Maeneo yenye shida ni mengi na yanazidi kuongezekakweli mdau,na jangwani darajani pia kumeanza kuwa na mashimo.Na mifuniko ya chemba za katikati ya barabara imeanza kudidimia chini hii ni hatari.Hasa kipande cha kisutu mpaka makutano ya mtaa wa samora.Wafanyie kazi mapema kabla maafa hayajatokea
niliahidi kuleta hii mada kuhusiana na hii miundombinu ya barabara ya Strabag/BRT
Ni wazi serikali inapata mapato kwenye hii barabara ambayo ni wazi kuwa iko bado kwenye kipindi cha uangalizi...! Yani mjengaji bado anaifanyia uangalizi kulingana na mkataba lakini hili halizuii serikali kufanya ukarabati udiotokana na mkataba wa ujenzi (naweza kukosolewa kwenye hili
Kwasasa hali si mbaya bado...uharibifu uliopo Kwasasa ni kwenye nguzo za usalama na vizuizi kwa waenda kwa miguu, alama na viashiria vingi vya barabarani, taa za kuongozea magari na taa za usikumsimamizi anayeiwakilisha serikali kwenye hili ni nani? TANROADS? hawayaoni haya matatizo madogo dogo ya ukarabati?
Tunavyoendelea kulivalia macho ya mbao hili litakuja litugharimu mamilioni ya pesa
-vizuizi vingi zaidi vitagongwa bila kubadilishwa
-Taa nyingi zitaungua bila kubadilishwa huku nyingine zikigongwa
-milango ile ya vioo inaweza kugongwa na kupasuka bila kubadilishwa
-mashimo madogo hayatazibwa na yataongezeka mpaka kuwa makubwa kabisa
Barabara itazeeka kabla ya wakati wake! Kama serikali inaona ni gharama kuisimamia hii barabara basi iikatie bima kubwa
Mradi wa mabilioni unapopewa matunzo duni inasikitisha mno
Nchi ya watu wadogo, taifa la kitu kidogo....huu mfumo hautaondoka kwa kutumbua na kubadili teuzi bali katiba pendekezwaHizi dosari ndogo ndogo ni very cheap kuzirekebisha lakini watendaji hawapendi kuzifanyia kazi kwakuwa 10% yake ni almost negligible kwahiyo watasubiri iongezeke ndipo wainuke
Maana, naona planning ya miundombinu ni kama ya muda mfupi,isiyozingatia ukuaji wa miji. Mfano kipande cha barababa toka ubungo mpaka mlandizi kilijengwa kwa njia mbili kuishia kimara, na kadhia iliyojitokeza wote tuliona ile misururu ya foleni. Na leo tunaona BRT imeishia kimara, wakati dsm imeshaungana na kibaha kimakaazi.Mwaka jana tulikuwa na moja ila ni sahihi kuna uhitaji mkubwa kwenye hili
Hebu ngoja hili nalo tulitengenezee mjadalaMaana, naona planning ya miundombinu ni kama ya muda mfupi,isiyozingatia ukuaji wa miji. Mfano kipande cha barababa toka ubungo mpaka mlandizi kilijengwa kwa njia mbili kuishia kimara, na kadhia iliyojitokeza wote tuliona ile misururu ya foleni. Na leo tunaona BRT imeishia kimara, wakati dsm imeshaungana na kibaha kimakaazi.
Unaona hiyo changamoto?