Mjadala wa Kisiasa kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
EUROPEAN UNION
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
11/Desemba/2013,
MJADALA WA KISIASA KATI YA UMOJA WA ULAYA (EU) NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) ULIOFANYIKA ARUSHA.


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mabalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa baraka za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamefanya mjadala wa kisiasa, mjini Arusha siku ya Jumanne, tarehe 10/12/2013.

Mjadala huo wa kisiasa umefanyika katika misingi ya Makubaliano ya Cotonou yaliyofanyika kati ya Umoja wa Ulaya na majimbo ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP). Mashirika ya Kikanda pia yamejumuishwa katika mchakato huu.

Pande zote zilichanganua dhana ya kisiasa katika nchi za kusini na kujadili hatua za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika suala la utawala, kuzuia mapigano, Ushiriki wa EAC katika amani ya Umajumui wa Afrika na Usanifu wa usalama, pamoja na vipengele vya msaada wa Umoja wa Ulaya katika maeneo hayo. Vile vile, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya walizungumzia mipango ya chaguzi katika nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki na mipango ya baadae ya kusimamia chaguzi kwenye nchi washarika.

Pia wamezungumzia juhudi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya na silaha ndogo ndogo. Pande zote mbili zilitoa mitazamo yao kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai (ICC).

Mwishoni Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya wamejadili kuhusu mahusiano ya kibiashara, ikiwemo hatima ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya kambi hizo mbili. EAC na EU wamethibitisha azimio la kufanya kazi kwa pamoja katika kukuza amani na uthabiti, na kuendeleza ukuaji barabara katika eneo hilo. Wamesisitiza azma yao katika ushirikiano na majadiliano ili kuongeza nguvu ya ajenda ya mjumuiko wa kikanda, EAC.

Mkutano huo uliendeshwa na wenyekiti wawili, Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC) na Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania. Vile vile mkutano huu ulihudhuriwa na Mabalozi na wawakilishi kutoka Balozi za Ubelgiji, Denmark, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Hispania, Sweden, na Uingereza pamoja na viongozi waandamizi kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

For more information, please contact:

Mr. Tom Vens, Head of Political Press and Information
Section Delegation of the European Union to Tanzania
Email: Tom.VENS@eeas.europa.eu
Direct Line: +255 22 2164503
Website: European Union - EEAS (European External Action Service) | Delegation in Tanzania
Facebook: https://www.facebook.com/EuropeanUnionTanzania



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…