Kumbe tunayoyaandika hapa yanawafumbua macho Watanzania wengi katika sakata hili la ufisadi wa Richmond/Dowans. Hongera sana WanaJF. Mpaka kufikia kutajwa katika majadiliano makubwa kama haya si kazi ndogo na umaarufu wa JF ndiyo utazidi kuongezeka popote pale walipo wabongo duniani.
huyu mzee mkinga akikaa na mtikila wataanzisha kanisa kubwa kuliko hata la kakobe. Mzee anaongea kwa uhakika bila woga utadhani alikuwepo.... Kweli huyu mzee ni noma!
Tanzania iko mbioni kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wana JF tafadhali nisaidieni katika hili. Ni suala la ufisadi ndilo litakalotufikisha huko ama udini?. Na tufanyenini ili kuweza kuepuka janga hilo?
Mnatumia theory za relativity kumhukumu Rais. Hata kama kuna blunders zimefanyika hapa, lakini nchi ina sheria, kanuni na taratibu katika maamuzi.
Je, mwanasheria mkuu au ngeleja wana mamlaka ya kupitisha ulipwaji wa DOWANS? Nani ana uhakika kama DOWANS watalipwa au hawatalipwa bila kupitishwa na Bunge?[/QUO
Serikali inasema italipa unasubiri uambiweje ili uamini kwamba watalipa! Hakuna cha Baraza la mawaziri wala Bunge lililopitisha hiki kitu na hapo ndio uone Mkwere anatupeleka wapi!
He will speak when he has something to say, not speaking because you want him to say something.
Anasubiri taarifa toka kwa watendaji wake ili awe na cha kusema.
Serikali haiendeshwi kwa pressure toka kwa anonymous mtandaoni.
wanaojua sheria, hivi kuna uwezekano wa kuifungulia kesi mahakama iliyoamua kesi ya DOWANS Vs Tanesco, maana inaonekana kana kwamba hjiyo kesi iliamuliwa kihuni na bila kufuata utaratibu, ni nani hasa aliyefungua hiyo kesi?
Naamini elimu ya kutosha tuliyonayo wana JF inachangia uzito ingawa kuna mapandikizi wanaojaribu kuvuruga umakini wa hoja lakini tunasonga. Big up JF but only for those with constructive contribution to the country.
Ni rais asiye na hekima ndiye anayeweza kuendelea na baraza la mawaziri lenye misimamo tofauti kuhusu suala zito kama la Dowans.
Nyie watu mbona mmeshindwa kupiga simu kutetea hoja zenu? wazungumzaji wamezungumza hoja zao na walisubiri mpige simu kupeleka hoja zenu na mkanyamaza kimya. Alaaaaaaaaaa
Tamko:
Jibu ni moja kama utafanya maamuzi magumu: USIIPIGIE KURA CCM, CHAGUA SERA KULINGANA NA WAKATI. MFANO, SERA YA SASA NI KUIBADILI KATIBA ILI IKUTUMIKIE VYEMA KAMA MTZ. HAPO VIPI!