ccm, chadema act, naomba mniombee.....hakuna joka kubwa kama hili, ila naona watu wameanza kuona rangi yake taratibu
 
Back
Top Bottom