Mivutano yaanza kuzuka ndani ya UKAWA

Mivutano yaanza kuzuka ndani ya UKAWA

Huyu Mwanadiwani ni mganga wa kienyeji? Maana hii huwezi kusema kama ni habari, majungu au ramli. Habari za ndani, viongozi wawili, n.k. Habari za ndani wapi? Hao viongozi wawili ni akina nani? Upuuzi mtupu, leta kitu kinachoeleweka ili watu wajadili, siyo hizi riwaya za abunuwasi.

Wanaotaka kurudi na warudi tunajua washanunnuliwa na manyani wenzao, UKAWA itaendelea kuwepo
 
UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.-Hivi ni mji wa Zanzibar au Unguja? Habari Leo nijibuni!
 
Kupitia Bunge la Katiba, wananchi wapenda Taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa UKAWA.

Waingereza wanasema, Birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa Bunge la Katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za Urais (Rais wa Tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge Maalum.

Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.

Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike. Kwa sasa ukweli umeanza kubainika.

Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.

Pesa wanazopata baadhi ya viongozi wa UKAWA ili kusaidia harakati zao za kulimega taifa ndizo zitakuwa sumu ndani ya UKAWA.

Muda huwa ni jibu mbadala.

We mpuuzi badala ya kushugulika na shida za wananchi uko busy na UKAWA. Mfano Leo hii toka asubuhi watu hatuna umeme na nyie MaCCM mlisema mgao wa umeme kuwa historia. Hivi mnadhani tutaendelea kushobokea siasa zenu wakati hospitali ya wilaya ya Kilosa haina hata Panadol na wajawazito wanabebwa na bodaboda?
 
siasa za bongo unaweza ukapata kichaa..
 
WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.

Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.

Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.

“Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha,” anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.

Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.

Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.

Wakati haya yakitokea ndani ya UKAWA, Rais Kikwete ametoa siku nyingine 60 za nyongeza kwa Bunge Maalum la Katiba ili kukamilisha kazi waliyopewa wabunge wa bunge Maalum la Katiba.

Rais Kikwete alisema, “Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.

“Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine,” alibainisha.

Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.

“Wakishindwa kutupa katiba katika muda tuliowapa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni,” alisema bila kufafanua zaidi.
Chanzo: Habarileo.

Interahamwe at work
 
Source: habari leo gazeti la ccm

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mbunge yeyote atakayerejea bungeni kuungana na mainterahamwe kwenye bunge lao la katiba, atakuwa anawakilisha tumbo binafsi ili kufukuzia mshiko wa 300000 kwa siku na sio maslahi ya umma!
 
Huyu Mwanadiwani kwa story za kubuni ndiye mwenyewe. Anatujazia server bure. Nafikiria kumpeleka kwenye ignore list yangu kwani sasa nimechoka kusoma uharo wake hapa.

Tiba

Chanzo cha habari ni gazeti makini linalomilikiwa na serikali, HABARI LEO, na sio mwanadiwani.
 
Huo muda woote uliopoteza kutunga hadithi yako si bora ungetumia kujichua.
 
Kuweweseka huku kunatokana na nini, kama sio uoga? Mwanzoni ilikuwa jeshi linatoa nchi, Mara Oman imejiandaa kurejesha dola ya usultani Pemba, hoja iliyouibuliwa na kudaiwa kudhihirishwa na maelezo ya Bw Duni. Mara kule kanisani Lukuvi akadai uamsho utachukua fursa huko Unguja. Bungeni Sita Akadai eti UKAWA wamerudi bungeni ila ukumbini hawakuwa wameingia kwani walikuwa dirishani wakiwinda posho! Sasa eti UKAWA una ufa!
 
WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.

Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.

Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.

“Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha,” anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.

Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.

Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.

Wakati haya yakitokea ndani ya UKAWA, Rais Kikwete ametoa siku nyingine 60 za nyongeza kwa Bunge Maalum la Katiba ili kukamilisha kazi waliyopewa wabunge wa bunge Maalum la Katiba.

Rais Kikwete alisema, “Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.

“Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine,” alibainisha.

Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.

“Wakishindwa kutupa katiba katika muda tuliowapa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni,” alisema bila kufafanua zaidi.
Chanzo: Habarileo.

Ndug yangu hoja ya msingi hapa si kwenda bungeni kwa kuwa waenfe ama wasiende ,katiba mpya haiwezi kupatikana na suala hili ni aibu kwa Kikwete!
Hoja hapa uchaguzi ujao utafanyika kwa mazingira gani??
Je CCM watapona mtikisiko wa kung'olewa??
 
Unajaza server kwa kuandika mambo ambayo tumeyaweka kando kwasas habari kuu ni Bajeti kama umelipwa ili uwe unaandika habari za UKAWA kila siku tumezichoka.

Ndugu, wewe uko hapa pia unajadili UKAWA halafu unaanza kulalamika kama wanaJF wengine ndiyo wanajikita katika mambo ya Katiba.

Unatakiwa uanzishe mjadala kama unadhani kuna jambo ambalo ni muhimu katika fikra zako zaidi ya mjadala wa Katiba.
 
Huyu Mwanadiwani kwa story za kubuni ndiye mwenyewe. Anatujazia server bure. Nafikiria kumpeleka kwenye ignore list yangu kwani sasa nimechoka kusoma uharo wake hapa.

Tiba
Ndugu, Nidhani hujaisoma habari yote na kama umeisoma yote ungegundua kama hii ni habari kutoka gazeti la kitaifa la Habarileo.
 
Vyombo vya habari vya serikali vinatumika vibaya na ccm. Hii inaonyesha jinsi gani kodi za wananchi zinatumika kwa manufaa kwa wachache. Vipo kimasilai kwa chama tawala. Ndio vyombo vya propaganda kwa ccm
 
Jaman tuwe wakweli ccm wanatutukana wananchi.ile ni katiba ya watu wote sio ya ccm
 
Ndugu, Nidhani hujaisoma habari yote na kama umeisoma yote ungegundua kama hii ni habari kutoka gazeti la kitaifa la Habarileo.

Habari leo ni gazeti au toilet paper ya choon!!? Si ndio hilo lilileta habari ya gari la mbowe halafu maofisa usalama kenya wakakanusha au sio??? Hilo ni gazeti linalo somwa na machangu na mashangingi wa ccm wala rushwa wakubwa na wauza madawa ya kulevya nadhan hata wahariri wake ni wale wana popelewa 0713 na viongozi wa ccm ndio mana hata haliuzikagi hilo
 
Back
Top Bottom