Mivutano yaanza kuzuka ndani ya UKAWA

Mivutano yaanza kuzuka ndani ya UKAWA

Ndugu, nadhani hata unachokiandika hukielewi achilia mbali mhariri na gazeti unalolitaja.

Rejea bandiko langu halafu niambie kati yangu mimi na wewe nani haelewi? Chanzo habari yako unasema ni JAMBALEO! Jambaleo ya akina Le Mutuz na wauza Sembe akina J.p..to haina credibility yoyote ndani ya Jamii yetu... Huwezi kujiandikia cheap propaganda hapa eti kuna ambao wanafaidika na fedha za nje bila ya kutuwekea data za kutosha hapa! Wewe hapo ulipo ukiwekewa TZS 10M wale jamaa wa Anti Money Laundering lazima wataifunga a/c yako kwa muda! Kikosi cha kuzuia fedha chafu hapa bongo wana njaa iliyopitiliza! ... Jipange upya ...
 
chanzo habari leo, naona siku hizi wanabadili propoganda tu kila siku, namuonea huruma sana mhariri wake, maana hafanyi kazi ipasavyo. na hao viongozi wa2 si warudi wao, kwani watakatwa miguu, propoganda nyepesi kama hizi haziwezi kutushika watu wenye akili timamu, labda labda wale wenye akili nusu za kichwani na zingine za tumboni.
 
HabariLeo, haya si ya kwenu, waachieni Tanzania Daima na Uhuru. Ninyi mnapaswa kujitanabaisha kama gazeti la umma lisilokuwa na mtazamo wa propoganda za rejareja.
 
Naona Habari Leo wameamua kuwa bed fellows wa wapinga maoni ya wananchi na kwa kweli wanatumika kweli kweli.

Stori hii ya propaganda nyepesi ni sawasawa na ule uongo uliosemwa bungeni na Samuel Sitta. Yaani mtu mzima kama yule akasema uongo ambao ulikuwa haumtofautishi na mbea mwingine yeyote wa mitaani tena kwenye vilinge vya ususi.

Kwa namna mwenendo wa Habari Leo unavyokwenda kwa kushabikia ukandamizaji na ubezaji wa wananchi unaofanywa na CCM, si ajabu Rais Jakaya Kikwete anahusika katika kutoa maelekezo ili Magazeti hayo ya Serikali yatumike kuharibu mchakato huu kwa maslahi ya CCM.

Kwa nini watumie vyombo vya serikali!?

Kumbe ni habari kutoka kwa Mwigulu Nchemba kupitia gazeti lao la HabariLeo...mie napita!
 
Hizi ni akili za kibavicha!.

Ndugu, kwani wewe kwa sasa umefanya nini?.

Kama hufahamu, hata kuandika tu comment ni kuchangia achilia mbali kugusia mada iliyoko ndani ya thread.

Wewe mpuuzi acha ujinga, onyesha maturity yako acha kusukumwa na tumbo
 
Hii habari iko chini sana kwa gazeti la serikali. Juzi tu limeleta habari kuwa gari la KUB limekamatwa Kenya likihusishwa na ugaidi. Ikabainika ni uwongo,hata polisi Kenya walikanusha,lakini uongozi wa gazeti haukuomba msamaha kwa wasomaji wake. Hili ni gazeti la UDAKU,sambamba na magazeti ya global publishers.
Kama wahariri wake ni Mwigulu,Nape,Wasira et al,tusitegemee habari tofauti.
 
Ni kweli wanainchi tumechoka kusikiliza jambo moja la katiba umefika muda tunataka katiba imalizike pesa za wavuja jasho zinatumika vibaya
 
Niwapongeze tu hao wapinzani waliogundua kuwa CHADEMA haina lengo jema lolote bali ni kuwatumia wapinzani wenzao ili kutimika matakwa yao ya kifedha kutoka ughaibuni.

UKAWA chaliiiii
 
kwani kama wanapata fedha nje kuna tatizo gani hapo?mbona tunadaiwa trillion 40 zote za nje .asiwadanganye mtu yeyote kila mtu anapata fedha nje.hao wanaopata ndani ni za walipa kodi wetu halafu wanazichezea.acheni propaganda jibuni maswala ya msingi yanawahusu wananchi fanyieni kazi mawazo ya wananchi yaliyopo ktk tume ya mabadidiliko .
 
Intarahamwe watahakikisha kila habari mbaya itatungwa dhidi ya UKAWA.

Hii inadhihirisha UKAWA is a pain in Intaharamwe's ass
 
Mipasho hii SI dalili nzuri chamani kwetu. Ukawa umetukalia vibaya kiasi hiki?
 
WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.

Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.

Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.

“Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha,” anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.

Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.

Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.

Wakati haya yakitokea ndani ya UKAWA, Rais Kikwete ametoa siku nyingine 60 za nyongeza kwa Bunge Maalum la Katiba ili kukamilisha kazi waliyopewa wabunge wa bunge Maalum la Katiba.

Rais Kikwete alisema, “Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.

“Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine,” alibainisha.

Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.

“Wakishindwa kutupa katiba katika muda tuliowapa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni,” alisema bila kufafanua zaidi.
Chanzo: Habarileo.

Mimi ni kigogo wa UKAWA napenda kutumia fursa hii kusema kwamba haya maneno hapo juu kuhusu ukawa hayana mashiko na ukweli wowote na kwa ufupi tu ni kwamba sasa tumezidi kupata nguvu ya pamoja na tumeshikamana kweli kweli.

Spidi hii ni mpaka utakapomalizika uchaguzi 2015 kuhakikisha ccm imengoka madarakani.

Kwa sasa ni shida kutengana tumeona ni njia pekee kupambana na ma intarahamwe. Tunaomba dua zenu, tumeanza zanzibar sasa tunaendelea na mikoa ya bara kuueleza ukweli umma wa watanzania. Ahsante
 
Huu Muungano wa UKAWA umekaa kitapeli tapeli, sio rahisi ukaweza kudumu.
 
Hivi watu wanapewa fedha ili waache kazi waliyopewa na wananchi ya kutunga Katiba wewe unaona ni sawa?
kotoka haina maana wamekimbia ni njia mbadala wa kushinikiza jambo maana wangebaki wasingesikika na kueleweka kama sasa....afu for that matter wamechelewa yani walitakiwa waoondeke tangu wengi walivyopitisha kura ya wazi na siri kwapamoja...
 
Back
Top Bottom