Mizengo Pinda: Mshahara wangu kama Waziri Mkuu hauzidi Shilingi milioni sita (6)

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,667
925
Waziri Mkuu amedai bungeni muda huu kwamba mshahara wake hauzidi Tsh. 6mil na akadai wanaodai analipwa zaidi ya hapo ni uzushi mkubwa kiasi kwamba yeye ni mkopaji tu katika mabenki na kuwa mshahara huo ni pamoja na mapato ya mkewe.

Source: leo bungeni -tbc

 
anasema yeye ni mkopaji mzuri wa mabenki haya pinda amepinda kweli
 
Akijibu swali gumu sana la Habib Mnyaa waziri mkuu kasema mshahara wake ni miioni sita kwa mwezi na tofauti kati ya mshahara wake na rais haizidi milioni moja.
Wenye data njooni mtwambie kama kadanganya tumshitaki kwa umma.
 
Akijibu maswali ya papo kwa papo, Mh. Waziri Mkuu amesema anapata take home ya shng. milioni 6 za tz.. Anasema mshahara wake na wa Mh. Rais na makamu wake, hauna tofauti kubwa, haizidi tshng. Mil. 1.. Amemjibu Zito kwamba kwa kutaja uongo kiasi cha mshahara wake, Mungu atamhukumu.

Kaongezea kwamba yeye ni kati ya viongozi wanaokopa sana mabenki, pale maisha yanapomzidia. Na juzi juzi amechukua mkopo CRDB na NMB..
 
kwani si walisema ni siri?mta mada naona unaendelea kumuhukumu ZZK
 
Mh. Pinda atapotea akitaka kushindana kwa hoja na Mh. Zitto.
 
je waziri mkuu analidanganya bunge au Zitto aliropoka?
ukweli uwapi?
 
Akijibu swali gumu sana la Habib Mnyaa waziri mkuu kasema mshahara wake ni miioni sita kwa mwezi na tofauti kati ya mshahara wake na rais haizidi milioni moja.
Wenye data njooni mtwambie kama kadanganya tumshitaki kwa umma.

Kudanganya au kusema uwongo
 

Anakopa bank kwa kuwa mshahara haumtoshi??.............. sasa hizo bank zinatumia vigezo gani kumkopesha maana inavyoonekana ana struggle sasa sijui atazilipaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…